Tumejifunza kwamba mateso ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, kwamba hakuna namna tunaweza kuondokana na mateso.
Hivyo kujiuliza
naondokanaje na mateso kwenye maisha yangu ni kujidanganya.
Swali sahihi kwako kujiuliza ni kwa nini nateseka, mateso ninayopitia yana maana gani kwangu?
Kwa swali hilo ndiyo unaweza kujua thamani sahihi ya mateso yako,
ndiyo unaweza kuchagua mateso sahihi kwako na kuyafurahia maisha yako licha ya kuwa na mateso.
Kujitambua kuna ngazi tatu ;
Ngazi ya kwanza ni kujua hisia ulizonazo , hizi ni muhimu kwa sababu ndiyo zinatawala sehemu kubwa ya maisha yetu.
Ngazi ya pili ni kujua kwa nini unakuwa na hisia ulizonazo.
Kama una furaha
ujue kwa nini na kama una huzuni kwa nini. Kama una chuki kwa nini na kama
una upendo kwa nini.
Ngazi ya tatu ni kujua maadili na misimamo binafsi, hapa ni kujua ni vitu gani
unathamini kwenye maisha yako, na unajipima kwa vigezo gani.
Ngazi hizi tatu zinachimba ndani ya kila mtu na unapozitambua, unaweza kujua
thamani ya mateso unayopitia kwenye maisha yako.
