Notification texts go here Contact Us Buy Now!

SECRET LOVE SEHEMU YA 03, 04, 05, 06, 07 & 08

 SIMULIZI: SECRET LOVE

MTUNZI: AISHA KHAN

SECRET LOVE SEHEMU YA 03


TULIPOISHIA: "Unasema? Yupi" hapo alinyanyuka kwenye kiti na kuchomoa macho kama mlusi aliyebananishwa.


"Mfupi ila simfahamu"


"Kakutuma nini"


"Eti nije kumwambia dada Tabu amkute chini ya mwembe"


SONGA NAYO


Alex Kama kawaida yake kupandisha hasira bila kufikiria wala kufanya uchunguzi, alianza kunilalamikia na kunifanya nitoke ndani haraka.


"Ndio mume wangu" niliongea kwa sauti ya unyenyekevu bila kujua mwenzangu tayari anakirusi.


"Kwanini unanipandishia sauti" alinihoji na kunifanya nishangae bila kumjibu chochote.


"Huo umalaya wako ndiyo unakupandisha kiburi... Sasa ngoja uone"


Alex alinishika kwa nguvu tayari kuanza kunivuta huku akinipeleka nisikokujua. njia nzima nilijaribu kumuuliza wapi ananipeleka ila hakutaka kunipa nafasi. Tulifika pembezuni mwa mto na kumkuta kijana flani kasimama chini ya mwembe.


Alex alinisukumu nikajikuta nimemuangukia mkaka yule ambaye alizidi kutushangaa.


"Samahani jamani" nilimuomba msamaha mkaka yule.


"Ongeeni sasa mlichopanga kuongea" aliongea Alex na kunifanya nizidi kumshangaa maana kijana huyo nilikuwa simfahamu.


"Brother kuna nini kwani?" Mkaka yule ambaye walikuwa rika moja aliamua kujishusha ili isitokee vurugu zaidi.


"Uliyekuwa unamhitaji huyo hapo, kwahiyo ongeeni sasa"


Mkaka yule baada ya kuona Alex anatafuta Shari aliamua kuondoka, ila kabla hajampita Alex alimshika Shati na kumfumua ngumi ya shavuni. Vita ilianza huku mimi nikiwa nashuhudia bila kutoa msaada wowote. Kiherehere cha Alex kilimponza maana alipigwa kama mtoto mdogo.


"Muonye mumeo, kama nimekupenda wewe siyo lazima na yeye nimpende" mwanaume huyo aliniambia na kuondoka zake huku mimi kimoyo moyo nikiwa nashangilia kwa furaha.


"We njoo hapa" Alex aliniita Ila sikuwa tayari kumsikiliza maana nilijua vibao vile ningegeuziwa mimi, haraka nilikimbia na kumuacha akinilalamikia.


"Mama naogopa kurudi nyumbani" niliongea kwa huzuni huku nikiwa nipo nyumbani kwetu, na muda huo ilikuwa tayari usiku.


"Ndoa ndivyo ilivyo, yakupasa kuvumilia. Ila yote uliyataka mwenyewe" mama aliniambia.


"Kwahiyo mama... mpaka sasa tu hutaki kuamini kwamba nilibakwa?"


"Ntaamini vipi na ulikuwa kwake? Afadhali useme nilikuwa natoka mtoni kuchota maji labda Hapo ningekuelewa, ila hapo binti yangu huwezi niaminisha"

Maneno ya mama yalinifanya nijiinamie huku nikilia.


"Usilie mwanangu"


"Hapa nilipo ni mjamzito" nilimwambia kwa uchungu.


"Jambo la kheri sana"


"Mamaaa....."


Muda huo Alex alifika na kusimama mbele yetu bila kutoa hata salamu kwa mama yake mkwe.


"Umekuja kufanya nini huku" alinihoji na kunifanya nikae kimya kwa kushangaa hali Chafu aliyonayo. Alex aliona Nampotezea muda alinishika mkono na kunipeleka huku akinipiga vibao kichwani. Mama alitusindikiza kwa macho bila kujua atanisaidia vipi.


"Acha Alex" niliongea baada ya Alex kunifikisha nyumbani na kuanza kunipiga ngumi za tumbo.


"Alex acha jamani"


"Hii mimba si ndo inakupa kiburi, sasa naenda kuitoa" aliongea Alex na kuendelea kunipiga bila kunionea huruma. Kama bahati aliingia Paulina na kuchukua mpini tayari kumpiga nao kichwani.  Na Hapo ndipo nilipata kupumua maana Alex alidondoka chini na kuzimia.


"Uko sawa Tabu" alinihoji huku mimi nikiwa natetemeko mwili mzima kwasababu ya kipigo. Paulina hakutaka kuniacha alinishika mkono na kuniinua ili tuelekee kwao kwa Msaada zaidi.


"Kwahiyo ndo umlete hapa?" Shangazi alihoji baada ya kuniona.


"Mama embu kuwa na roho ya huruma, huyu ni damu yetu ujue" Paulina alinitetea huku nikiwa nimetulia.


"Najua hilo ila yupo kwenye ndoa na siyo heshima binti wa kitanzania ambaye ameolewa arudirudi kwao bila ridhaa ya mumewe" maneno ya shangazi yaliniingia Moyoni na kuniumiza.


"Shangazi, samahani naomba kwa leo tu nikae kesho naondoka" niliongea kwa upole na kumfanya shangazi aingie chumbani kwa hasira.


"Usijali... Kwanza unajisikiaje?" Paulina alinihoji.


"Tumbo inaniuma sana"


"Sanaaaaa?"


"ndiyo"


"Moyo wangu unaniambia twende hospitali, embu twende kwanza"


Nilimsikiliza Paulina ikabidi kuelekea hospitali.


