- Unga - 3 ¾ vikombe
- Maji dafudafu (warm) - ½ kikombe
- Maziwa dafudafu - ½ kikombe
- Yai - 1
- Siagi (butter) - 1/3 kikombe
- Sukari - 1/3 kikombe
- Hamira - 2 vijiko vya chai
- Siagi (nyengine) - ¼ kikombe
- Chumvi - 1 kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika donuts
Changanya maji dafudafu (warm) pamoja na maziwa katika bakuli.
Tia sukari ukoroge mpaka iyayuke.
Weka hamira, acha kiasi dakika 10 mpaka ibadilike kuwa kama povu.
Piga yai utie humo, pamoja na siagi ya 1/3 na chumvi.
Tia unga kidogo kidogo katika mchanganyiko wa hamira.
Kanda kisha acha uumuke kiasi dakika 45 uwe size ya mara mbili yake.
Gawa unga katika vidonge, kisha acha vidonge viuumuke tena kidogo.
Sukuma kisha pakaza juu yake siagi katika ile ya ¼ kikombe.
Kunja katika shepu ya croissants kwa kukata katika shepu ya ncha tatu (triangle) kisha zungusha unga kuanzia upande ulio mpana kuelekea upande mdogo.
Panga katika treya ya kuchomea (bake). Nyunyizia ufuta kisha acha zi
