Notification texts go here Contact Us Buy Now!

JIJI LA KICHAWI SEHEMU YA 02

JIJI LA KICHAWI 2

SIMULIZI ZA JOSHUA



JIJI LA KICHAWI

0713111547 WHATSAPP

Mbele ya barabara aliona mtu aliyevalia nguo nyeupe mwenye macho yakung’aa sana,isaya alianza kupiga kelele kila mmoja ndani ya gari alishangaa wakina mama walianza

``wewe dereva mwendawazimu nini una nini kondakta nae alishangaa dereva kashikwa na nini’’

Isaya aliendelea kumwona mtu Yule akiwa mbele yake kwa haraka alitaka kushika breki ili gari lisimame ,ilikuwa ni ngumu kushika breki kwa haraka kwani gari lilikuwa na spidi ya ajabu ‘’

JE NINI KITAENDELEA

``Aiseee dereva wewe kuwa makini humu ndani umebeba abiria na siyo magogo sawa dereva ‘’

Watu waliendelea kurusha lawama zao kwa isaya

Isaya aliendelea kukanyagia breki ila alifanya hivyo bila mafanikio

Kondakta sharifu alivyoona hali ya hatari inatokea alisogea mbele ya gari na kumsukuma isaya kisha alishika usukani ule

Isaya gafla alishaangaa kuona barabara nyeupe ,alipojaribu kuwaeleza abiria alichokuwa amekiona kila mtu alibaki akimshangaa sana na kumwambia kuwa bila shaka anaumwa au anaota maana siyo kawaida kabisa kwa vitu alivyokuwa anavisema daladala ilipofika litulingwa ilifunga breki na wote waliteremka

Ndani ya gari alibaki bibi mmoja kizee aliyekuwa amevalia nguo za rangi nyekundu

Isaya alimtazama sana bibi Yule kisha alimsogelea na kumwambia

``wewe bibi unaelekea wapi maana gari gari limeshafika mwisho wa kituo’’

Bibi Yule alimkazia macho isaya kisha akatoka nje na alipofika nje akamsumya kwa nguvu

``nywiiiiiiii dawa yako ipo jikoni’’

Isaya alibidi amshtue sharif na kumuuliza ``hey sharrif huyu bibi vipi ana wanga nini’’

Maskini isaya alikua amekosea sana kitendo cha kumwambia bibi wa watu anawanga

Bibi Yule alimsikia isaya waziwazi kisha akamwambia

``nilikua nakutafutia kosa sasa umejileta mwenyewe’’

Sharifu akiwa ndani ya gari alikua akishuhudia kila kitu aliachia kicheko cha nguvu huku akisema

``hahahahahah mzee baba umezingua mwombe bibi wa watu msamaha mabibi wa hapa town hawachezewagi atiiii sasa wewe leta ujuaji uone’’

Isaya kwa hasira alijibu

``mwanangu sharifu maisha ndio haya haya ,huyu kikongwe aanzaje kunitisha mimi mtoto wa town aseeeeee aache ujinga atembee na mia ‘’

Isaya alimfuata bibi Yule na kumtimu

``nakwambia ondoka mwanga wewe ,’’

Isaya alipomfikia bibi Yule alimshika shati na kuchomoa uzi mmoja wa shati la isaya bila isaya kujua

Bibi Yule hakuwa na la kufanya zaidi ya kuondoka

Hii hutokeaga sana katika taifa letu Tanzania siyo kila ajali inasababishwa na uzembe wa madereva la hasha!!!!  Ajali nyingi usababishwa na wachawi  ,Siku hiyo ingepaswa ajali mbaya sana kutokea kikongwe Yule aliyekuwa akitukanana na isaya alikuwa ameteuliwa na wachawi atoe kafara abiria ndani ya gari lile hivyo wakati ule isaya alipoona mtu mbele yake ilikua ni mzimu ambaye alikua anataka kumyumbisha isaya ili ajali iweze kutokea ,kutokana na kikongwe yule kushindwa kufungua tunguri la kichawi ndani ya gari lile  kwa hofu ya abiria wale ,alipelekea zoezi lile la kafara kushindwa kufanyika


Ilipofika saa kumi na mbili na nusu isaya alirudisha gari kwa bosi ili aweze  kuelekea katika geto lake alilopanga kwa mapumziko

Isaya  alielekea moja kwa moja hadi getoni baada ya kukabidhi funguo za gari kwa boss ,alipofika ndani ya chumba chake ni kama hakuelewa alichokiona

Kitanda chake kilikua kama kimegeuzwa chini kukaangalia juu ,isaya alikitazama kitanda kile kwa takribani dakika moja bila kupata majibu ila alijipa na kusema

``ohoooooo nimekumbuka asubuhi nilifanya usafi hapa wenda niligeuza bila ya kujua ‘’

Kutokana na uchovu na mahangaiko mengi isaya alijilaza kitandani mwake

Akiwa amejilaza haikupita nusu saa ,alisikia kitanda kikitetemeka ,kitanda kilitetemeka sana mithili ya tetemeko la dunia  ,isaya alitaka kuamka aangalie kuna nini alipoinua mgongo alishikiliwa kwa nguvu sana kama chuma inasavyo sumaku alitaka kupiga kelele mdomo nao ulinata kama umewekewa superglue(gundi)



Je NINI KITAENDELEA

 

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.