"Usijali mimba  Haijaharibika. Mwenyezi Mungu yupo na wewe , ila huyo mwanaume anayekupiga kiasi hiki ana moyo wa kibinadamu kweli?" aliniambia nesi na kunifanya nitabasamu kwa uchungu bila kumjibu.


Asubuhi na mapema tulirudi nyumbani kwa shangazi maana ilitubidi kulala huko kutokana na hali yangu kuwa mbaya.


"Wallah naapa Tabu, kama ningekuwa wewe aisee ningemuwekea sumu mshenzi huyo" aliongea Paulina huku tukiwa tupo njiani.


Tulipofika nyumbani tulishangaa kumkuta Alex kasimama akitusubiri kwa hamu.


"Mungu wangu" niliongea kwa hofu kisha Esta akanishika mkono ili kunituliza.


"Ndo huyo sasa mpeleke" aliongea shangazi ambaye alikuwa amekaa kwenye kigoda huku akinywa chai taratibu.


"Mamaaa..." Paulina alimuita kwa uchungu.


"Mama kitu gani? Mume kaja hapa anamtafuta mkewe ulitaka nisemeje?"


"Twende nyumbani" Alex aliniambia.


"Hauwezi kwenda naye kirahisi rahisi namna hiyo, au umesahau ulivyotaka kumuuwa?" Aliongea Paulina kishujaa.


"Siongei mara mbili, Tabu ongoza njia"


"Acha tu niende" nilianza kujitoa kwa Paulina ili kuepusha balaa.


"Tabu una nini wewe"


"Ntakuwa sawa wala usijali"


"Sasa sikiliza we Shemu, siyo kwamba tulikukabidhi huyu mwanamke ili umuue..tungetaka kumuua tungemuua wenyewe, sasa basi.. muheshimu laa sivyo ntayachomoa moyo wako" maneno ya Paulina yalimfanya Alex atabasamu kwa zarau kisha kunifuata mimi niliyeanza safari.


"Mama sijapenda tabia yako" Paulina alimwambia shangazi na kuingia Zake ndani.


"Unahitaji nikufanye nini?" Alex alinihoji baada ya kufika nyumbani.


"Nisamehe Alex"


Alex alitabasamu na kunirushia jembe nikalime.


"Sitaweza, hali yangu siyo nzuri" niliongea huku nikiwa nimeanza kulia, ila kwa jicho nililokatwa ilinibidi kuelekea shamba.


Majira ya mchana nilikuwa shambani huku nikiwa napumua kwa shida ukija kuangalia kichapo nilichokipata na vilevile nilikuwa nanjaa kali. Nilikumbuka mama alivyonitazama siku ile ninavyopigwa bila hata kunitetea kwa maneno basi, hapo ndipo nilizidisha huzuni. Muda huo alikuja mdada jilani yake na Paulina na kuniambia.


"Tabu... Poleni jamani"


"Poleni? Kwanini mbona tuko sawa"


"Kumbe hujasikia?"


"Kusikia nini?"


"Mume wa shangazi yako amefariki"


"Unamaanisha mjomba?" Nilimhoji kwa presha.


Unahisi nini kitatokea?



SECRET LOVE SEHEMU YA 04


TULIPOISHIA: "Poleni? Kwanini mbona tuko sawa"


"Kumbe hujasikia?"


"Kusikia nini?"


"Mume wa shangazi yako amefariki"


"Unamaanisha mjomba?" Nilimhoji kwa presha.


SONGA NAYO


"Ndiyo! Yaani muda huu huu" binti huyo Baada ya kunipa taarifa zile, aliondoka na kuniacha nikilia. Sikutaka kupoteza muda haraka nilielekea kwa shangazi. Hali niliyoikuta nyumbani ilinisikitisha na kuungana na wenzangu kuomboleza.


Msiba uliendelea ikabidi wanakamati wapange ratiba kamili ya mazishi.


"Hapana tunamsubiri kijana wangu  Ulimwengu hatuwezi kuzika na bado hajafika" aliongea shangazi na kuwafanya wazee wa kijiji kutulia. Haikuchukua muda, Ulimwengu alifika pamoja na kijana flani.


"Haipaswi kulia namna hiyo, kikubwa tumuombe Allah amlaze mahala pema" aliongea Ulimwengu ambaye ni binamu yangu na kutufanya tupunguze kilio. Mazishi yalienda vizuri tukabaki tukiomboleza zile siku tatu za msiba.


"Yaani shemeji ni sheitwani, hata kufika msibani kweli?" Aliongea Paulina huku tukiwa tumetulia jikoni tukiandaa chakula kwa ajili ya wageni.


"Achana na Alex anahisi yeye ndiye alijiumba"


Muda huo aliingia Ulimwengu na kukaa pembeni yangu.


"Mpenzi wangu ndiyo ukaamua kunisaliti kweli" utani wa binamu ulinifanya nitabasamu na kushusha macho chini.


"Mbona umekonda hivyo Nini shida mke wangu" Ulimwengu alinihoji.


"Hapana kaka hamna shida labda ni hii hali ya ujauzito niliyonayo"


"Hivi kaka... Yule uliyekuja naye ni nani?" Paulina alimhoji.


"Boss wangu"


"Bosi wako?"


"Ndiyo"


"Kivipi mbona mdogo sana"


"Eeeee hana wazazi ,alipo ni ya tima so yeye ndo mlisi wa kampuni ya baba yake"


"Toba " Paulina jicho lilimtoka na kutamani kumjua zaidi.


"Anamchumba? Halafu kaka..." Kabla hajamalizia Ulimwengu alinyanyuka na kumwambia.


