Ni nani mhalifu mwenye akili zaidi katika historia? Kwa nini?
Mtu ambaye yuko kwenye picha ni James Verone.
Unaweza kuwa tayari unajua juu ya huyu mtu kwa sababu tukio hili lilitokea nyuma sana mnamo 2011.
James Verone aliondoka nyumbani kwake Gastonia, North Carolina, tarehe 9 Juni 2011 na kufanya kitu ambacho nadhani hutoweza fikiria.
Alikwenda katika benki iliyo karibu na akampatia karani barua ambayo alisema,
"Huu ni wizi wa benki. Tafadhali nipe dola moja. "
James alitoa barua hii na aliketi na kungojea polisi.
Kabla ya hii, alituma barua kwenye gazeti moja la eneo hilo, Ambayo iliwapa taarifa kwamba anaenda kuiba bank haraka sana na kwamba alikuwa mtu mwenye akili timamu, lakini sio mwenye mwili mzuri.
Kisha alilialika Gazeti la Gaston kumuhoji katika Jela ya Kaunti ya Gaston ambapo alikuwa amewekwa maabusu kwa kosa la wizi.
Hata hvyo $ 1 ilikuwa ndogo sana kwa wafungua mashtaka dhidi yake kuendelea na kesi hiyo.
Hata hvyo inageuka kuwa, James alikuwa anafanya kazi Coca-Cola na alipopoteza kazi aliyokuwa ameshikilia kwa karibu miongo 2, na kusababisha kupoteza bima ya afya Ambayo alikuwa akiitegemea kujitibia.
Alikuwa akiugua uvimbe kwenye kifua chake, viungo vya arthritiki na mguu wa gammy na aliamua kuwa njia pekee ambayo angefanya maisha bora ni kupitia huduma ya afya ya serikali ambayo angelipata akiwa jela.
Labda sio mhalifu mwenye akili zaidi katika historia, lakini James Verone ni mtu mwenye akili timamu.
Asante kwa kusoma
