Waambieni, Waambieni tafadhali.
Wasiwe wema eti kwasababu dunia tunapita kwa muda mfupi, hata wakiwa wabaya hii dunia bado tunapita tu.
Nendeni mkawe sauti yetu kwa kuwaambia wawe wema kwasababu wema unaboresha uwepo wetu hapa duniani.
Hamna haja ya kunionea huruma, ikiwa jua litachomoza kesho basi amini bado tumaini ninalo, tutaamka kama ninyi labda kama pua hizi tunazomiliki hazitapitisha tena ile hewa ya oksijeni.
Si rahisi kwa binadamu kubeba kosa asilolitenda waambie wasimpoteze anayejishusha kwao maana ni gharama.
Najua hawajui msalaba waliotutwisha mabegani mwetu, ni mzigo mzito, unatupa shida kutembea kwenye ulimwengu huu wa wana riadha.
Si siri wanatuchukia, ila watambue hatukupanga kuwa yatima,hatukupanga kuzaliwa kwenye kizazi chao. Kama wanaijua kesho yao waendelee na ubabe wao.
