******#QUEEN_OF_DARKNESS*****
****#WITH_QUEEN_NIRMARY**
***** 05 *****
Na mwanamke wa baharini aliitwa BETILISA pia mtoto wake aliitwa GRACE. Jaribu kutuliza akili mpenzi msomaji usije ukachanganya mafaili. MONALISA ambae ni mama TRACE yeye anaishi nchi kavu. Na BETILISA ambae ni mama yake GRACE alikuwa akiishi baharini. Na kijana ambae ndie mfalme wa giza huko baharini aliitwa HIYAN. Sijui tunaelewana wapendwa!!?
Basi baada ya utambulisho huo mfupi tunaendelea na story yetu.
****#BAADA_YA_MIAKA 18****
Kwa Sasa watoto hao walio zaliwa siku saa na sekunde moja walikuwa Ni mabinti wakubwa na warembo kweli kweli. Grace na Hiyan walikuwa na ukaribu mkubwa Sana kwa sababu walikuwa wakiishi wote na waliishi kwa kuaminishwa na wazazi wao kuwa kwa hapo baadae watakuja kuwa mke na mume. Yaani Mfalme ambae ni Hiyan atakuja kumuoa Grace. Grace na Trace walikuwa na umri sawa wao walikuwa na miaka 18 alafu Hiyan kwakuwa aliwazidi kwa miaka miwili yeye alikuwa na miaka 20.. Pia MONALISA kwa kipindi chote hicho Cha miaka 18 alikuwa akiishi kwa kudhani yule bibi ajuza ndie mume wake wa Ndoa. Lakini kumbe si hivyo.
Siku moja asubuhi na mapema MONALISA aliamka na kuanza kumbwatiza mume wake. Wakati huo mtoto wao alikuwa ameenda shule.
"Yapata miaka kumi na minane kwa Sasa sijauona mwili wako. Mimi na wewe Ni mke na mume lakini tunaishi Kama mtu na Kaka yake. Kwanini kila nikikuomba haki yangu ya Ndoa unanipiga karenda!!? Ina maana wewe hujawahi kunimiss ndani ya hiyo miaka yote tulio ishi bila kuingiliana!?"
"Hivi wewe mwanamke unaakili kweli!? Hayo maneno gani ya kuniambia!? Nilishaa kwambia Sina muda wa kukaa kuanza kuingiliana na wewe. Wewe mwenyewe wafaham majukum yanayo nikabiri"
"Majukum gani hayo!? Au una mwanamke mwingine anae kutimizia haja ya mwili wako!?"
"Shut up!!?"
Kwa Mara ya kwanza Bibi ajuza alimuwasha Kofi MONALISA.
"Whaaaaaaaaat 😮 😮😮"
Hata Mona alishangaa kwani mumewe toka amuoe hakuwahi kumnyooshea hata kidole 👉
#INAENDELEA.......