MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 01
UTANGULIZI: kwa jina naitwa Tabu, nina umri wa miaka 18, naishi na mama yangu mzazi ambae kaolewa na mwanaume mwingine kutokana na sababu nisizozijuwa. Katika kijiji chetu nimesifika kwa upole na nidhamu licha kilichonishangaza ni kwamba, toka nianze kujielewa mpaka nimekuwa binti mkubwa ni neno dogo lenye herufu 5 tu! "mkosi" ambalo mama yangu mazazi alipenda kuniambia na sikujuwa linatokana na nini maana nilikuwa Sina tabia za wanaume na ukija kuangalia nimelelewa kwenye maadili ya kiislam. Neno hilo katika ubongo wangu lilitulia kiasi kwamba kiasi kwamba nikalichukulia Kama jina langu. Ukweli mama alinilea vizuri wala hakuwahi kuninyanyasa, sema ifikapo nikakosea kidogo, tusi lililokuwa likimtoka ni "we Mkosi" sikuwahi kutaka kujuwa sababu za yeye kuniita jina hilo Bali nilichukulia poa.
SONGA NAYO!
"Tabu mwanangu" aliniita mama huku tukiwa tunachambua maharage chini ya mti uliyopo karibu na nyumba yetu.
"Abee mama"
"Maisha ya hapa kijijini yanazidi kuwa Mabaya hata sijui lini juwa litaacha kuwaka"
"Unamaana gani"
"Baba yako kasema wende kwa shangazi yako ili tujisatiti kwa muda na mambo yakikaa sawa utarudi"
"Kwani shangazi mwenyewe si yupo hapa hapa kijijini, mi sioni umuhimu wa Mimi kwenda huko"
"Unasemaje we Mkosi" mama aliongea kwa jazba na kunifanya niwe mpole.
"Namaanisha Kama maisha magumu hapa, basi na kwa shangazi ni hivo hivo"
"Hapana! Shangazi yako yupo vizuri... Em kwanza... Kwanini hutaki kwenda kwenu? hujui kuwa Kule ndo kwenu? Unafikiri hapa utapata urithi? Kule ndo kwa Baba yako mzazi sijui unanielewa"
"Nimekuelewa" nilikubali kishingo upande, na sikupoteza muda maana ilikuwa tayari jioni, ndipo nilipanga nguo zangu na kuelekea kwa shangazi ambaye alikuwa anaishi mbali Kidogo na nyumbani kwetu. Nilipofika nilipokelewa na Paolina ambaye ni binti yake lika yangu Kisha tukaenda kuoga, baadaye tukawasha moto nje na kutulia huku tukipiga story.
"Tabu, wanaume wa siku hizi unajuwa wananishangaza sana" aliniambia Paolina huku akitabasamu kwa mbali Kama mwenye jambo zuri.
"Kwanini" nilimhoji kiroho safi.
"Basi nikatoka zangu shule, kukatiza hivi sijakutana na mpumbavu mmoja " maneno ya Paolina yalinifanya nitabasamu huku nikiwa nimejawa bashasha yakutaka kujuwa je! mwenzangu anasumbuliwa na dudu mapenzi au laa.
"Huyo fala akaanza kuniambia oh ametokea mjini anataka anioe yaani Tabu amenifanya Nicheke kwa sauti"
"Usitishike kisa kakwambia mtoka mjini, hujui huko mjini nimuokota makopo au laa... Maana wanaume siyo wa kuamini kabisa, ukija kuangalia wewe umepata nafasi ya kusomeshwa usiichezee ndugu yangu"
"Yaani hicho ndo nakupendea! Ndo maana nilikuwa nimekumiss"
Tuliachia kicheko kwa pamoja na muda huo shangazi alifika Akiwa na mfuko mkononi.
"Shkamoo shangazi" nilitoa salamu huku nikiwa nimenyanyuka.
"Marhaba mtoto mpotevu" alinijibu huku akionekana kufurahiya ujio wangu.
"Mama! Tabu atakaa hapa mpaka pale mvua itakaponyesha" aliongea Paolina na kuiondoa tabasamu ya shangazi.
"Sijakuelewa" shangazi alihoji kwa usiriazi na kunifanya niingilie Mada.
" shangazi. Mama kasema Nije kuishi hapa mpaka pale mvua itakapoanza kunyesha, kwasababu Hali ya nyumbani siyo nzuri, na mazao yote yameungua kutokana na jua kuwa kali msimu huu"
"Aaah sawa" shangazi alijibu kiroho mbaya na kuelekea ndani huku Akiwa amekunja uso. Kama Dakika mbili mume wa shangazi alifika na kutusalimia kwa shangwe, baada ya kusikia nimehamia kwa muda alizidisha furaha na kuniambia atanichinjia jogoo.
Siku iliyofuata asubuhi na Mapema, tulijiandaa na kuelekea mtoni kuchota maji, tukiwa tupo njiani tulikutana na wanaume wawili waliyotuzidi umri wakaanza kutuita kwa matamanio.
"Achana nao, wanaume wa huku wanatamaa sana" aliongea Paolina.
"Duh! Wakaka wakubwa hawajielewi"
"Ndo walivyo wakiona mgeni, jicho limewatoka kwasababu yako"
"Wananipata wapi sasa, kwanza Kaka Ulimwengu anarejea lini" nilimhoji.
