Notification texts go here Contact Us Buy Now!

QUEEN OF DARKNESS SEHEMU YA 03

 ******#QUEEN_OF_DARKNESS******
   *****#WITH_QUEEN_NIRMARY**
                       ***** 03 ****

Bibi kizee yule baada ya kumsogelea mwanamama yule aliye toka kujifungua muda sio mrefu alimpa heshima mtoto yule ambae alikuwa haelewi chochote ndani ya uso wa dunia aliye zaliwa sekunde chache zilizo pita... Baada ya kumpa Salam katoto kale alitabasam 😊 😊 kana kwamba kanamfaham yule bibi.

Bibi yule alimsogelea mtoto na kumnyanyua alipo mnyanyua mtoto yule alitoa Nuru Kali kwenye paji lake la uso ☀️☀️☀️☀️.

"Waoooooohh huyu ndie malkia aliye kuwa akisubiriwa kwa kipindi kirefu sana. Hatimaye leo amewasili"

Bibi yule aliongea moyoni mwake lakini chaajabu alipotaka kutoweka na yule mtoto alishindwa kabisaa. Kwani kisheria Huwezi kumchukua mtoto ikiwa mama yake mzazi yupo hai... Alafu ukiangalia mtoto mwenyewe Bado ni mdogo hajaanza hata kunyonya.

Basi Bibi yule alimshusha na kumuweka kando ya mama yake Kisha alimnyanyua mama na kuanza kumpa huduma ya kwanza. Baada ya muda kidogo mwanamama yule alianza kurudisha faham zake taratibu. Bibi yule alipoona mwanamama yule anataka kufumbua macho alijibadili na kuuchukua muonekano wa mwanaume ambae ndie mume halali wa mama yule aliye toka kujifungua hivi punde. Ambae kwa Sasa mumewe hayupo Tena duniani.

"Aaaaah mume wangu.. Huo usafiri hujaupata mpaka Sasa!!? Mwenzio nimeshaa jifungua alafu hali yangu si nzuri naomba uniwahishe hospitali"

"Ooh sawa mke wangu Kwanza hongera kwa kuniletea mtoto mzuuri"

"Ahsante mume wangu"

Bibi yule aliye uvaa uhusika wa mume wa mwanamama yule alipo piga jicho lake mlangoni Huwezi kuamini mwili wa mume wa mama yule ulitoweka sehemu isiyo julikana.

Kisha aliendelea kumuandaa mwanamama yule na kumuwahisha kituo Cha afya kwa mujibu wa maelezo yake alikuwa Bado hayuko sawa kiafya hivyo alihitaji uchunguzi zaidi. Je vipi kuhusu baharini!!? Usikose!!! Kufuatilia kigongo hiki kikali kushinda vyote. Yaani hii inaitwa kiboko yao. Pongezi ziende kwako ulie kichagua kigongo hiki

#INAENDELEA....

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.