Notification texts go here Contact Us Buy Now!

HADITHI-BINTI MFALME LEGITA SEHEMU YA 02

HADITHI- BINTI MFALME (Legita)
SEHEMU - 2

MTUNZI- LISSA WA MARIAM
"Hapana sipo tayari kuona unapatwa tatizo, bado nakupenda Chansa, ninachoomba usikatili penzi langu, mapenzi yangu yote yapo kwako na sio kwa mfalme, siwezi kukubali nikukose, nitajitahidi kuishi na wewe kwa siri" Gwanta aliongea kwa hisia 

"Sawa, lakini pia hata kama unakuja kwangu, tunatakiwa tuwe tunaonana usiku tena kwa tahadhali sana ili watu wasije wakatuona, alafu umekuja na kijakazi wako huoni kama ni hatari kwetu?"

"Ondoa hofu, hawezi kusema kitu yule ni msiri wangu"

"Sawa mfalme anarudi lini?"

"Nafikiri zimebaki siku mbili atakuwa amerudi katika himaya ya Kwembeo, ila kuna jambo zuri sana, nataka nikutafutie kazi pindi mfalme atakaporudi, lengo langu uwe karibu nami, niweze kukuona kila wakati"

"Sawa nitafurahi sana"

"Leo usiku nitakuwa mgeni wako nakuja kulala na wewe" alisema Gwanta kisha akamkumbatia Chansa na kuanza kumbusu huku akimpapasa

"Inatosha tunaweza kufumwa hapa embu nenda kwenye ngome yako" Chansa alimwambia

"Sawa" malkia Gwanta aliondoka huku kijakazi wake Zamo akimfuata nyuma

Hayo ndo yalikuwa maisha ya malkia Gwanta aliweza kumsaliti mumewe ambae ni mfalme Seuta, mfalme mwenye nguvu ambae aliheshimika na kuogopwa katika vijiji vyote vya jirani, Gwanta alikubali kuolewa na mfalme huyo kwa tamaa ya kuwa malkia tu, ila moyo wake bado ulikuwa kwa Chansa mwanaume ambae sasa amehamisha mapenzi yake kwa Legita binti wa mfalme,

Legita hakufahamu kama Chansa aliwahi kuwa na mahusiano na mwanamke ambae baba yake amemuoa, hayo yote yanafanywa kuwa siri kubwa, kati ya Chansa na Gwanta

*******
Baada ya siku mbili kupita, Mfalme Seuta anarudi kutoka safari akiwa na wazee wake wa baraza ambao ni wasahauri wake, safari yake ilikuwa katika kuhakikisha anaweza kumiliki himaya mbili, moja ya Kwembeo na nyingine ya Bweleo ambayo ipo jirani na kijiji chake, juhudi zake ziligonga mwamba kwani, wanakijiji wa Bweleo walikuwa hawataki kutawaliwa na mfalme Seuta, tayari walishamchagua kijana mdogo na kupendekeza awe mtawala wao

"Nitahakikisha naitawala Bweleo, lazima himaya zote ziwe zangu, mimi ni mfalme mwenye nguvu, nitakuwa mpumbavu kama nishindwa kutimiza hili" alisema mfalme Seuta kwa hasira,

"Hivi baba, kwani kuna umuhimu gani wewe kutawala himaya zote hizo? huoni kama unaweza kusababisha maafa kwa wanakijiji wako, maana wanakijiji wa Bweleo walishasema hawataki kutawaliwa, kufa kwa mtawala wao wa mwanzo haimaanishi wewe ndo uwatale kimabavu, wao wenyewe watachagua mtu wanayemtaka" alidakia Legita

"Nyamaza!! Huwezi kumpinga mfalme ni Sawa na kumdharau, mfalme mwenye nguvu kama mume wangu hawezi kushindwa kwenye jambo lolote alitakalo, mume wangu naamini utashinda tu, hakuna mtu mwenye uwezo wa kukuzidi wewe" malkia Gwanta alimuunga mkono mumewe

"Wewe ni malkia ambae unachangia katika kumpotosha baba yangu, nitahakikisha ndoto zako zote juu ya baba yangu nazifutilia mbali, unahisi baba akilazimisha hayo nini kitatokea? Watu watapata tabu wanaweza kufa" Legita alisema huku akimkazia macho mama yake wa kambo

"Legita naomba uende kupumzika" mfalme alisema

"Sawa lakini unapaswa unisikilize ushauri wangu" Legita alitoka na kuwaacha mfalme na malkia

"Mfalme wangu, sasa unafikiria kufanya nini?"

"Nitafanya chochote ikiwezekana tutapambana, huyo mtu wanayemtaka wana Bweleo lazima afe, itabidi vijana wangu wasikae bure wawe wanafanya mazoezi kwaajili ya pambano, maana muda wowote naweza kufanya jambo kubwa" 
ITAENDELEA

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.