Notification texts go here Contact Us Buy Now!

Elimu ya upishi wa keki

KEKI: (JIELIMISHE UNUFAIKE)

Elimu ya upishi wa keki


MASWALA YA UPISHI WA KEKI: Tunaangalia matatizo yanayotukumba katika upishi wowote ule wa keki (hata mkate wa mayai ni keki!) kwa hivyo litambue kosa lako ujirekebishe. Kwa urahisi wa kulitafuta kosa lako (!) Tumeweka matatizo kwa mafungu, kisha kila fungu lina matatizo kadhaa, na kila tatizo lina sababu kadhaa.
Tunaanza....

MATATIZO YA KEKI KUUMUKA:

SUALA LA 1. KEKI HAIKUUMUKA AU IMEUMUKA KIDOGO TU
Sababu zake:
1>>Ulichotumia kuumua keki yako (kwa mfano baking powder):
labda ulisahau kuongeza baking powder? Au hukutia ya kutosha? au umetia ya kutosha lakini baking powder yenyewe imesha expire? au Haija expire lakini hukuihifadhi uzuri kwa hivyo imekwisha nguvu zake (Ukisha ifungua baking powder, ihifadhi kwenye chombo chenye mfuniko wa kubana ili isipigwe na hewa na kuharibika haraka au kama unainunua kwa vipaketi vidogo, basi usivifungue vipaketi hivyo hadi unapokuwa tayari kuvitukia kwenye upishi).
2>>Mchanganyiko wa keki nao ukiuchanganya sana au usipouchanganya sana pia inasababisha keki yako iisiumuke uzuri kwa hivyo changanya vya kutosha ili mahitaji yote yachanganyike uzuri lakini usizidishe. Mahitaji yakisha kuchanganyika tu usiendelee kuchanganya utaharibu upishi.

3>>Moto ulotumia ulikuwa mdogo kwa hivyo keki haikupata joto kuifanya iumuke itakikanavyo. Hakikisha oven lako limepashwa moto ulohusiwa kabla kuweka mchanganyiko wa keki. Pia jizuie kufungua mlango wa oven ovyo baada ya kuweka keki ndani kwani unapitisha hewa ya baridi na kupunguza moto ndani kwa ove, Jaribu kulipasha oven lako moto kubwa sana kwa hivyo tumia moto ulohusiwa utumie.

4>>Mahitaji ya majimaji nayo yakizidi au yakipungua keki haiumuki uzuri. Kwa hivyo usizidishe wala kupunguza maji kulingana na ulivyphusiwa kwenye recipe. Kumbuka upishi wa keki hautaki kukisiwa. Kwa hivyo kama ulitumia maji mengi punguza, na kama ulitumia kidogo, ongeza ukirudia mapishi tena.

5>>Tumia mahitaji yanayokusudiwa kwa upishi wa keki ndio upate keki inayoumuka vizuri. Kwa mfano unga na siagi/margarine tumia ulioandikwa 'SUITABLE FOR BAKING' Ukitumia mahitaji yasokusudiwa kwa upishi wa keki keki inaharibika. kirahisi.
Kama keki inatumia mayai, jaribu kutumia mayai fresh ambayo hayawekwa kwa mda mrefu. Pia hakikisha mayai siyo baridi. Kama una mazoea kuweka mayai kwenye friji (jokovu) hakikisha umeyatoa yakae kwa mda nje ya friji ili yatoke ubaridi kabla kutumia kenye upishi wa keki.

6>>Labda umetumia chombo kikubwa sana kulingana na recipe ilivyohusia. Recipe ikikuhusia utumie chombo cha ukubwa fulani jaribu utumia ukubwa huo huo au kama itazidiwa au kupungua ukubwa basi iwe ni kwa idadi kidogo sana au sivyo keki inakuwa matatizo kupata kimo ikiokwa.

7>>Pia baada ya kuchanganya mchanganyko wako, usiuweke sana kabla kuoka. Kwa hivyo hakikisha kuwa moto wako upo tayari huku unachanganya mahitaji ili ukimaliza tu unautumbiksa kwenye chombo na kuoka mara moja. Usiuache ukae kwa mda mrefu kabla kuokwa.

SUALA LA 2: KEKI IMEUMUKA UPANDE MMOJA:
Matatizo na jinsi ya kuyarekebisha

1>>Hukuchanganya mahitaji yako kwa uzuri. Hasa katika kuchanganya baking powder na unga. Hakikisha mahitaji hayo yamechanganyika kwa uzuri ili ukiweka mahitaji ya maji maji, sehemu yote ya mchanganyiko unakuwa umepata baking powder na inaweka kuumuka.

