MAHITAJI YA KUPIKA GLAZED DONUTS*
Hamira pakti 2
Maji 1⁄4 kikombe
Maziwa ya vugu vugu kikombe 1+1/2
Sukari 1⁄2 kikombe
Chumvi kjk 1 cha chai
Mayai 2
Samli/kimbo 1⁄3 kikombe
Unga vikombe 5 cups
Mafuta
*GLAZE:*
Siagi 1⁄3 kikimbe
Sukari ya unga vikombe 2
Vanilla kjk 1+1⁄2 cha chai
Maji ya moto vjk 4 -6 vya kula
*JINSI YA KUPIKA GLAZED DONUTS*
GLAZE
Yayusha siagi.
Epua baada ya kuyayuka.
Mimina sukari ya unga na vanilla na changabya vizuri.
Tia maji kjk 1 baada ya kingine hadi upate uzito utakaopendezewa.
DONUTS
Tia maziwa, sukari, chumvi, mayai, samli au kimbo na unga vikombe 2 na hamira.
Saga kwa sekunde 30 huku ukiwa unakwangua bakuli .
Endelea kusaga kwa spidi ya kati kwa dakika 2.
Mimina unga ulobakia na uchanganye.
Funika na acha iumuke kwa dakika 50-60.
(Utajua kama unga umeumuka iwapo ukishika hautojirudi.)
Weka donge lako sehemu ilomwagiliwa unga.
Sukuma upate unene wa 1/2 inchi.
Kata doughnuts.
Funika na acha ziumuke kwa dakika 30-40
Weka mafuta jikoni yapate moto.
Tumbukiza doughnuts kwenye mafuta ya moto.
Geuza doughnuts zikishakuja juu.
Kanga hadi ziwe na rangi ya kahawia dakika 1 kila upande.
Epua kutoka kwenye mafuta na zichuje
Chovya doughnuts kwenye glaze na ziache zipoe.
