MAHITAJI YA JUICE YA UKWAJU NA TANGAWIZI
- ukwaju kiasi
- sukari robo
- hiliki ya unga kijiko kimoja cha chai
- maji kiasi
- Tangawizi mbichi(iliyosagwa) nusu kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA JUICE YA UKWAJU NA TANGAWIZI.
- Chemsha ukwaju,ukipoa weka tangawizi na ufikiche pamoja na ukwaju kisha ukamue rojo lote..kisha uchuje
- Chukua rojo la ukwaju uliochujwa ongeza maji kiasi na weka hiliki tia pamoja na sukari kisha koroga mpaka sukari ikolee vizuri
- Weka katika fridge ikipata baridi tayari kwa kunywa.