2>>Labda hukusawazisha mchanganyiko kwenye chombo cha kuoka. Baada ya kutia mchanganyiko kwenye tray ya kuoka, jaribu kusawazisha sehemu ya juu kwa mwiko wa keki (spatula) au tumia kisu butu. Usipige pige treya kwenye meza utaharibu keki! Pia hakikisha waya ndani ya oven zipo sawa sio upande mmoja uko chini na mweninge juu.

3>>Matatizo ya oven : labda oven lako lina matatizo kwa hivyo halileti moto sehemu zote ndani mwa oven, kwa hivyo sehemu nyengine bado zina hewa ya baridi na kwengine moto zaidi. Kwa hivyo angalia kama oven lako linafanya kazi uzuri.

SUALA LA 3: KEKI IMEUMUKA SANA HADI IMEFANYA KILIMA SEHEMU YA KATIKATI AU/NA HATA KUPASUKA
1>>Inasababishwa na moto mwingi au moto wa juu na chini haupo sawa.
2>>Pia mchanganyiko umepigwa sana. Kwa hivyo usizidishe kupiga aidha mayai au mchanganyiko wa sukari na siagi. Recipe ikikuhusia changanya kwa mda wa dakika kumi usiwe bado upo tu unachanganya baada ya nusu saa!

SUALA LA 4: KEKI IMEFANYA KISHIMO KATIKATI (SEHEMU YA JUU):

1>>Inaweza kusababishwa na moto kuwa mdogo. Hakikisha umelipasha na oven limeshika oven moto uzuri kabla kuiweka mchanganyiko wa keki, Pia usiwe wa kufungua fungua mlango wa oven mara kwa mara kwani unapitisha hewa ya baridi ndani na kuupunguza moto.
2>>Pia inawezekana umetoa keki kwenye oven kabla haijaiva kabisa. Hakikisha unapitisha kijiti KATIKATI mwa keki ili kuangalia kama imewiza (kijiti kinatakiwa kitoke kisafi bila mgando wowote, ukiona kijiti kimetoka na mchanganyiko wowote au kinangata, basi keki haijaiva vizuri).
3>>Pia kuigonga au kuisukuma chombo cha keki huku na kule wakati inaokwa. Ukisha iweka keki kwenye oven usiiguse mpaka iwive. Siyo umeweka keki kwenye oven ndio sasa umekumbuka kuna karai la mafuta hukulitoa uanze kuisukuma keki hapa na pale!
4>>Pia hakikisha umetumia mahitaji yalokusudiwa upishi wa keki, hasa unga na siagi/margarine ya keki.
5>>Pia inasababishwa na wingi wa sukari au siagi/margarine, kwa hivyo punguza kiwango ukijaribu tena.
6>>Ukichanganya sana mahitaji pia inasababisha keki kutoumuka vizuri. Hakikisha umecnhangaya uzuri kisha uache uendlee kupika. Ukichanganya sana utaharibu mapishi.

SUALA LA 5: KEKI IMEFANYA KISHIMO KATIKATI (SEHEMU YA CHINI)

1>>Mchanganyiko ulikuwa mkavu kwa hivyo mahitaji ya maji maji yalipungua, jaribu kuweka ulichohusiwa kwenye recipe.
2>>Moto sehemu ya chini ulikuwa mwingi sana.
3>>Chombo chako cha kuoka kilikuwa maji maji -hakikisha umekikausha kabisa kabla kutia mchangayiko wa keki yako.
3>>Ulitia mayai mengi zaidi katika mahitaji.
SUALA LA 6: KEKI KUUMUKA/KUJAA LAKINI BAADAE IKANYWEA
1>>Moto ulotumia ulikuwa mkubwa sana au mdogo. Tumia wingi wa moto uloambiwa kwenye hiyo recipe unayotumia.
Pia hakikisha moto unaotumia upo sawa kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa upishi, sio mara kwa mara, moto unapunguzikaa mara unazidi.
2>> Mchanganyiko wako uliupiga/kuuchanganya sana katika matayarisho.
3>> Ulitumia mafuta mengi katika upakaji wa mafuta kwenye treya ulotumia. kwa hivyo sehemu za pambizoni zimezidi mafuta. Jaribu kupaka treya zako za kuoak mafuta kiasi tu.
4>>Tumia unga,siagi au margarine zilokusudiwa mapishi ya keki.
5>> Treya ya kuoka hiyo keki ilikuwa kubwa kulingana na wingi wa mchanganyiko unaotumia. Jaribu kutumia vipimo vya treya kama ulivyohusiwa kwenye recipe.
6>> Umetumia baking powder nyingi zaidi ya ulivyohusiwa kwa vipimo vya recipe unayotumia. Jaribu kutumia vipimo ulivyohusiwa kwa recipe. Usizidishe wala kupunja kitu!
7>> Mahitaji ya majimaji yalikuwa mengi kwenye mchangayiko kwa hivyo ukipika tena, upunguze.
8>> Ulitumia sukari na siagi kidogo kwenye mchanganyiko au uliongeza mahitaji mengine yote lakini ukapunja sukari na siagi/margarine.

