Notification texts go here Contact Us Buy Now!

JINSI YA KUPIKA MAKARONI YA MADUARA YA NYAMA YA KUSAGA(MEAT BALLS MACARONI)

*MAKARONI YA MADUARA YA NYAMA YA KUSAGA(MEAT BALLS MACARONI)*

MAKARONI YA MADUARA YA NYAMA YA KUSAGA(MEAT BALLS MACARONI

MAHITAJI YA KUPIKA MAKARONI YA MADUARA YA NYAMA YA KUSAGA(MEAT BALLS MACARONI).

1.Pakti ya Macaroni
2.Nyama ya kusaga robo
3.Kitunguu maji kidogo 1
4.Kitunguu thomu punje 3
5.Karoti kubwa kiasi 1
6.Pilipili boga 1
7.Nyanya(Tungule) kubwa 3
8.Mafuta robo kikombe
9.Chumvi kijiko cha chakula 1 na 1/2
10.Ndimu 1
11.Nyanya ya paketi robo
12.Royco pakti 1
13..Maji lita moja

 MAANDALIZI YA KUPIKA MAKARONI YA MADUARA YA NYAMA YA KUSAGA(MEAT BALLS MACARONI).

1.Osha Viungo vyote vinavyohitajika kuoshwa
2.Para keroti weka pembeni,kata kata kitunguu maji weka pembeni malizia kukata pilipili boga nyembamba weka pembeni
3.Twanga kitunguu thomu weka pembeni
4.Weka maji kidogo kwenye kibakuli kisha kamua ndimu yako vizuri
5.Saga nyanya zako ziache pembeni
6.Chukua nyama ya kusaga weka ndimu,chumvi na vitunguu thomu
7.Kisha tengeneza maduara ya nyama makubwa kiasi weka kwenye sufuria

JINSI YA KUPIKA MAKARONI YA MADUARA YA NYAMA YA KUSAGA(MEAT BALLS MACARONI).
1.Yapange maduara ya nyama kwenye sufuria safi yafunike yaache yaivie mvuke na yabakie na maji maji kidogo
2.Pasua macaroni yako weka kwenye sufuria na maji na chumvi kisha yaweke jikoni yaache yaive mpaka yalainike kisha mwaga maji yaliobakia kwenye sufuria kwa kuyachuja macaroni yako
3.Rudisha sufuria jikoni acha ikauke maji na mimina mafuta
4.Yakipata moto kaanga vitunguu kisha pilipili boga na kisha karoti
5.Vikipiga brown weka nyanya na chumvi funika kwa dakika 3
6.Kisha ongeza nyanya ya paketi na royco
7.Mimina nyama ya kusaga acha kidogo
8.Sasa weka macaroni yale uliyo chemsha na koroga ili yachanganyike vizuri na nyama na viungo vyengine
9.Acha kwa dakika 2 rosti likipungua na kuingia kwenye macaroni vizuri epua mimina kwenye chombo chako cha kulia weka mezani

Angalizo:
1.Usiweke maji wakati wa kupika rosti hakikisha linakua zito zito
2.Pikia moto wa wastani upishi uwive taratibu
3.Hakikisha huunguzi vitunguu maji wakati wa kuvikaanga

Furahia Macaroni Yako.

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.