"Maswali yako siyawezi"

Aliondoka huku Paulina naye akamfuata nyuma huku akiendelea kumsumbua. Nikiwa nimetulia zangu, alikuja kijana yule na kuniambia.


"Samahani naweza kupata maji ya kuoga"


"Ndiyo, ya vuguvugu?" Nilimhoji.


"Utakuwa umetisha sana" mkaka huyo aliondoka na kuniacha nikichakalika ili kumtengea maji bafuni.

Baada ya muda nilimtengea na kwenda kumuita, kabla sijaingia ndani nilishangaa kumuona Alex akiwa amekaa na vijana waliyopo msibani.


"Mungu wangu nini tena" nilijisemea moyoni na kuamua kumpotezea.


"Samahani... Maji tayari bafuni" nilimkuta akiwa amekaa kwenye mkeka pamoja na familia nzima akiwemo mama.


"Oohh ok Asante sana" aliongea na kunyanyuka tayari kutoka ndani. Shangazi alinitazama vibaya mpaka nikashindwa kumuelewa. Niliamua kukaa pembeni ya Paulina ili kumueleza kuhusu Alex.


"Alex yupo hapa" nilimwambia nikimnong'oneza.


"Naenda kumfukuza" aliongea Paulina huku akitaka kunyanyuka ila nilimzuia kwa kumshika mkono.


"Hapana"


Muda huo alikuja mtoto wa kiume na kuniambia.


"Dada Tabu... Yule mkaka aliyopo bafuni kanituma nije kukwambia umpelekee taulo eti uitazame kwenye begi yake"


Kabla sijanyanyuka shangazi alinikalisha na kusema.


"We nenda kamwangalie mumeo, em Paulina mtafutie taulo Jabir"


"Kumbe jina lake Jabir " aliongea Paulina Haraka kuelekea chumbani nami nikaelekea jikoni ili kuendeleza na majukumu yangu. Nikiwa nipo jikoni aliingia Alex na kusimama juu yangu .


"Kwanini jana hukurudi nyumbani?"


"Ningerudi vipi na msiba huu"


"Aaaah yaani huu msiba ni bora kuliko mimi"


"Heee Alex wewe ni kiumbe gani lakini"


"Usinipandishie mdomo eti kisa upo kwenu, ntakupiga nakwambia"


"Yaishe basi"


"Leo ole wako ulale huku utaisoma namba"


Upande wa huku Paulina alimpelekea Jabir taulo, alipofika karibu na bafu alijikohowesha na kusema.


"Samahani nimekuletea taulo" 


"Oohh asante"


Jabir alinyoosha mkono na kukabidhiwa taulo. Ndipo Paulina alirudi akiwa anachekacheka kwa furaha.


Upande wetu ubishi uliendelea.


"Sahau mimi kuja huko, ntakaa hapa mpaka pale familia itakapokuwa sawa" niliongea na tayari kumpuuzia huku nikiendeleza majukumu yangu.


Alex kwa utata wake na roho mbaya iliyojaa chuki na fitina, Alinikata kibao na kuondoka zake, kiukweli moyo uliniuma nikaamua kuacha kupika na kuelekea nyuma ya nyumba ili kulia. Nilikaa huko huku nikiomboleza kiasi kwamba nikatamani kheri angekuwa mimi ndiye nimefariki. 


"Unalia?" Nilishtushwa na sauti ya mwanaume ambaye sikuweza kuitambua. haraka kugeuka kumtazama.


"Oohh samahani" niliongea huku nikifuta machozi kisha nikanyunyuka Baada ya kumuona Jabir ambaye kwa haraka nilielewa huwenda alikuwa anatafuta mtandao ndiyo maana kaja nyuma ya nyumba.


"Pole kwa msiba naelewa jinsi gani unavyojisikia"


"Nimeshapoa"


"Ila siyo vizuri kwa mrembo kama wewe kulia maana vijana wengi unawapa Tabu"


Maneno ya Jabir niliyaelewa na kutambua ni kijana mcheshi asiyekuwa na majivuno.


"Naitwa Jabir vipi kuhusu wewe" Jabir alinipa mkono, kiubanadamu ilinibidi kumpa na wangu ili asijisikie nimemzarau.


"Naitwa Tabu"


Kwa bahati mbaya Alex alikuwa anapita pita huku akivuta sigara kiuficho maana msibani hairuhusiwi mtu yeyote kuvuta sigara wala kunywa pombe. Ndipo alipotuona tulivyoshikana mikono.


Unahisi nini kitatokea!

SECRET LOVE SEHEMU YA 05


TULIPOISHIA: Kwa bahati mbaya Alex alikuwa anapita pita huku akivuta sigara kiuficho maana msibani hairuhusiwi mtu yeyote kuvuta sigara wala kunywa pombe. Ndipo alipotuona tulivyoshikana mikono.


SONGA NAYO


Kwa bahati mbaya Alex alikuwa anapita pita huku akivuta sigara kiuficho maana msibani hairuhusiwi mtu yeyote kuvuta sigara wala kunywa pombe. Ndipo alipotuona tulivyoshikana mikono. 


Alex alikunja uso ila kwa hali ya Jabir aliyonayo kimwonekano aliogopa kuanzisha vurugu ikambidi kurudi nyuma. Majira ya jioni Alex alinitoa jikoni huku akiwa ananipiga makofi jambo ambalo liliwashtua watu waliyopo msibani, mama na shangazi walitoka ndani huku wakishangaa ninavyopigwa. Kama bahati Ulimwengu alifika na kushuhudia tukio lile.


"We mshenzi" Ulimwengu haraka alitufuata na kumpiga ngumi Alex. Bila kupoteza muda alimpiga mpaka Alex akaanza kutokwa na damu puani.


