Notification texts go here Contact Us Buy Now!

JIFUNZE NAMNA YA KUWA SINGLE MOTHER, NA KUWA NA MAHUSIANO YA KAWAIDA/MAPENZI KAMA WATU WENGINE!

Mwandishi wa makala hii ni

#@Pius Nkanabo.

Moja ya changamoto kubwa katika maisha ya sasa kwa wanawake ni kuwa single mother na hapohapo kupata mwanaume wa kukupenda bila kujali mtoto au watoto wako.

Ingawa sasa hivi dunia imebadilika, suala la mwanamke kuolewa akiwa na mtoto au kuwa na watoto wake na kuwa na maisha yake ni jambo la kawaida lakini bado kuna wanawake wengi ambao wanapata wasiwasi wanapokua na watoto.

Kuna mawazo mengi yanakuja vichwani mwao, kuna maswali mengi ambayo hua wanajiuliza. 

“Hivi nitapendwa tena kweli? Hivi atampenda mwanangu? Hanioni mzee? Atakua kama Baba yake? 

Vipi Baba wa mtoto akileta vurugu? Ndugu wa mume watakubali kweli ndugu yao aoe mwanamke aliyezaa hata kama tunapendana?” Kuna maswali mengi na mengi zaidi ya haya ambayo yanakupa wasiwasi na kukufanya ukose raha ya maisha.

Wanawake wengine hata hulazimika kuolewa na wanaume waliozaa nao hata kama wanawatesa kwa kuogopa tu kuwa single mother. Wengine wanawakubali wanaume ambao wanawanyanyasa na kuwafanya wajihisi takataka kwakua tu wanaamini kua kwa kuzaa kabla ya ndoa basi wanapoteza usichana wao na ile haki a kuringa. 

Haki ya kuchagua inapotea, hivyo katika Makala hii nitakufundisha ni kwa namna gani unaweza kuwa single mother na ukawa na mahusiano ya kawaida tu na ya furaha.

(1) Usimfiche mtoto wako/Usifiche kama una mtoto; Kitu cha kwanza kabisa unachotakiw a kukijua nikuwa mwanao ni Baraka,m mtoto si mkosi hivyo huna haja ya kumficha. Kuna wale ambao washawapeleka watoto wao vijijini na wanataka waitwe dada. 

Hapana hilo ndiyo kosa la kwanza, kama unataka mtu yeyote akupende basi unapaswa kuanza kwa kujipenda kama Mama. Usimfiche mwanao na usimuone kama kikwazo cha kukufanya usiolewe.

Kuna wanawake wengi ambao hawana watoto hawajaolewa kama ambavyo kuna wanawake wengi wenye watoto wameolewa na wanafuraha. 

Sisemi mtoto wako awe matangazo kwamba kila mwanaume unayekutana naye umuambie lakini pia asiwe kificho. Wakati wa kujitambulisha nilazima useme una mtoto mmoja au wawili, unaishi naye, anaishi kijijini kwa Mama yako au yuko kwa Baba yake.

Angalia mwanaume mstaraabu na yule ambaye unaona kuwa huyu hata mimi kanivutia na kama umekubali kutoka naye basi kakuvutia na muambie. Akitaka muonyeshe na hata picha yake kwenye pochi yako, mwanaume anapoona uko comfortable kuwa Mama, huoni aibu na huoni kama ni kasoro au humuoni mwanao kama mzigo basi nayeye ataona hivyo hivyo. 

Lakini kama siku ya kwanza tu ushaanza kulalamika ulivyotelekezewa mtoto na unavyo hangaika niamini atakukimbia kwani ataona kama ni mzigo.

Hapa nataka niweke kamsisitizo kidogo, wakati wa kumtambulisha mwanao, kuseama kuwa una mtoto ndiyo mwanaume atakupima. Ukishaanza kulalamika kuwa umetelekezewa, sijui umesusiwa, ukaongea na mahangaiko yako kutaka uonewe huruma jua kua unamuambia kuwa kama akiwa na wewe basi utakua ni mzigo mkubwa na anaweza kushindwa kuubeba hivyo anakukumbia. Usiongee sana kuhusu mwanao siku ya kwanza, muambie tu una mtoto basi.

(2) Usimuonyeshe mwanao kila mwanaume mtambulishe unapokua siriasi; Katika hauta za kwanza usimuonyeshe au ukamtambulisha mwanao kwa wanaume unaotoka nao. Jiheshimu na mtambulishe mwanao mwanaume ambaye uko naye siriasi tu.

 Hata kama mtoto ni mdogo lakini sio kila mwanaume anayekutongoza unampeleka kwako, hapana, akitaka kuja kwako muambie una mtoto hawezi kwa wakati huo.

Iko hivi unapokua unamuonyesha mwanao kwa kila mwanaume mbali na kumuathiri mtoto hukuathiri na wewe. Kwamba mahusiano yenu hayajawa siriasi, umemuonyesha mwanao baada ya muda kakuahca. Unaanza kuwaza labda kaniacha sababu ya mtoto, kumbe jamaa hata hakua na mpango nawe hata kama ungekua bikra angekuacha tu, lakini ile hali ya kuhisi umeachwa kwasababu ya mtoto itakufanya ujichukie na kuona kama kuwa na mtoto ni laana.

(3) Acha kumzingumzia mwanao kila mara mnapotoka wawili; Yes umehsamtambulisha, kashajua kua una mtoto, kama hajaulizia tena acha kumzungumzia mwanao kila saa. 

