Notification texts go here Contact Us Buy Now!

SECRET LOVE SEHEMU YA 02

SIMULIZI: SECRET LOVE
MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 02

TULIPOISHIA: Nilianza kupiga kelele huku nikimlalamikia Esta aje kunisaidia, ajabu ukimya uliokuwa nje ulinidhihirishia tosha Hakuna mtu aliyopo maeneo hayo.

SONGA NAYO!

"Estaaaaaaaaa" niliendelea kumlalamikia huku nikiomba Msaada hata kwa yeyote ambaye anaenisikia aje kunisaidia, ajabu Hakuna aliyejitokeza, ukija kuangalia nyumba za vijijini zilivyo unaweza kukuta nyumba moja mashaliki jilani yake manghalibi. Mkaka Yule ambaye jina lake nilikuwa silitambui, alitumia mbinu zake awezavyo mpaka akafanikiwa kunibaka. Nilibaki mwenye majonzi na Majuto hata nilipomuomba niondoke hakuniruhusu mpaka asubuhi. Njiani niligeuka Kama chizi na wala sikuona aibu maana nilikuwa nalia kwa uchungu, uso wangu ulikuwa umejaa ngeu huku macho yakiwa yamevimba kutokana na kulia kwa muda mrefu, hakili ilinituma kwenda kwa mama yangu ila nikaona ni Vyema kwenda kwa shangazi maana mama angeniua. Kichwani mwangu jina la Esta nililiandika kwa herufi Kubwa huku nikitamani kumuona kwa muda huo. Nilipofika nyumbani nilishangaa kukuta familia nzima imenisubiri kwa hamu mpaka mama yangu pamoja na baba yangu wakambo wakiwa wapo hapo, sikujali kitu chochote zaidi ya kuongeza kilio huku nikisogea walipo. Mama alinishangaa Sana na kunikimbilia.

Kama Dakika kadhaa, nilikalishwa katikati ya familia ili kueleza nini kimenisibu. Nililia kwa uchungu huku nikiwasimulia ilivyokuwa ila ajabu Hakuna hata mmoja aliyenielewa bali walidai ni tabia yangu na nirudi kwa mwanaume huyo.

"Mama hata wewe jamani" niliongea kwa uchungu.

"Staki kusikia chochote kutoka kwako. wewe ni mkosi katika maisha yangu, na sijui laana hii itaisha lini kwangu" aliongea mama kwa uchungu na kunifanya ninyanyuke bila kuongea chochote.

"Lakini mama, mbona Tabu Hana tabia mbaya" aliongea Paolina ambaye alionekana kuwa upande wangu.

"Tabia yake imejidhihirisha sasa, arudi kwa mumewe kwangu haishi" aliongea shangazi bila hofu na kuwafanya wote wanyanyuke na kunisindikiza nilikotoka. Niliendelea kulia kwa uchungu huku nikijiona nilizaliwa kimakosa au huwenda jina langu linatafsiri kubwa kwenye maisha yangu.

Walinifikisha kwa mwanaume Yule mwenye roho ya chato, ndipo walikaa kikao mpaka majira ya jioni. Mwanaume mwenyewe alikuwa hajulikani wapi anatokea wala familia yake ni ipi.

"Nisamehe Sana Tabu" aliongea Paolina huku akilia baada ya familia kuondoka na kuniacha kwa mwanaume huyo.

"Esta ameniua" niliongea kwa sauti ya chini mno. 

"Ntamkomesha, lazma nimfanye ajute kwa hili. ila mama yako amenishangaza sana ujue.... Eee! mama Kama mama ambaye dunia nzima inampa majina ya kifahari nani Kama mama leo hii nimepata kuona mama wa ajabu, au siyo mama yako? Hata Kulia au akutetee kweli? yeye si ndo amekulea na anajuwa tabia yako! Nimeshangaa anasema kabisa mbele ya watu eti umeyataka mwenyewe.... Dah Tabu pole Sana, Angalia mpaka shangazi yako alivyokugeuka kwani una nini wewe" maneno ya Paolina yalizidi kunitia huzuni na kushindwa kuongea chochote zaidi ya kusema. 

"Esta ameniua"

Paolina aliangua kilio na kuondoka haraka. Nilibaki chini ya mwembe huku nikijiuliza baada ya hapo nini kitafuata kwenye maisha yangu. 