MATATIZO YA UPISHI WA KEKI

SUALA LA 7: KEKI HAIKUKOLEA/KUPIGA RANGI SAWASAWA SEHEMU ZA JUU

1>>Keki hukuiweka katikati kwa oven au vile viwaya ndani ya oven vinavyowekewa tray za kuoka havipo sawa (sehemu moja ipo juu kuliko nyeninge).

SUALA LA 8: KEKI IMEUNGUA:

1>>Kama keki imeungua sehemu ya juu, moto ulikuwa mwingi sehemu ya juu.
na kama iliungua chini , moto ulikuwa mwingi sehemu ya chini
Ukipika tena uwe mwangalifu moto uwe wa kiasi juu na chini.

MATATIZO YA KEKI (SEHEMU ZA NJE):

SUALA LA 9: SEHEMU ZA KEKI ZA NJE ZIPO MAJI MAJI NA ZINANGATA.
1>>Umetumia sukari na siagi/margarine nyingi (punguza ukipika tena).
2>>Jaribu kutumia unga ulokusidiwa upishi wa keki.
3>>Keki iliachwa kupoa kwenye trey ilopikiwa. Baada ya kuioka keki, iache ipoe kidogo tu kwenye treya ulopikia, kisha itoe uweke kwenye waya (cooling rack) ili ipoe bila kutenda mvuke.

SUALA LA 10: SEHEMU YA NJE YA KEKI IMETENDA GAMBA AMBALO LIMEKUWA GUMU
1>>Umeoka keki kwa moto mkubwa sana (kwa hivyo sehemu za nje zimekauka) au umetumia moto mdogo (kwa hivyo keki imechukua mda mrefu kuwiva ndani) Jaribu kutumia moto wa oven uliohusiwa kwenye recipe.
2>>Aidha umetumia sukari nyingi au kidogo kwenye upishi. Tumia kiwango ulichohusiwa.
3>>Au umezidisha kiwango cha mayai kwenye upishi (punguza ukipika tena)
4>>Pia inasababishwa na kuchanganya mahitaji sana katika utayarishi.

SUALA LA 11: SEHEMU YA JUU YA KEKI IMEPASUKA PASUKA.

1>>Moto sehemu ya juu (au chini mwa keki) ulikuwa mwingi kwa hivyo punguza utakapoipika tena.
2>>Mchanganyko wako ulikuwa mzito kwa hivyo utabidi uufanye majimaji kidogo ukipika tena.
3>>Au mcnahangyiko uliunganya saana! Mchanganyiko wa keki haufai kucnayanya sana., Ukichanganyika tu uzir anza kuupika!.
Hukutia mahitaji kwa vipimo sawa, jaribu kutia mahitaji yote (sukari,siagi au baking powder) kiwango ulichohusiwa kwenye upishi.
4>>Umetumia unga ambao sio wa upishi wa keki!.

MATATIZO YA KEKI (SEHEMU YA NDANI)

SUALA LA 12:SEHEMU YA NDANI YA KEKI IPO MAJIMAJI (KAMA MFANO WA SIMA)
1>>Umetumia kiwango kikubwa cha sukari,mayai na/au baking powder.
2>>Umetumia unga ambao sio wa kupikia keki kwa hivyo jaribu kutumia unga ulokusudiwa kwa mapishi ya kuokwa.
3>>Hukuchanganya mchanganyiko uzuri.

SUALA LA 13:KEKI IMEKUWA LAINI SANA MPAKA INAVUNJIKA VUNJIKA MAPANDE MAPANDE
1>>Umetumia mafuta au siagi nyingi katika upishi.
2>>Mchanganyiko haukupipwa kwa mda unaofaa umeupiga kidogo tu
3>>Mayai hayakutiwa wingi unaofaa
4>>Umetumia sukari au baking powder nyingi sana, punguza ukiipika tena
5>>Umetumia unga ambao sio wa kupika keki.

