NITAOLEWA LINI?
MTUNZI: McLAURIAN
WASAP: 0768276551
NITAOLEWA LINI? PART: 01.
"Nitaolewa lini? , mbona hata mdogo wangu ameolewa na kuniacha nyumbani nikiwa mpweke?. Ee Mungu wangu naomba unisaidie kupata mchumba handsome, mrefu kidogo, mweusi au maji ya kunde na mwisho awe na pesa. Nakuomba sana mpaka magoti yangu sasa yamechubuka" Nilimuomba muumba wetu huku nikiwa na uchungu mkubwa sana.
Kwa majina naitwa Debora ni miaka 4 sasa tangu mdogo wangu aitwaye Jacline aolewe na mpaka sasa amefanikiwa kupata watoto 2.
Hali hii inanifanya nisikie vibaya kabisa hasa kwa majirani ambao wananizunguka. Kibaya zaidi siku moja nikiwa nyumbani, kwa mbali nilimsikia mama akiwa anaongea na baba juu ya suala langu la kutoolewa. Ama kweli nilizidi kujisikia vibaya kabisa mpaka nikajikuta machozi yananitoka mithili ya mtu aliyechapwa viboko.
Baada ya hali hiyo, nilianza kusali sana bila kukoma huku nikiwa namatumaini makubwa sana ya kupata mme ambaye nilikuwa nampenda. Mda uliendelea kusonga mbele huku miaka nayo ikazidi kukimbia kama mshale na hatimaye nikafikisha miaka 28 bila kuolewa.
Ama kweli sio kama najisifia lakini nilikuwa mzuri na mpaka sasa mi mzuri kweli hasa shingo langu ambalo limepanda kama twiga, kifuani balbu zilikuwa saa sita kabisa ambazo hazikuihutaji brauzia kabisa.
Urefu wangu ni wastani, rangi yangu maji ya kunde, lips zangu nzuri kweli, sauti yangu nyororo na laini kama kinanda, shape namba 8 tena sio la kichina, na tumbo langu jembamba huku katikati likiwa na kitovu ambacho kikekaa vizuri kabisa.
Ama kweli kama ni kuumba basi nimeumbwa kwelikweli bila kusahau macho yangu makubwa na meupe kweli yaliyoambatana na pua ndefu kama ya mzungu huku uso wangu ukiwa hauna hata chunusi moja.
Uzuri wangu huu ulinifanya niwe napiga picha nyingi sana ambazo nilikuwa nazipost FB na INSTA lakini badae nikafura account ya FB kwani walikuwa wananisumbua sana hasa wahindi na waarabu ambao mara nyingi walikuwa wananipigia video call kupitia messenger.
Mbali na uzuri wangu na miaka yangu yote niliyokuwa nayo, sikuwahi kulala na mwanume yeyote wala kuhisi joto lake kabisa hivo nilikuwa bado b****....ra huku nikiwa nimepanga kumpatia mwanaume wangu mtarajiwa zawadi hiyo.ya uaminifu.
Kwa upande wa dini, nimelelewa maadili mazuri ya dini ya Kikristo huku nikiwa pia na malezi mazuri kutoka kwa wazazi wangu yaani baba na mama.
Sasa nikawa nashangaa kuona rafiki zangu ambao wanasura za kawaida sana kulinganisha na mimi wanaolewa tena na wamaume wazuri wenye kumcha Mungu, handsome, warefu na pia wenye pesa. Kilichoniuma zaidi ni rafiki yangu aitwaye Marry ambaye alikuwa anadanga kabisa maeneo ya tabata na Sinza mpaka karibia watu wengi wakawa wanalifahamu hilo lakini alituacha midomo.wazi mara baada ya kuolewa na mtoto wa mchungaji.
Niliumia sana maana hata wavulana wengi walikuwa kama wananiogopa kutokana na muonekano wangu na mwishowe nikawa natongozwa na wazee lakini sikuwa tayari hata kidogo maana nilijua wanaenda kunitoa usichana wangu halafu badae wataniacha jambo ambalo sikuwa tayari kabisa.
Niliendelea kuomba kila siku ndipo niliposikia kuwa kuna mchungaji anaombea mabinti ambao hawajaolewa kupata wachumba na badae kuolewa.
Nilijiandaa mpaka kanisa hilo na kama bahati siku hiyo mchungaji wa kanisa hilo aligusia hapohapo jambo ambalo lilinipa matumaini na furaha moyoni mwangu.
Nikiwa naendelea kupata matumaini, mchungaji huyo alisema,
"Mabinti wote ambao hamjaolewa na mnataka kuolewa jongeeni mbele...wahi...wahi...kuna miujiza inataka kuendeka mda huu kila mtu anapata mmwe leo hii"
Baada ya kusema hivo, asee nilishangaa kuona hata wadada niliodhani wameolewa tayari nao wanakimbizana kwenda mbele sehemu aliyokuwepo mchungaji.
Nami nilijiunga kwenye msafara huo huku nikiwa naona aibu kwa mbali.
"Mnaotaka wanaume mmeisha..? kama umebaki njoo..njoo" Mchungaji alirudia mara ya pili ndipo hata wamama waliokuwa na miaka kama 40 hivi nao wakanyanyuka jambo lililoacha vicheko miongoni mwa waumini.
Hali hiyo ilinifanya nijione mdogo na mwenye matumaini makubwa ya kupata mme kwani nilikuwa mzuri kuliko wote waliokuwa mbele hapo.