"Toka hapa sasa hivi" Ulimwengu alimwambia Alex bila mzaha.


"Natoka vipi bila mke wangu" Alex aliongea kwa zarau na kumfanya Ulimwengu amchote mtama tayari kwenda chini.

 

"Poa we si umenipiga utaona" Alex alianza kuchamba huku akielekea kwake.


"Na wewe, uliolewaje kwa mvuta bangi kama yule?" Ulimwengu alinigeukia ila kwa wakati huo sikuwa na neno zaidi ya kulia.


"Basi" Ulimwengu alinivuta na kunikumbatia huku akiendelea kunibembeleza, yote yaliyotokea Jabir alikua anashuhudia.


Baada ya muda majira ya usiku tulikaa wa nne huku tukiwa tunapiga stori mbalimbali.


"Wanawake wanamatatizo wallah.. taarifa hii mngenipatia kabla ningekuja" aliongea Ulimwengu na kumfanya Paulina agongelee msumali.


"Yaani kaka hukuwepo, nakwambia Tabu anapigwa sawa sawa na miaka yake. Halafu hapa alipo ni mjamzito ila juzi kati nimemkuta Alex anampiga ngumi za tumboni eti anataka aitoe mimba"


"Dah! Huyo mtu mkatili sana" aliongea Jabir .


"Na wewe umezidi... Nani alikwambia ukurupuke kuolewa" Ulimwengu aliniambia.


"Hapana Bina, ni story ndefu" nilimjibu nikilia.


"Hiyo story nataka kuisikia maana haieleweki binti niliyemuacha mpole muoga wa wanaume leo hii eti kaolewa tena kwa jambazi" Ulimwengu alizidi kuonyesha ni jinsi gani tukio Lile lilimkwaza.


Taratibu nilianza kuwapa mkasa kilichonikuta mpaka leo hii ninavyohangaika, kiukweli story yangu iliwahuzunisha mno.


"Jaribu kuacha ndoa, rudi nyumbani" aliongea Jabir.


"Sawa" nilijibu kwa upole.


"Hapana Tabu ongea ukweli. Mwaya ukweli ni kwamba mama hamtaki vilevile na mama yake hamtaki. Eeee kwani uongo" Paulina aliongea.


"Unasemaje wewe?" Ulimwengu alihoji.


"Ndiyo. Yaani Tabu huwa anakuja akiwa anabubujikwa na damu anaomba Msaada kwa mama ila mama anamfukuza kama mbwa na hata akielekea kwa mjomba anafukuzwa hivyo hivyo"


"Nisikilize Tabu, hata siku nikiondoka utaendelea kuishi hapa na wala nisije kusikia umerudi kwa huyo mshenzi" aliongea Ulimwengu.


"Kweli bina?" Kiukweli sikuamini kama kuna mtu angeweza kutokea na kuja kunitetea. Nilishukuru zaidi ya kumshukuru.


Baada ya muda, Paulina alikuwa amekaa na shangazi huku wakijadili jambo fulani.


"Hakikisha unamteka kiasi kwamba aondoke akiwa ameanza kupanga mipango ya ndoa. Ulimwengu kaniambia huyu kijana ni tajiri kuliko yaani anamali mpaka zingine hazijui zilipo" maneno ya shangazi yalizidi kumpagawisha Paulina.


"Sasa mama alikuja huku kwanini?"


"Ulimwengu anakwambia huyu kijana anaroho nzuri kuliko kitu chochote. Eti alifanya kuona barua ya kaka yako ya kuomba likizo kwa ajili ya msiba hapo papo akamwambia lazma waje wote"


"Dah natamani muda huu anitongoze"


"Eee kuwa mjanja maana hapa muda wowote wanaweza kuondoka"


Upande wangu nilikuwa nimelala sebuleni kwenye mkeka huku nikilia kutokana na maumivu tumboni. 


"Jikaze na wewe" aliongea mama yangu ambaye alikuwa amekaa pembeni yangu, muda huo alikuja Jabir na kumuuliza mama.


"Mbona analia?"


"Oohh utamuweza huyu" mama alijibu huku akitabasamu. Ndipo Jabir alisogea nilipo na kuchuchumaa karibu yangu.


"Tabu vipi hali yako?"


"Siyo nzuri"


"Unajisikiaje"


"Tumbo inaniuma sijui kwanini"


Jabir haraka alielekea chumbani ndipo alitoka akiongozana na binamu Ulimwengu.


"Eti mke wangu vipi hali" Ulimwengu alinihoji kiutani.


"Naumia tumboni" nilimjibu ndipo aliniinua kwa ajili ya kunipeleka hospitali.


Taratibu tulitoka ndani na kuelekea kunako gari waliyokuja nayo.


"Kaka Tabu amepatwa na nini" Paulina alihoji na kutufuata. Tulipanda gari na kuelekea hospitali. tukiwa tupo Ndani ya gari huku Mimi na Paulina tukiwa tumekaa nyuma huku Ulimwengu akiwa anaendesha gari pembeni yake Jabir.


"Tabu uko sawa?" Jabir alinihoji baada ya kugeuka nyuma kunitazama.


Gafla mbele tulimuona Alex akiwa amesimama barabarani huku mkononi akiwa ameshikilia panga, mapigo ya moyo wangu yalinienda mbiyo huku nikijiuliza nini kinaendelea.


"Huyu mshenzi namgonga" aliongea Ulimwengu huku akiwa ameshikilia uskani kwa hasira ishara amedhamiria kumgonga.


Unahisi nini kitatokea?


