MAHITAJI YA BUTTERCREAM YA KUPAMBIA KEKI.
- Siagi isiyokuwa na chumvi gram 150
- 🍃Icing sugar gram 500
- 🍃Arki ya vanilla kijiko kimoja cha kulia
- 🍃Rangi chakula ya kiasi tu inategemea na wewe mwenyewe unataka ikolee vipi nyingi au kiasi tu au pia unaweza ukatumia rangi nyengine yoyote unayopenda wewe ya chakula
- 🍃Maziwa ya maji ya kawaida vijiko viwili mpaka vinne vya kulia
- 🍃Sprinkle ( hivi vinapatikana supermarket vimekaa kama vipipi flani )
MAELEZO YA KUTENGENEZA BUTTERCREAM YA KUPAMBIA KEKI.
- 🍇Chukua bakuli tia Siagi yako anza kusaga kwa mashine ya cake au mwiko wa kusongea ugali mpaka ibadilike rangi iwe cream
- 🍇Baada ya hapo achia kusaga mimina Icing sugar yako na Endelea kusaga mpaka uhakikishe Icing sugar imechanganyika vizuri
- 🍃Baada ya hapo achia kusaga tia arki ya vanilla au yoyote unayopenda wewe mwenyewe pamoja na Rangi ya chakula yoyote unayopenda wewe mwenyewe pamoja na Maziwa ya maji ya kawaida
- 🍇Endelea kusaga mpaka uhakikishe rangi yako imechanganyika vizuri
- 🍃Chukua cake yako ikate sehemu ya juu kabisa kama imevimba na kama haijavimba si lazima kuikata
- 🍇Anza kuieneza cake yako buttercream juu na pembeni halafu iweke sawa kwa kutumia spatula au kisu cha kusawazishia cake iwe smooth vipo special na vinapatikana maduka ya vifaa vya cake ( au unaweza ukaipamba zaidi )
- 🍃Baada ya hapo ipake sprinkle Jemmy juu ( sprinkle hizi zinapatikana supermarket vimekaa kama vipipi flani )
- 🍇 Baada ya hapo unaweza ukaiweka kwenye fridge cake yako ili ipate kukazana isigande ipate baridi tu
- 🍃Baada ya hapo itoe cake yako kwenye fridge
- 🍃🍇Na mpaka hapo cake yako ipo tayari kwa kula ni rahisi sana
MWISHO!!!.