Baada ya kutukusanya, alitwambia tufumbe macho tuombe..., tulifanya hivo kwa mda wa dakika kama 5 hivi. Badae tulifumbua macho kisha mchungaji akaanza kusema?
"Wanaume kutoka kusini, mashariki mletwe na upepo wa kisulisuli, muwaoe hawa mabinti zetu. Jehova bwana wa mabwana ruhusu upepo wa kisulisuli ulete wanaume wakutosha waweze kuoa warembo wetu ....sema ameeeeni...sema ameeeeni."
Tulibaki mbele tumesubiri wanaume waje kwa miujiza hiyo lakini mwishowe hakutokea mwanaume hata mmoja ndipo tuliporudi kwenye nafasi zetu huku tukiwa tunachekana wenyewe kwa wenyewe.
Mchungaji aliendelea kutupa moyo kuwa kila aliyejingea mbele hataodlndoka bila mchumba. Kauli hiyo ilinipa matumaini makubwa sana hasa uzuri wangu na tabia yangu huku nikiwa bado sijawahi onjwa na mtu yeyote yule.
Mambo yalizidi kuwa mambo. Baada ya ibada takatifu tulitoka nje kisha nikasimama simama kwa mda wa dakika kama 10 hivi huku nikisubiri maajabu ya kupata mchunba ambaye atakuja kunioa.
Kama maajabu hivi alitokea kijana mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina la SEBO kisha akaniambia,
"Mambo dada"
"Nzuri za wewe" Nilimjibu.
"Mi naitwa SEBO we waitwa nani?"
"Naitwa Debora" Nilimjibu huku nikiwa nimeinamisha kichwa chini kwa aibu .
"Ohh..kumbe, sasa nina ombi moja sijui utanikubalia?"
"Mhhh...ombi gani hilo? " Niliguna kisha nikamuuliza.
"Dada yaani kila siku nakuonaga ila nashindwaga kukwambia lakini kiukweli unautesa moyo wangu mpaka nadhani utakuwa umeanza kutoboka kwa ajili yako."
"Mhh..kivipi mbona sijakuelewa? " nilimuuliza.
"Yaani nakupenda sana tena sana ili uwe mke wangu unizalie watoto wazuri kama wewe"
"Mhhh..." Niliguna tu huku nikiwa natafuna kucha .
"Mbona waguna naomba unikubali please ana please"
"Subiri nijifikiri vizuri nitakupa jibu " Nilimwambia kisha tukabadilishana namba.
Baada ya kubadilishana mamba, nilipanda daladala nakuelekea nyumbani kwetu maeneo ya Boko huku nikiwa na furaha ya aina yake kwa miujiza ya kumpata mchumba japo sikuwa nimempa jibu..
Nilipofika nyumbani, nilioga kwanza kisha nikaingia chumbani mwangu ndipo niliposhika simu yangu kwa furaha zote kisha nikamcheki Sebo na bahati nzuri alikuwa online.
"Mme wangu ombi lako limekubaliwa ila naomba usinitende maana nimejitoa kila kitu kwako ili niolewe na wewe" Nilimjibu kwa njia ya whatsap.
"Ohh...nashukuru sana mke wangu yaani nina furaha kama yote siju kama jioni unaweza kuja nyumbani kwangu maeneo ya changanyikeni.."
"Mhh...kwa leo haitowezekana labda siku nyingine nitakwambia" Nilimjibu
"Kwanini jamani?"
"Leo kuna wageni wanakuja nyumbani " Nilimjibu.
"Ok, "
Safari yangu ya mahusiano ilianzia hapo yaani mda ulivyokuwa unazidi kwenda nikatamani kuolewa hata ndani ya wiki moja maana nilikuwa nimechoka kukaa nyumbani kwakweli.
Mambo yalizidi kunoga kwelikweli mpaka tukaanza kutumiana picha, kupigiana video call huku SMS zikiwa hazina idadi kwa siku.
Funga fungua hatimaye wekend ilifika yaani jumamosi ndipo nilipomwambia mama kuwa naenda kusuka ilihali nilikuwa naenda kwa Sebo.
Mama aliniruhusu kwani nilikuwa mtu mzima kisha safari ya Boko kuelekea changanyikeni ikaanza. Baada ya mda wadakika kama 30 hivi, nilifika barabarani ambapo nilimkuta Sebo amenisubiria kisha tukapanda bajaji mpaka nyumbani kwake.
Baada ya kungia ndani, nilikuta kitanda kimetandikwa vizuri kwa shuka jeupe sana ambalo lilikuwa limechorwa maua ya kopa yaani ( LOVE).
Pembeni kulikuwa na kasofa ka mtu mmoja lakiki palikuwa na nguo ndipo nilopokaa kwenye kitanda na Sebo akakaa pembeni mwangu.
Tulianza kupiga stori taaratibu ndipo alipoanza kunishikashika kwenye maziwa yangu na mapaja yangu jambo ambalo sikulipenda kabisa kwani mpango wangu ni mpaka niolewe ndo niguswe.
"Usinishike tafadhari..nakuheshimu sana na utanishika sana mpaka utanichoka utakaponioa" Nilimwambia huku nikiwa namshika mikono yake.
"Hee! sasa kama ni hivo umekuja nyumbani kwangu kufanta nini?" Aliongea kisha akaenda kufunga mlango.
JE ILIKUWAJE?