Kutengwa na familia yangu mpaka mama yangu mazazi hicho ndicho kilizidi kunishangaza na kunipa moyo wa kuvumilia matokeo ya ndoa. Niliishi na mwanaume huyo jina lake Alex hata siku moja sikuwahi kumchekea wala kumpiga story ya aina yoyote.

Miezi miwili ilikatika nikiwa bado nipo kwenye ndoano na si ndoa. Kichapo ndicho kilikuwa chakula changu, Kama kawaida ya wanaume wa kijijini wakiwa ni walevi lazma wawe na kisirani kwa wake zao, nilihangaika kwenye ndoa kila siku asubuhi naamkia shamba, kurudi usiku wa manane.
Haikupita Miezi kadhaa nilikuwa tayari mjamzito. 

"Labda ningefanikiwa kumuona baba yangu huwenda yeye alikuwa ananipenda" niliongea huku nikilia na kumfanya Paulina ajiskie vibaya na kuzidi kunionea huruma. Mazingira ya nyumbani kwa shangazi niliyatamani na kuhisi kuna kitu nimekikosa.

"Usiseme hivo, yote ni changamoto ya maisha" aliongea Paolina. 

"Nimekumbuka story zako, nimekumbuka kuangalia TV"

"Vyote now tunaweza kufanya mbona"

"unaweza kufosi huzuni, ila furaha haifosiwi.. Jina langu ni Tabu ndio maana wanasema jina ni mtu mwenyewe"

"Tatizo hicho ki Alex kinawaza kupiga tu, siku moja ntakuja nimchambe"

"Ananipiga Sana, sijui ntaishi vipi na mimba hii... nawaza kutoroka sijui ntatorokea wapi"

"Pole jamani" Paolina alizidi kunipa pole licha Hakuwa na Msaada wowote. 

"Najifikiria kujinyonga nitoke duniani, nimechoka mateso haya" niliangua kilio na kumfanya Paulina asogee kunikumbatia huku akinitia moyo.

"Hapana Tabu, haupaswi kukata tamaa, unapaswa kuwa mwenye nguvu ili uyashinde majaribu. sasa ukianza kufikiri akuhusu kujinyonga nani atajifunza kupitia wewe? historia yako itakuwa mbaya mpaka milele, ila ukipambana kila mmoja atataka kujifunza kupitia wewe"

"Esta nishetani, afanye asirudi kwenye kijiji hichi"

"Masuala ya Esta achana nayo, wewe focus kufikiria kuhusu maisha yako na mwanao"

Muda huo alifika Alex akiwa ni mwenye hasira. Paolina alimtazama jicho mbaya huku mimi nikiwa nimeanza kutetemeka, Alex alisogea nilipo na kunizaba kibao, kitendo kilichomchukiza Paolina na kuanza kumfokea.

"Mwanaume mzima hujuielewi, kazi kumpiga mkeo hivi hujui kuwa ni mjamzito"

"Halafu wewe shika adabu yako" Alex alimwambia Paolina na kuanza kuniinua kwa fujo.

"Niache Ale, utaniua siku moja" niliongea kwa upole huku nikivuta kanga iliyonidondoka na kubaki kwenye andasketi.
Paolina alipomshika shemeji yake mkono ili kumzuwia asiniumize, alipigwa kibao na kudondokea pembeni.

"Twende nyumbani mshenzi wewe" alinipeleka kibabe huku Paolina akitusindikiza kwa macho.

"Yaani ningekuwa mwanaume huyu fala angenitambua leo" Paolina alijisemea kimoyo moyo.

"Niambie kule kwa shangazi yako ulikuwa umefuata nini hali ya kuwa nilishakukataza" aliongea Alex baada ya kufika nyumbani.

"Nisamehe" niliomba msamaha huku nikitetemeka kwa woga.

"Yule mshenzi kasema unamimba, ni kweli"

"Ni kweli"

"Pumbavu zako"

Baada ya kunitusi alitoka zake nje kwa ajili ya kuvuta sigara.

"Shkamoo kaka Alex" mtoto mdogo wa kiume alimtolea salamu baada ya kumfikia.

"Marahaba"

"Dada Tabu nimemkuta"

"Wa nini?"

"Nimetumwa kwake"

"Na nani"

"Mkaka flani hivi"

"Unasema? Yupi" hapo alinyanyuka kwenye kiti na kuchomoa macho kama mlusi aliyebananishwa.

"Mfupi ila simfahamu"

"Kakutuma nini"

"Eti nije kumwambia dada Tabu amkute chini ya mwembe"

Unahisi nini kitatokea!
Usikose mkasa huu

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.