SECRET LOVE SEHEMU YA 06


TULIPOISHIA: Gafla mbele tulimuona Alex akiwa amesimama barabarani huku mkononi akiwa ameshikilia panga, mapigo ya moyo wangu yalinienda mbiyo huku nikijiuliza nini kinaendelea.


"Huyu mshenzi namgonga" aliongea ulimwengu huku akiwa ameshikilia uskani kwa hasira ishara amedhamiria kumgonga.


SONGA NAYO


Mimi na Paulina tulifumba macho huku Ulimwengu akiwa amekunja uso akmtazama Alex ambaye mtungi ulikuwa kichwani na kumuendesha utakavyo. Kabla hajamfikia alisimamisha gari na kuniuliza.


"Nimgonge?"


Kabla sijajibu Alex alisogea tulipo na kuanza kuniita huku akilia.


"Mke wangu wewe ni Malaya na nakwambia ntakuua"


"Achana naye" Jabir aliongea kistaarabu.    ndipo Ulimwengu aliwasha gari na kuendelea na safari.

 Usiku huo nilitibiwa vizuri maana pesa ilikuwepo yakutosha.


Kiukweli uwepo wa binamu yangu ulinifanya nijivunie nakutamani aendelee kuwa karibu yangu maana shangazi na mama walilazimika kunipenda. Siku iliyofuata nilichukua ndoo na kuelekea mtoni kwa ajili ya  kuchota maji, nikiwa nipo Njia nilishangaa kuona mtu pembeni akinipiga picha kupitia camera. Kwa aibu nilishusha macho huku nikiwa nimesimama.


"Wow sasa umepona" aliongea Jabir maana yeye ndiye alikuwa ananipiga picha.


"Ndiyo"


"Unaelekea wapi?"


"Mtoni"


"Kufanya nini?"


"Kuchota maji"


"Oohh embu twende wote nami nikaangalie kulivyokuzuri"


Nilitabasamu kisha tukaongozana mtoni. Stori za Jabir zilinifurahisha maana alikuwa ni mcheshi mno.


"Fanya hivi" Jabir alinyoosha mguu na kuniambia na mimi ninyooshe. Kwakuwa hali yangu siyo majivuno, nilinyoosha kwa aibu.


"Tulia kama dakika thelathini"


"Hapana siwezi"


"Inatakiwa uweze ili mtoto aje akiwa anafanana na mimi"


Hapo nilitabasamu.


"Tabu"


"Abee"


"Acha uvivu jitahidi kufanya mazoezi... Haijalishi una mume wa aina gani ila tambua hicho ulichokibemba tumboni ni cha thamani kubwa. Najua unapitia marefu mpaka huwezi kuyaelezea yakupasa upambane na uchukulie kama mitihani"


"Nashukuru sana"


"Kliniki unaenda?"


"Hapana"


"Siwezi kukuuliza kwanini ila now anza. sawa!"


"Asante jamani" nilijibu huku nikiwa nimeanza kulia maana niliona kuna mambo mengi sifanyi na nihatari kwa mtoto. Kulia kwangu kulimhuzunisha Jabir ambaye alinisogelea taratibu na kunikumbatia.


"Mama acha kulia unaniumiza huku niliko" Jabir aligeuza sauti na kuongea kama mtoto ili kuweza kunitoa kwenye mudi huo. Kiukweli alinichekesha kiasi kwamba nikasahau kulia.


"Umeacha kulia?" Alinihoji huku akiwa amenishika begani.


"Ndiyo" nilikubali.


Tuliendeleza story huku tukiendelea na safari.


"Wow mbona sehemu nzuri hivi!" Aliongea Jabir baada ya kufika mtoni. Nilichota maji na kujitwisha ndoo.


"Utaweza kweli?" Jabir alinihoji.


"Ntaweza" nilimjibu kwa aibu na kuanza kutembea.


"Emu kwanza"


Jabir alinitua ndoo huku akiendelea kusema.


"Ntakusaidia kwasababu Wewe ni mjamzito hutakiwi kuteseka namna hiyo" maneno ya Jabir yalizidi kunipa faraja maana katika maisha yangu sikuwahi kumuona mwanaume anayeonesha kunijali.


"Asante jamani"


Tulianza kwenda mdogo mdogo huku akiniuliza maswali mbalimbali.


"Viumbe hawa bado tu wanaishi duniani?"


"Unamaanisha Alex?"


"Ndiyo! naona ni katili sana"


"Anafanya ukatili kwangu tu. Kwasababu jina langu linaniponza"


"Tabu?"


"Mama alinipanga jina hili kwasababu nisizozijua"


"Na vipi ukimuuliza"


"Hanijibu kitu zaidi ya kunitukana"


"Pole ila mpende kwakuwa bado yupo hai. Now natamani ningekuwa kama wewe"


"Unaongea hivo kwasababu mama yako alikuwa mwema sana kwako"


Muda huo Jabir alipokea simu.


"Yes babe... Kuna tatizo gani?

Uso wa Jabir ulibadilika na kupokea mshangao baada ya kumsikia mpenzi wake aliyopo jijini dar es Salam akilia bila kutoboa, na hapo simu ilikatika na kumuacha Jabir akiita.


"Hallo, hallo"


"Kuna tatizo?" Nilimhoji ila hakujibu zaidi ya kuniambia tuwahi nyumbani.

Tulipofika nyumbani Jabir hakuweza kufanya chochote zaidi ya kuchukua begi ili kuweza kuondoka.


"Jamani mwanangu mbona haraka hivi" aliongea shangazi huku sote tukiwa tupo nje ili kumsindikiza.


"Hapana mama nimepata dharura naimani Ulimwengu mtakuwa wote na kama kuna chochote kikatokea nyuma yangu msisite kunijulisha" 


"Ntakukumbuka Jabir" aliongea Paulina huku mimi nikiwa namtazama tu.


