SIMULIZI ZA JOSHUA / 8 months ago
JIJI LA KICHAWI 3
0713111547
Akiwa amejilaza haikupita nusu saa ,alisikia kitanda kikitetemeka ,kitanda kilitetemeka sana mithili ya tetemeko la dunia ,isaya alitaka kuamka aangalie kuna nini alipoinua mgongo alishikiliwa kwa nguvu sana kama chuma inasavyo sumaku alitaka kupiga kelele mdomo nao ulinata kama umewekewa superglue(gundi)
Isaya alikuwa njia asijue cha kufanya zaidi ya kutulia kimya kusubiri hukumu yake ,akiwa bado kitandani alisikia vicheko vya watu wasioonekana
``hahahahahhahahahahah huhuuuuuuuuuu’’
Zilikuwa ni sauti za wanawake wakicheka sana ,isayaalitetemeka sana alijaribu tena kusimama alirudishwa chini alikuwa akivutwa na kamba za kichawi ,
Ilipita kitambo kidogo isaya akiwa anajigaragaza kitandani huku akisikia maumivu makali sana kwa kamba alizokuwa amefungwa
Isaya alilia na kulowanisha godoro lake kwa machozi ,alijaribu tena kuongee kwa mara hii sauti yake ilitoka kwa nguvu alisema
``kama mnaniua si mniueeeee nimechokaaaaa aaaaa’’
Sauti za watu wakicheka zilijirudia tena
``hahahahaahhahahahh huuuuuuuuhuuuu’’
Isaya aliishiwa na nguvu kabisa mwili ulilegea ,alikua akipambana sana kuondoa kamba zilizokuwa zimemshikilia mwilini ,baada ya dakika kama kumi alijisikia huru sasa ila alikua na uchovu mwingi sana
Isaya aliamka na kuchukua kopo kubwa la maji kisha akanywa ,alijisemea mwenyewe
``hii nyumba silali tena lazima niondoke nitakufa mimi jamani’’
Alirudi kitandani na kujilaza tena kwani alikua na uchovu sana kutokana na masumbufu ya siku ile
Kesho ilipofika isaya aliamka na kuelekea kazini ,alichukua gari akiwa na kondakta wake sharifu kwa ajili ya kuwasaka abiria ,isaya alitamani sana kumwadithia sharifu yaliyotokea jana usiku ,akiwa anataka kumwadithia alihisi kama kitu kikimwambia aache ,isaya alijikuta akishindwa kumwadithia sharifu yaliyomkuta
Gari liliendeleza ruti zake ,kwa kuzunguka kila kona ya jiji lile
Katika jiji la sumbawanga pembezoni kabisa mwa mji ,kuna sehemu iitwayo BURUDISHO wengi walipendelea kuiita sugar mumy Pub ,sehemu hii kulikua na uhuni wa kila aina ,vijana wengi sana katika jiji lile baada ya kazi zao walipendelea sana kujipumzisha maeneo hayo
Katika sehemu hiyo wakina dada wakila rangi walipatikana hapo uhuni na ufuska wote ulipatikana sehemu hiyo ,wakina dada walikuwa wakijiuza mchana peupe ,waswahili wanasema
``ukistaajabu ya musa utaona ya firauni’’ kweli hali iliyokuwepo BURUDISHO ilikua inatisha mwanaume yoyote aliyekuwa akipita hapo alikua akikimbiliwa na wanawake ,watu walivutwa mashati wakinang’aniwa na makahaba waliokuwa wakijiuza sehemu hiyo
Isaya akiwa anaendesha gari kuelekea BURUDISHO sharifu alianza kumdokezea isaya
``oiiii mzee huku hatari baba kuna mademu ving’ang’anizi tutanyang’anywa pesa zote sijui kama bosi atatuelewa sasa’’
``oiii umesema kuna mademu wooow safi baba kumbe kuna viliwazo huku sasa kama vipi wewe rudisha gari na hizi hela kwa boss mimi nitabaki hapa mkuu geto kwanza michosho sitaki kwenda ‘’
``bro turudi bwana ndugu hawa ni hatari wakisha kuteka kila siku lazima urudi humu’’
``niache mkuu niachie shilingi elfu kumi tu hapo nichukue kimwana’’
Gari lilifunga breki isaya alishuka ,sharifu alirudisha gari kwa bosi ,isaya alipokanyaga tu chini alipokelewa na wanadada zaidi ya watano
``twende kaka ,njoo huku bwana mimi msafi achana na huyu haogi’’
Isaya alivutwa na makahaba wale ,ilikua ni juu ya isaya sasa kuchagua ni kahaba yupi atamfaa kwa usiku ule
Isaya alimteua binti mmoja mweupe sana kisha aliongozana nae mpaka gesti
Walipofika ndani alimuuliza ``hey baby shi ngapi kulala na wewe’’
``buku tatu tu kaka na ya chumba kukodi elfu tano ‘’
``upo serious elfu tatu tu ‘’
``ndio kama utaongeza ya soda nitashukuru’’
Isaya alijisemea kimoyomoyo ``kweli maisha magumu ananipa mwili wake kwa elfu tatu’’
Isaya alijimwaga kitandani na kimwana Yule
Ilipofika saa saba usiku baada ya kumaliza mchezo alishangaa kumuona binti Yule anawaka waka machoni ,macho yake yalikuwa yaking’aa kama dhahabu ,isaya aliogopa sana alipomwangalia usoni alijihisi kuhishiwa na nguvu ,binti Yule alicheka kwa nguvu ``hahahahahahahahahahah’’’
…………………………………………………………………JE NINI KITAENDELEA ……………………………………………………..