Kuna mahusiano mengi yanakufa kwakua tu wadada wanapewa raha, hivyo wanajisahau na kuharibu. Mwanamke, mahusiano yamnapokua mazuri unapaswa kuacha kujisahau na kuanza kujipenda.mwanamke anapompenda mwanaume anataka kila wakati awe naye, akimuona online basi awer anachart naye.
Mteja anaweza kukupigia simu akilalamika kuwa mpenzi wangu namuona online lakini nikimtumia meseji hanijibu. Yaani anakua na kisirani akiwaza anafanya nini online hajibu SMS zangu, wanawake wanadhani hii ni dhaarau bila kujua sisi wanaume tuna mambo mengine.
Kwamba ili uwe na furaha ni lazima uwe na kitu kingine cha kufanya zaidi ya mpenzi wako. kwamba mwanamke, ukiingia online basi sio kutaka tu kuchart na mpenzi wako bali hata kusoma umbea, kuangalia youtube au kuchart kitu kingine, ili hata mpenzi wako asipokutumia mseji au kujibu SMS yako usipaniki!
Unapokua kwenye mahusiano jua kuwa mwanaume wako ana mambo mengine zaidi ya kuwasiliana na wewe, kukuwaza wewe au kukuridhisha wewe. Hivyo kama utamfanya mpenzi wako kuwa ndiyo kila kitu kwako, ndiyo bosei wako, shoga yako, Mama yakeo, jirani yako, mtu wako wa kisirani, mtu wako basi ni rahisi kuhisi hupendwi pale anapokua na mambo yake na kuleta kisirani mwisho kuharibu.
Jifunze kuwa na furaha yako mwenyewe, kufanya vitu vya kukupa raha na mpenzi wako akawa mtu wa ziada.