"Ntakumiss pia" kauli ya Jabir ilimpa faraja mno. Ndipo Jabir alinigeukia na kuniambia.


"Hakikisha unakula vizuri, pia fanta mazoezi kama yale niliyokuonesha naimani utapata mtoto mzuri kama wewe" kiukweli maneno yake yaliuchoma moyo wangu maana nilikuwa nimeanza kumzowea ghafla. Shangazi na Paulina walishangaa mno na kushindwa kuniuliza chochote muda ule.


Tulimuaga kwa furaha iliyojaa huzuni maana tulitamani aendelee kuishi nasi milele na milele. Ndipo Gari iliondoka taratibu.

Baada ya muda tulishangaa kuiona ikirudi na kusimama tulipo, ndipo Jabir alitoka na kunifuata nilipo.


"Nilikuwa nimesahau"


"Umesahau nini mwanangu" shangazi alimhoji huku akijishobokesha na kumsukuma Paulina mbele yangu kitendo kilichomuumiza Paulina.


"Samahani kidogo" Jabir alimuomba Paulina asogee pembeni maana alikuwa amenizuwia.


"Oohh" Paulina haraka alisogea. Ndipo Jabir alivua Cheni ndogo aliyokuwa amevaa na kuushika mkono wangu tayari kuniwekea Cheni hiyo kiganjani.


"Hii utampa mtoto endapo utakapomsimulia kuhusu jamaa mpumbavu mpumbavu uliyewahi kukutana naye" 


Maneno ya Jabir yalimfanya shangazi anyankue Cheni ile na kusema.


"Hii ni ya Paulina"


Unahisi nini kitatokea?


SECRET LOVE SEHEMU YA 07


TULIPOISHIA: "Hii utampa mtoto endapo utakapomsimulia kuhusu jamaa mpumbavu mpumbavu uliyewahi kukutana naye" 


Maneno ya Jabir yalimfanya shangazi anyankue Cheni ile na kusema.


"Hii ni ya Esta"


SONGA NAYO.


"Mama...." Paulina aliita kwa mshangao huku Ulimwengu akiwa anacheka.


"Sasa mama ndo nini sasa unafanya" Ulimwengu alimhoji.


"Mwaya Jabir . Tabu ameshaolewa hii ni ya Paulina ambaye hajaolewa" shangazi aliongea tena bila aibu. Ndipo Ulimwengu alimshika Jabir begani na kumwambia.


"Muelewe mama yetu. Anahisi wewe huna mtu anatamani uwe mkwe"


Maneno ya Ulimwengu yalimchekesha Jabir na kusema.


"Mama nampenda Paulina vilevile na Tabu. Ila hii zawadi siyo ya Tabu wala Paulina. Hii ni kwa ajili ya mtoto atakayezaliwa"


"Aaaah" shangazi alijibu kinyonge na kunikabidhisha. 


Ndipo Jabir aliondoka na hakurudi tena.


Majira ya usiku tulikuwa tumekaa mimi na Paulina huku tukipiga story.


"Wewe na Jabir damu zenu zimeendana" Paulina aliniambia bila kinyongo.


"Nisamehe Paulina"


"Usiombe msamaha ila mama anastahili kukuomba msamaha maana ujinga aloufanya sijavutika nao"


"Sasa kwanini alifanya vile"


"Mama alitamani niolewe na Jabir"


"Jabir anampenzi"


"Acha utani"


"Kweli, kwasababu kuondoka kwake ni dharura kutoka kwa mpenzi wake"


"Kisicho na bahati hakiliki"


Tukiwa tunazidi kupiga stori, alikuja shangazi na kuniuliza.


"Ile Cheni iko wapi?"


"Mama..." Paulina alimuita kwa mshangao.


"Funga mdomo... Na wewe harakisha weka hapa"


Nilianza kujisachi ndipo niliiona na kumkabidhisha.


"Mama unafanya kitu gani"

Ulimwengu muda huo alifika na kumhoji.


"Kwani nafanya nini" shangazi alimjibu huku akificha akihisi huwenda Ulimwengu hajaona.


"Nimeona. Leta ulichokificha"


"Nini kwani"


"Cheni umeficha"


Ndipo shangazi aliitoa kwa aibu na kunirushia.


"Hii siyo haki unayomfanyia marehemu kaka yako. Wewe ndiye umebaki kama baba yake sasa unamtesa binti yake kiasi hiki unazani kaka yako huko aliko anaamani na wewe" maneno ya Ulimwengu yalimkasilikisha shangazi na kumfanya aanze kuropoka kwa hasira.


"Hana amani na mimi kwanini? Kama aliwahi kumpenda Tabu kwanini alimterekeza na kutaka kumuua" maneno ya shangazi yaliniingia kichwani tayari kuvuruga ubongo wangu na hapo ndipo nilianza kuamini huwenda kuna siri kubwa mama aliyonificha ndomaana hanichukulii kama mtoto wa kumzaa.


"Eeee wifi umefika mbali" mama aliongea baada ya kutoka jikoni.


"Naomba kusikia tena" niliongea huku nikinyanyuka kutoka kwenye mkeka.


"Kusikia nini na wewe?" Shangazi alinihoji.


"Wallah leo Kama hamjaniambia ukweli naenda kujinyonga" niliongea huku nikiwa nimemaanisha.


"We mkosi unaongea kuhusu nini" mama alipaza sauti akiamini huwenda ntatulia kama kawaida yangu bila kujua kwa wakati huo nilikuwa nimechafukwa.


