Notification texts go here Contact Us Buy Now!

QUEEN OF DARKNESS SEHEMU YA 02

 ******#QUEEN_OF_DARKNESS******
      *****#WITH_QUEEN_NIRMARY***
                      ***02***

"Mke wangu hebu subiri nikaite usafiri nikuwahishe hospitali"

Mume aliongea huku akiwa anamlaza mkewe kitandani..

"Mume Wangu uchungu unaniuma Sana nahisi mtoto anataka kutoka Kuja duniani"

"Jikaze mke wangu jikaze"

Huku nako upande wa bahari kulichafuka Kama jinsi mawimbi yake yalivyokuwa yamechafuka.

"Aaaaaaaaaaahhhhhh 😣😣😣😣" Tulia hebu shusha jazba usimbane mtoto atashindwa kutoka vizuri"

Mkunga wa sehemu ya baharini alikuwa akijaribu kumuelekeza mwanamama huyo jinsi ya kumpush mtoto nje.

"Usipumue hebu ziba pumzi usitoe pumzi nje"

"Mmmmmmmmmhhh 😣😣😣😣"

Nje ya chumba hicho Cha mkunga kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakisubiri ujio wa mtoto mpya ndani ya kasri lao.

Kuna mwanaume aliye onekana kachanganyikiwa kuliko Wote inavyo onekana huyu ndie baba wa mtoto huyo anae tarajia Kuja duniani kwa muda mfupi ulio salia.

Huku nchi kavu nako mwanaume yule ambae ndie mume wa mwanamama mjamzito alipo fungua mlango tuu ili kwenda kuomba msaada wa usafiri. Ghafla alivamiwa na wale kunguru wenye njaa Kali na kumshambulia mpaka walipo tosheka. Masikini baba yule alipoteza maisha papo hapo... "Aaaaaaaaaaahhhhhh 😣😣"

Mwanamama aliendelea kulia huku akifikiri mumewe ameenda kuomba msaada nje ili awahishwe hospital. 

Sasa wakati yule mwanamke wa baharini anajifungua huku nchi kavu nako huyu mwanamama mjamzito nae alijifungua. Huwezi kuamini mpenzi msomaji walijifungua wakati mmoja Tena wote kwa pamoja. Na watoto wao walilia vilio kwa pamoja na Wote walizaliwa ilhali wakiwa Ni watoto wa kike. Baada ya kunguru wale waliokuwa wakimshambulia mwanaume yule kusikia sauti ya Kilio Cha mtoto walijikusanya kwa pamoja na kugeuka kwenye umbile la kibinaadam Tena la kutisha.. Mwanaadam huyo alikuwa kwenye taswira ya muonekano wa Bibi kizee aliye zeeka Sana. Baada ya kunguru wale kujiunga na kutokea Bibi kizee. Alipiga hatua na kumfuata mwanamke yule ambae alikuwa hajiwezi.

#INAENDELEA..........

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.