"Sijajua ila alisema akirudi kijijini ataniletea bonge la zawadi"
"Kweli binamu yangu ameanza kufanikiwa huko"
"Olewa naye" alinitania, tukaangua kicheko kwa pamoja huku tukizidi kupiga story. Baada ya muda tulitoka mtoni tukiwa na maji ndipo tulishangaa kuwakuta makaka wale wamesimama tulipowaacha.
"Usishangae wametusubiri sisi" aliongea Paolina.
"Dawa yao nikukaa kimya"
Tulipowafikia walianza kutuita, ndipo mmoja alisogea tulipo na kutuzuwia tusipite.
"We kaka vipi" aliongea Paolina kwa hasira.
"Acha zako Paolina, roho mbaya haijengi... Em muache rafiki yako tuongee"
"Hivi nyie mnamjuwa huyu ni Nani kwangu"
"Si ndo tunataka tumjuwe, em dada yake, yule jamaa anaomba namba yako"
Niligeuka kumtazama aliyenyooshewa kidole ndipo niliamua kupita na kuendelea na safari yangu.
Baada ya siku kadhaa makaka wale walianza kunisumbua mpaka ikawa destuli yao, kila nikikatiza kona hii nakutana nao, nikienda sokoni nawaona, ila hata siku moja sikuwahi kutoa muda wangu ili kuongea nao. Kwa kuwa Mara nyingi nyumbani nilipenda kubaki mwenyewe maana Paolina alikuwa anasoma kidato cha tano, nilipata rafiki jilani tukawa tunatembeleana. Urafiki ulinoga kiasi kwamba nikamuamini mpaka nguo tukawa tunavaliana.
"Naona Sina jipya tena" aliongea Paolina baada ya kufika nyumbani.
"Kwasababu ya Esta? " nilimhoji.
"Eeee"
"Wala siwezi kukutenga kisa yeye, ni rafiki yangu wewe ukiwa haupo"
"Jitetee"
Siku zilisonga, Na mvua haikunyesha licha nilitamani mvua inyeshe nirudi nyumbani kwa mama yangu, ukija kuangalia kwa shangazi nilikuwa Kama mtumwa maana kazi nyingi nilikuwa nafanya Mimi kwasababu sisomi.
"Naomba nisindikize kwa kaka yangu nimesikia ni mgonjwa" aliniambia Esta baada ya kunikuta nimetulia nyumbani, Na kwa kuwa kila kazi nilikuwa nimemaliza, sikuwa na budi kumsindikiza. Tulifika tukakaribishwa ndani, kisha tukaanza kuangalia TV. Ilipofika majira ya jioni nilimuomba Esta tuondoke ila akaniambia tungoje wifi yake anaandaa msosi.
"Jamani ngojeni namalizia kupika" aliongea wifi yake Esta na kunipa tumaini ya kusubiri. Kama nusu saa chakula kilitengwa tukala na kumaliza.
"Em tuondoke shangazi yangu mkali nahisi we mwenyewe unamfahamu" nilimwambia Esta ambaye alizidi kuleta mapya.
"Kaka kasema tusubiri atupatie pesa"
"Pesa? Za nini sasa? "
"Si unajuwa juzi kavuna mpunga wa kutosha"
"Ndo atupatie pesa? "
"Ee"
"Sasa Mimi nahusika vipi hapo?"
"Kaka yangu anaroho Nzuri Sana, hawezi kunipatia pesa peke yangu"
"Mmmmhh sawa"
"Usigune"
"Hapana, tatizo shangazi yangu mkali halafu toka nizaliwe sijawahi kwenda sehemu kuanzia asubuhi mpaka muda huu"
"Heee! Tabu na wewe, situmekuja saa tano"
"Kwani saa tano siyo asubuhi"
Tuliendelea kuongea mpaka majira ya saa moja usiku na hapo nilikuwa tayari nimenyanyuka kwa ajili ya kuondoka. Muda huo aliingia kaka yake Esta na kutuomba radhi kwa kuchelewa, ndipo alimuita Esta nje ili kumkabidhi pesa. Hapo Tumaini ya kwenda nyumbani ilirudi, nikakaa na kumsubiri arudi.
Kama Dakika Mbili aliingia kijana ambaye sikutaka kumtazama maana nilikuwa bize naangalia mchezo kwenye TV. Gafla nilishangaa kuona mtu kwa nje anauvuta mlango na kuubamiza kwa nguvu. Hapo ndipo nilipata muda wa kumtazama aliyeingia, nilishangaa kumuona mkaka Yule anaependa kunifuatilia na kudai ananipenda. Mapigo ya moyo wangu yalinienda mbio huku nikiwa namtazama kwa mshangao.
"Mambo mrembo" alinisalimia baada ya kunifikia na kunishika kidevu kwa matamanio. Haraka niliurusha mkono wake kwa hasira na kuufuata mlango ambao ulionekana kufungwa kwa nje baada ya Mimi kuanza kuuvuta kwa nguvu. Kijasho chembamba kilianza kunitoka, Haraka nikageuka kumtazama mkaka Yule nikashangaa kumuona kabaki kwenye bukta tu.
Nilianza kupiga kelele huku nikimlalamikia Esta aje kunisaidia. ajabu ukimya uliokuwa nje ulinidhihilishia tosha Hakuna mtu aliyopo maeneo hayo.
Unahisi nini kitatokea!
Usikose mkasa huu.