"Kwanini naitwa Tabu? Kwanini pindi nifikapo kwenye matatizo hata yawe makubwa kiasi gani huwezi kunitetea kama mwanao" nilimhoji huku machozi yakiwa yananitiririka.


"We Tabu"


"Utanipa jibu au"


"Umepatwa na nini?"


"Unataka kujua"


Haraka nilikifuata kisu kilichoko chini, Na kukushika kwa ajili ya kujichoma, usiriazi wangu uliwashangaza watu wote maana kawaida hali yangu ni upole na kukubali chochote niambiwacho. Walianza kupiga kelele wakiniomba nisijichome ila kwa wakati huo nilikuwa nimedhamiria. Kama Bahati alitokea baba yangu mlezi nyuma yangu na kunishika mkono kisha Tukaanza kupambana huku mimi nikiwa napiga kelele kama chizi. Ulimwengu alisogea na kunishika ndipo walifanikiwa kunyang'anya kisu kile.


"Mniache nife tu"


"Hapana mwanangu" mama aliongea huku akilia.


"Mara hii umelia kwa ajili yangu?" Nilimhoji.


"Siyo hivyo binti yangu embu tulia ntakwambia ukweli"


"Mama umeyaharibu maisha yangu" niliongea kwa huzuni na kushuka chini. 


"Naomba mjomba kaa na mwanao mueleze ukweli bila kumficha ili muweze kuganga yajayo" Ulimwengu alitoa pendekezo hilo na kutoka zake, baada ya muda tuliingia ndani na mama kwa ajili ya mazungumzo.


"Chanzo cha yote ni hii Cheni" aliongea Paulina baada ya kubaki na mama yake.


"Usiniuzi na wewe"


"Umeyataka Wewe"


Upande wetu mama alianza kuniomba msamaha.


"Katika maisha yangu niliamini endapo sitakuthamini hata baba yako huko aliko hatapata amani... Mwanangu wewe ni wa pekee na uliniachia laana mpaka leo hii naamini ujio wako ni mkosi katika maisha yangu, marehemu baba yako enzi hizo alinipenda ila sikuwahi kumpenda hata kidogo, kilichotokea alinitendea unyama ambao hata siku unakuja kuniambia kuhusu Alex kukubaka niliona umerithi kwangu.  Baba yako alinibaka siku ya harusi yangu"


"Harusi yako na yeye au"


"Nilikuwa nafunga ndoa na mtu mwingine nimpendaye, enzi zetu mwanamke akijulikana amebakwa ilikuwa ni laana na hatoolewa kamwe. Nilihangaika na haikuchukua muda baba yako alifariki"


"Alikuwa amejua kuhusu mimi"


"Bado"


"Kwanini sasa hunipendi"


"Kwasababu nilijaribu kukutoa bado upo tumboni ikashindikana, nyumbani kwetu walinifukuza nikaja kutesekea hapa kwa wifi yangu. Wallah nilitumia dawa za kila aina ili kuweza kukutoa ilishindikana. Nilipata mateso kwenye nyumba hii Mungu ndiye anajua"


"Kwanini jina langu ni Tabu?"


"Nilikuzaa kwa Tabu sana"


"Usingeniita Tabu ungeniita basi mbwa huwenda tabu hizi nisingezipitia"


"Usilie naimani unaenda kufanikiwa, hata nilipokuzaa nilijaribu kukutupa ila moyo ulikataa, nilijaribu kutaka kukunywesha sumu ila mwenyezi Mungu alikuwa anamipango juu yako. Ndipo niliona nikupange jina la Tabu licha mama yangu alitamani nikuite Mariam,  Kiukweli nimeteseka na wewe mpaka nimempata huyu baba yako nilikuwa mwenye mateso maana sikupata mtoto tena na niliambiwa na doctor wewe ndiye chanzo "


"Mimi chanzo kivipi? Chanzo ni zile dawa ulizokuwa unatumia kwa ajili ya kunitoa tumboni"


"Nisamehe Binti yangu... Maneno yangu makali ndio yalikufanya unapata matatizo"


"Kwa mfano leo hii jina langu Mariam ningepitia Haya?"


Unahisi nini kitatokea?

SECRET LOVE SEHEMU YA 08


TULIPOISHIA: "Mimi chanzo kivipi? Chanzo ni zile dawa ulizokuwa unatumia kwa ajili ya kunitoa tumboni"


"Nisamehe Binti yangu... Maneno yangu makali ndio yalikufanya unapata matatizo"


"Kwa mfano leo hii jina langu Mariam ningepitia Haya?"


SONGA NAYO.


"Ndo maana nimetanguliza samahani"


"Usinifanyie haya tena. Mama mimi nakupenda"


"Najuwa hilo mwanangu, naimani mambo yote yatakuwa sawa"


Tuliombana msamaha mwishowe tukasameheana.


"Pole jamani" Paolina alinipa pole baada ya kunikuta kibarazani.


"Nimeshapoa hivi umeiona ile Cheni"


"Ifiche mama asiione" alinikabidhi kiroho safi bila kinyongo chochote.


"Mtu huwa anapitia mateso mpaka anahisi huwenda alizaliwa kimakosa"


"Nikweli ila nafuraha kuona kaka Ulimwengu ametoa onyo kwa yeyote atakaye kurudisha kwa Alex"


Siku zilisonga hatimaye binamu yangu Ulimwengu alirudi mjini kwa ajili ya kuendeleza majukumu yake ya kila siku, mama yangu alirudi nyumbani na kuniacha kwa shangazi akidai Alex akija nisimsikilize.


"Tumboni kwasasa uko sawa?" Paolina alinihoji baada ya kunikuta nikitafuna embe mbichi.


