Notification texts go here Contact Us Buy Now!
Machapisho

MUME YUKO MBALI NA MAPENZI YAMEPUNGUA NINI UTAFANYA?

hv jaman kama mpenz au  mume wako mlikuwa mkipendana sana halaf hafla akapunguza mapenz kwa kuwa mpo mbali nini ufanye ili kurudisha upendo wake kwako?

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Maoni 1

  1. WASIA KWA MWANAMKE AMBAE MUME WAKE YUKO SAFARI... ✅
    ****************************
    Ewe mwanamke ambae mumeo yuko safari ujue kua safari imekuwa kwa ridhaa yenu wote wawili na mumekubaliana ndio ukamsindikiza hadi stage ya bus ama airport..
    *✅ Na ni wajibu wako kumpa nasaha ya kisheria, huko aendako amche Allah. Wanawake wa kiswahaba walikua akitoka mume wamwambia mume " mche Allah wala usilete riziki ila ya halali, hakika tunaweza kusubiri njaa na dhiki za dunia lakini hatuwezi kuhimili Jahannam siku ya kiama". Je leo wako wanaowausia waume zao hivyo?
    *✅Mpe nasaha mume huko aendako afanye mema na ajiepushe na kumuasi Allah katika muamala wake wa kazi na watu kwa jumla.
    *✅Mpe nasaha kwa Ibada mbali mbali za sunnah na faradhi (kuswali kwa wakati,kutoa zaka ama sadaka ,kufunga Sunnah , kuwatendea wema watu na mambo ya kheri...)
    *✅Ewe mwanamke wa kiislam, anaposafiri mume wako , pesa anazotuma, mali na vitu alizobakisha nyumbani , na watoto zote hizo ni amana juu ya mabega yako na utaulizwa siku ya Qiyama. Kullukum ra'in wa kullu rain mas-ulun 'an ra'iatih (mume ni mchunga na ataulizwa juu ya familia yake,na mke ni mchunga na ataulizwa juu ya mali ya mume wake...) Huna ruhusa ya kutoa kitu ila kwa idhni ya mume, epuka Israf na kutumia pesa zake kwa mambo hayana muhimu na hayako kwa bajeti aliokupangia ila kwa idhni yake, Na huna ruhusa kuingiza mtu nyumbani ila kwa ruhusa ama makubaliano na mume.
    *✅ Isitiri heshima na ndoa yako na mumeo. Huna ruhusa kutoka ila kwa idhni ya mume japo kwenda kuamkua wazazi ama jamaa wa nyumbani.. Mwanamke anaetoka bila ruhusa ya mume njia zote anazopita yuko kwenye laana.
    *✅Epuka mambo ya kumtia dhana mbaya mume (kuchelewa kurudi usiku ukitoka , kuwasiliana na wanaume wasio kuwa mahram, kutangamana na wanawake wasiokuwa na maadili mema...)
    *✅ Uwe na Subra na maisha ya kuwa mbali nae, hujui matatizo anazozipitia huko japo pengine labda hushindwa kukuelezea kila kitu kwa kuhofia kukutia wasi wasi.
    *✅ Daima mpe nasaha ya kuwa na subra huko aliko na kumuombea Dua kila wakati unaposwali.
    *✅Ukiwasiliana kwa simu usimtie maneno ya kumkera ama kumvunja moyo. Daima tumia lugha nzuri ukizungumza nae ili apate kuliwazika baada ya dhiki na uchovu wa kazini..
    *✅ Mpe nasaha ya kujipangia maisha yenu baadae ili asiwe wa kusafiri daima..
    * ✅ Ishi kwa wema na wazazi wake , ndugu na jamaa zake kwa Subra na kuwastahimilia ukitarajia malipo kwa Allah.. kumbuka hakuna mkamilifu ila hizo ni familia mbili tofauti lazima utapata tofauti ya kuishi na watu wengine, muhimu kuwa na subra..
    * ✅ Pia epuka vikao vya umbea na masengenyano na wanawake wengine.. kwani utasikia mengi na mengine hutayafurahia. Bora utumie muda wa ziada kwa kujikurubisha kwa Allah kwa Dua na kusikiza mawaidha na Ibada zengine....

    * ✅ HII NASAHA KWA KILA ANAEMPENDA MUME WAKE NA ANAEIJALI NDOA YAKE ..

    WA BILLAH TAWFIQ KWA MWENYE KUJITAHIDI...

    MKONO KWA MKONO HADI PEPONI..
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.