SUALA LA 14. KEKI IMEJAA MAFUTA:
1>>Ulizidisha kiwango cha siagi katika mahitaji.
2>>Hakikisha umeipiga/umechanyana siagi na mahitajimengine uzuri.
3>>Kama unatumia siagi, usiiyeyushe, inafaa iwe baridi unapoichanganya kwenye mahitaji.
4>>Fuata maelezo ya recipe vizuri! Kama imekuhusia ucnayanye siagi na sukari mwanzo kabla mahitaji mengine usichanganye mahitaji mengine yoyote hadi hayo ulohusiwa uchanganye yamekuwa sawa!

SUALAL LA 15: KEKI INA MATUNDU/MASHIMO MAKUBWA NA MINGI NGANI YA NYAMA ZAKE

1>>Mchanganyiko haukuchanganya vizuri kwa hivyo mahitaji hayakuchnaganyika uzuri
2>>Ulitumia mayai zaidi kuliko ulivyohusiwa au umetumia mayai ambayo yalikuwa baridi (unafaa mayai uyaache yatoke ubaridi kama unayahifanyi ndani ya friji)

SUALA LA 16: KEKI IMEKUWA KAVU NA KUVUNJIKA VUNJIKA
1>>Umeoka keki kwa moto mkubwa sana (kwa hivyo sehemu za nje zimekauka) au umetumia moto mdogo (kwa hivyo keki imechukua mda mrefu kuwiva ndani) Jaribu kutumia moto wa oven uliohusiwa kwenye recipe.
2>>Hukutia mayai au umetumia mayai kidogo kwa hivyo ukipika tena usisahau kutia mayai.
3>>Tumia unga ulokusudiwa kupikia keki (flour suitable for baking)
4>>Mchanganyiko wako ulikuwa mkavu kwasababu hukutumia kiwango cha sawa cha mahitaji ya majimaji
5>>Jaribu kutumia sukari ya kusagwa.

MATATIZO YA KEKI WAKATI WA KUITOA KWENYE TREYA BAADA YA KUOKWA:

SUALA LA 17: KEKI IMEGANDA KWENYE TREYA YA KUOKA AU IMEKATAA KUTOKA KWENYE TREYA BAADA YA KUPIKWA.
1>>Aidha treya ya kuokwa haikupakwa mafuta au mafuta yalopakwa hayakuwa ya kutosha. Upakaji wa mafuta kwenye treya za kuoka zinasaidia keki isigande ikishaiva.
2>>Keki haikupewa mda kupoa kidogo kabla kutolewa kwenye treya au uliiacha ipoe kabisa kabla kuitoa. Ukisha itoa keki kwenye oven, iache ipoe kidogo tu kisha jaribu kuimimina taratibu. Kama imeiva uzuri na treya ilipakwa mafuta, ni rahisi kutoka.
3>>Kabla hujaitoa keki kutoka kwa treya, hakikisha umepitisha kisu kikali baina treya na pambizoni mwa keki kuhakikisha haijaganda na pia kujaribu kubandua sehemu zozote ambazo zinawezekana bado zimeganda kwa treya.

KAMA KUNA TATIZO LOLOTE LILE UMELIKUMBA AMBALO HATUJALIWEKA HAPA, TUJULISHE TUPATE KULIONGEZA. SHUKRAN!!!

ZINGATIA:
1.Upishi wa keki hautaki kukisiwa.Tumia viwango vya mahitaji sawa na recipe unayotumia.
2. Mahitaji unayotumia yawe yalokusudiwa kwa upishi wa keki kwa mfano unga unaokusudiwa kwa upishi wa keki (suitable for baking) siagi au margarine imekusudiwa kwa upishi wa keki. Kila mahitaji yana viungo tofauti ndani yake kwa hivyo ukitumia mahitaji ya swa, keki inakuwa haikupifi chenga sana.
3.Mahitaji kama siagi (isiwe imeyayuka), mayai (yasiwe baridi), mchanganyiko wako usiwe na joto sana , au sivyo keki itakuletea matatizo!

UKIZINGATIA HAYA YOTE, UPISHI WA KEKI UTAKUWA RAHISI NA UTAPIKA KEKI INAYOKURIDHISHA KILA SIKU

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.