"Niko sawa ila nasikia hamu ya embe dodo"


"Wow hapo naona baby tumboni yuko sawa"


Tukiwa tunaendeleza story, alikuja Alex Kama kawaida yake kusimama juu ya watu bila salamu.


"Tabu ingia ndani" Paolina aliniambia huku akiwa amekunja uso.


"Unaenda wapi, twende nyumbani" Alex aliniambia baada ya kuniona nanyanyuka.


Nilipoona kizaazaa kinaanza nilikimbia kuelelea kunako mlango ili kujificha, ajabu kabla sijaingia shangazi alitoka na kusimama mlangoni huku akinizuia nisiingie.


"Shangazi anakuja kunichukuwa nipishe niingie" niliongea kwa hofu huku nikiwa nahangaika kugeuka nyuma aliko Alex ambaye kwa muda huo alikuwa anarushiana maneno na Paolina.


"Wende wapi?" Swali la shangazi lilizidi kunishangaza.


"Mama mpishe aingie" Paolina alinitetea.


"Aingie wapi na mumewe amekuja kumfuata"


Hapo ndipo Alex alitabasamu na kuanza kunifuata. Kiukweli kitendo cha kuchukiwa na familia yangu kiliniumiza na kuona sina kwa kukimbilia, ndipo Alex alinifikia na kunishika mkono kisha akamwambia shangazi.


"Nashukuru shangazi"


"Nitokee" shangazi alimjibu na kuingia Zake ndani.


Tulipofika nyumbani hakuna kilichoongelewa zaidi ya kipigo. Alinipiga kiasi kwamba nikapoteza fahamu.


Baada ya masaa manne kupita, nilirudisha fahamu na kuanza kuangaza huku na kule ila sikupata kumuona Alex. Taratibu nilijikongoja na kuelekea nyumbani kwa mama yangu.


"Kweli ndo akupige namna hii?" Mama aliongea kwa hasira baada ya kuiona hali yangu.


"Mama nisaidie"


"Sasa jamani mi ntafanya Nini?"


"Utafanya nini? Kwahiyo upo radhi kuniona nikiteseka namna hii?"


"Sasa wewe umeshaolewa, nije kukutoa kwenye ndoa huoni kama ntakuwa nakusababishia mateso binti yangu?"


"Kuna mateso zaidi ya haya niliyonayo?"


Haikuchukua muda Alex alifika. Kwa uzalendo wa baba yangu mlezi alimkalisha chini na kuanza kumshauri jinsi ya kuishi na mwanamke. Ndipo alinirudisha nyumbani na hakuweza kunipiga tena mpaka mimi mwenyewe nikashangaa.


"Twende sehemu" Paolina aliniambia baada ya kunikuta nimelala chini ya mwembe.


"Sehemu gani?" Nilimhoji.


"twende utajua"


Haraka nilivuta kanga na kuongoza naye nisikokujua. Moja kwa moja tulielekea mtoni na kuwakuta mabinti wenzetu wakifua huku wakipiga stori.


"Mbona sielewi" nilimhoji.


"We tulia kwanza"


Paolina alikunja dela yake na kuelekea waliko madada wale, haraka alimzaba kibao binti flani ambaye niliitambua sura yake baada ya kugeuka kumtazama Paolina.


"Esta....." Niliita kwa mshangao na kuwafanya wote kugeuka kuniangalia. Esta aliponiona alijawa na aibu huku akijifanya kufua. Paolina hakutaka kumpotezea alimshika dela na kuanza kumvuta akimleta niliko.


"Jamani utamuumiza" binti flani alitaka kumtetea ila Paolina alimnyamanzisha akisema.


"Kisicho kuhusu kisikuchukue muda, kama hautaki na wewe kuunganishwa funga bakuli yako"


Ndipo Paolina alimfikisha mbele yangu na kuniambia.


"Mpige mpaka pale hasira zako zitakapoisha" 


"Esta kwanini siku ile ulinifungia kwa Alex" nilimhoji huku nikiwa nimeanza kulia.


"Unamhoji kitu gani... chapa mshenzi huyu" Paolina alisema baada ya kuona ukimya wa Esta.


"Alex alikupa shiingapi ili uweze kuniharibia maisha yangu" nilizidi kumhoji ila hakuweza kunijibu zaidi ya kushusha macho kwa aibu. Paolina kwa kuwa alikuwa anaelewa vyema hali yangu alimvuta Esta na kuanza kumpiga makofi huku mimi nikiwa nimeduwaa baada ya kukumbuka tukio lile.

Paolina alimpiga kiasi kwamba Esta akaanza kuomba msamaha.


"Sema sasa kwanini ulimfungia mwenzio" Paolina alimhoji huku akipumua kwa hasira.


"Dada Tabu naomba nisamehe, ukweli ni kwamba.... Alex alinipa elfu 20 akaniambia nijifanye kuwa karibu yako. kiukweli najuta sana" Esta aliongea huku akilia.


"Kwasasa nina ujauzito, na.... Alex ananipiga sana, umefurahi kusikia?" Nilimhoji.


"Nisamehe jamani"


"Siku ile nilikuwa nahasira na wewe sana, ila kwasasa nilishakusamehe.. hii ni dunia na wala sikuombei yakukute yaliyonikuta" niliongea kwa huzuni na kuanza kuondoka zangu. Paolina hakuacha kumshughulikia alimpiga mpaka pale hasira zake zilipomuishia.


"Mbona uliniacha" Paolina alinihoji baada ya kunifikia.


"Sikutaka kuendelea kumuona"


"Nimemshughulikia Naimani ataadithia"


"Nashukuru kwa kunipigania"


"Tumboni vipi! Uko sawa kweli?"


Unahisi nini kitatokea?

Maoni 1

  1. Very nice story.
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.