Notification texts go here Contact Us Buy Now!

JIJI LA KICHAWI SEHEMU YA 01

JIJI LA KICHAWI 1

SIMULIZI ZA JOSHUA / 8 months ago


KIJIJI LA KICHAWI

NA JOSHUA SHAO

Isaya akiwa amejiinamia chini aliwaza na kuwazua ni jinsi gani atauepuka umaskini ,alivyokuwa akifikiria hakupata jibu kabisa ,ghafla akiwa anawaza mambo mbali mbali aliona kivuli cha mtu kikipita mbele yake ,isaya alishangaa sana ,hofu ilimjia na uwanaume wake wote alijikuta akitetemeka sana

Isaya alibaki akijiuliza maswali akilini mwake ``hivi naota au ni kweli si nimeona kivuli kinatembea ,inakuaje kivuli kinatembea alafu mtu mwenyewe haonekani ama kweli ili jiji la sumbawanga lazima nihame tu hakuna jinsi kabisa ,kwanza usalama wa maisha yangu uko wapi mimi maisha magumu ‘’

Isaya akiwa anaendelea kuwaza juu ya kivuli kile, bibi mmoja alipita pale akiwa amebeba kikapu kichwani na mkononi akiwa amebeba dumu la maji ,isaya alikua amejiinamia chini tu muda wote

Bibi Yule alipomkaribia isaya ,isaya aliinua kichwa chake na kumsalimu

``shikamoo bibi’’

``marahaba kijana wangu habari yako’’

``nzuri bibi’’

Isaya alimtazama bibi Yule kwa huruma sana, hii ni kutokana na mwonekano wa bibi ,miguu ya bibi Yule ilikua imejazana magamba ,ngozi yake ilikua ngumu sana mwili wake pia ulikua umedhohofu,isaya alimwonea huruma na kubakia akimtazama tu ,alipofika mbele kidogo bibi Yule alitoweka

Isaya alishindwa kujizuia alipiga kelele kwa nguvu

```uwiiiiiiiiiiiiii nakufa nakufa ‘’ isaya alikimbia kutoka pale alipokuwa,alipokuwa akikimbia umati wa watu ulijitokeza kila mmoja akimuuliza isaya shida yake ni nini.kutokana na hofu isaya aliyokuwa nayo alishindwa kabisa kueleza ni nini kimempata ,watu waliokusanyika kumsikiliza walishikwa na hasira wengi wao walikuwa wakitukana

``huyu mwehu nini anapiga kelele mchana peupe tunamuuliza vipi nini shida hajibu’’

Baadhi ya watu waliondoka ila wakina mama wachache waliongozana na isaya huku wakimuuliza shida ni nini ‘’

Isaya aliwaeleza wakina mama wale yaliyomsibu

Kila mmoja alistaajabu na kumweleza isaya kuwa asishangae hayo ndio mambo yaliyopo jijini pale

Mama mmoja alimshka isaya begani na kumwambia ``mwanangu umekuja hapa toka lini’’

``mama nina wiki mbili sasa ‘’

``pole mwanangu usijali ndio mambo ya jiji letu sie tushazoea kwetu kupishana na majini njiani ni jambo la kawaida ,tena na kwambia mshukuru Mungu hujaelekea LITULINGWA kule hakufai mweeeh ila usijali baba ‘’

``sawa mama nashukuru’’

Wakina mama wale walimwaga isaya na kumwacha akiwa mwenyewe

Isaya ni kijana kutoka mkoani Manyara ,kutokana na ujuzi wake mzuri wa kuendesha magari alichukuliwa na tajiri mmoja wa sumbawanga ili aweze kumsaidia katika kazi zake hususani kuendesha daladala zake zinazofanya ruti ndogo ndogo za pale mjini

Ilikua ni siku chache tu toka isaya awasili pale mjini lakini alikua amekwisha ona mambo mengi ya kumchosha na kumwogopesha


Siku zilienda na isaya aliweza kuyasahau mambo yote yaliyokuwa yametokea ,taratibu alilizoea jiji ,isaya alikabidhiwa daladala na mapema kabisa alianza kazi ya udereva

Siku moja akiwa na gari akiwa anafanya safari ya kupeleka abiria kutoka ludwashi hadi masange ghafla alishtushwa na kitu kilichopo mbele yake

Mbele ya barabara aliona mtu aliyevalia nguo nyeupe mwenye macho yakung’aa sana,isaya alianza kupiga kelele kila mmoja  ndani ya gari alishangaa wakina mama walianza

``wewe dereva mwendawazimu nini una nini kondakta nae alishangaa dereva kashikwa na nini’’

Isaya aliendelea kumwona mtu Yule akiwa mbele yake kwa haraka alitaka kushika breki ili gari lisimame ,ilikuwa ni ngumu kushika breki kwa haraka kwani gari lilikuwa na spidi ya ajabu ‘’

JE NINI KITAENDELEA

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.