Kwa kifupii nikuwa hata kama unampenda mwnaao vipi acha kuwa Mama kila wakati, dakika mbili mwanangu hiki, mwanangu kile, mwanangu anaumwa, jana ilikua hivi, juzi ilikua vile, mwanangu anapenda hiki, Baba yake kafanya kile na mengine kama hayo.

Huyo mwanaume anatakiwa kujua kuwa pamoja na kuwa una mtoto lakini hata yeye atapata nafasi ya kukufaidi. 

Sasa kama akiona unazungumzia mtoto kila wakati atawaza kuwa kama hatujaoana yuko hivi tukioana itakuaje. 

Lakini kisaoikolojia inamfanya kumchukia mwanao anakua kama anamuonea wivu kuwa anamnyang’anya penzi lako. Nilazima umuonyeshe kuwa naye ana umuhimu hivyo muongelee mwanao kidogo mengine yawe yenu.

(4) Hakikisha unakipato chako, weza kumhudumia mwanao; Kama ni single mother na unatamani kuwa na mahusiano ya furaha suala la kazi ni lalazima. 

Nilazima uwe na kipato flani cha kuweza kukuhudumia wewe na mwanao. 

Hata kama Baba wa mtoto ana hela vipi na anawahudumia kila kitu kama huna hela zako wanaume watakukimbia. Kuna sababu kuu mbili hili linatokea, sababu ya kwanza nikua mpenzi mpya atamuonea wivu baba wa mtoto.

Kwamba akiona kuwa hela zote zinatoka kwa Baba wa mtoto moja kwa moja atajua kuwa yeye ndiyo hukupangia maisha hivyo hata mkioana huwezi kuamua mambo yako mwenyewe mpaka huyo Baba na atahisi unaweza hata kumkubali kimwili kwakua anakupa hela zote. Pili nikwakua atawaza huyu nikimuoa mzigo wote nitabeba mimi kwamba baba wa mtoto anaweza kuacha kutoa matumizi hivyo nikalea mtoto wa mwenzangu.

Nikweli naakupenda lakini suala la hela nalo ni gumu, nilazima uwe na kipato chako ili hata kama unapokea pesa kutoka kwa Baba wa mtoto asiwe ana kicontrol muda wote.

 Lakini pia ukiwa na kipato chako utamtoa wasiwasi mpenzi mpya kuwa hatabeba mzigo wa kulea peke yake. 

Atajua kuwa kazi yake inaweza kumlea mwanao hata kama mkioana itakua kinyume chake. Hiki ni kitu ambcho wanaume wengi hukiwaza sana kubeba majukumu ya mtu mwingine.

(5) Omba hela kama wanawake wengine na si kwaajili ya mwanao; Upo kwenye mahusiano, labda ndiyo machanga lakini hata yana muda ila kila mara mtoto anaumwa, mtoto anataka nguo ya sikukuu, mtoto hiki unaomba pesa. 

Kumbuka hapo hajakuoa hivyo hata wewe kukuhudumia si kazi yake, lakini ushaanza kumpa na jukumu la kumhudumia na mwanao. Atakimbia akijua kuwa kama hapa sijamuoa ni hivi nikimuoa ni itakuaje.

Homba pesa kama wanawake wnegine, ukiwa na mahitaji mengine kam aya nywele, nguo zako na vitu vyako vingine. 

Hata kama hizo hela utazitumia katika kumhudumia mwanao lakini asijue. 

Muombe pesa kuhusu mwanao kama kuna kitu kikubwa kama ugonjwa, hapo kama huna muambie na angalia ata kusaidiaje na hicho pia kitakua kipimo kuwa anakupenda au la na kama akikuoa na mwanao akapata tatizo atakua Baba kwake au la?

(6) Ondoka unapoona dalili kuwa hampendi au hafurahii wewe kuwa na mtoto; Najua unahamu sana ya kuolewa, una hamu ya kuwa na mtu, lakini kama unataka kuwa na furaha katika ndoa au mahusiano yako ni lazima uwe na mtu ambaye kwanza atakubaliana kuwa wewe ni Mama, pili atakubaliana kuwa unampenda mwanao kuliko kitu kingine chochote kile. Kwamba kama anakupenda nilazima akubaliane na wewe kuwa Mama.

Akianza mambo ya mtoto aende kwa Baba yake, mara aende kwa Bibi yake na mambo mengine kama hayo muambie hapana. Mimi ni Mama yake na nitamlinda mimi, ajue kwamba hata kama atenda kwa Baba yake si kwakua yeye kataka au hata kama utampeleka kwa Bibi yake si kwakua yeye kataka bali kwakua umetaka wewe na unaona mazingira yanaruhusu. Ukishaona chuki kidogo tu kwa mwanao ondoka kabisa.

Hutakua na furaha katika maisha yako kama utaolewa na mwanaume ambae anamchukia mwanao. 

Hilo nina uhakika nalo kwani upendo wa Mama kwa mtoto ni kitu tofauti. Mwanaume yeyote unayekutana naye anapaswa kulifahamu hilo. Mwisho nimalizie tu kwa kusema, usiogope, kufanya kitu kibaya na kama mwanaume akikuacha kwakua una mtoto na unampenda basi badala ya kulia tabasmau na mshukuru Mungu kwani kuna wengi wapo kwenye ndoa na wapo tayari kutoka ili tu wapate watoto.

#@Pius Nkanabo

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.