Notification texts go here Contact Us Buy Now!

KISA KIDOGO CHA MKWAWA AMBACHO HUKUFUNDISHWA SHULENI.

KISA KIDOGO CHA MKWAWA AMBACHO HUKUFUNDISHWA SHULENI.

Wajerumani walipovamia Tanganyika walipigana vita na ngoma nyingi sana, ila katika maisha na hadi leo katika kumbukumbu za maisha yao, Mtu anaitwa Mkwawa watamkumbuka milele. Ngoja nikupe kisa kimoja kifupi tu ambacho hukuwahi kufundishwa shuleni.

July 1891 kamanda wa kijerumani Von Zelewiski anaongoza kampeni ya kijeshi kumpindua Mkwawa, kiongozi wa kabila wa wahehe.  Zelewiski alikuwa na jeshi la watu 320 wakiwamo waofisa pamoja na wabeba mizigo humohumo. Mkwawa alikuwa ni kiongozi mjanja na mwenye mbinu za ajabu, uchawi ukiwemo. Alikuwa na majasusi makabila yote ya jirani, alipata taarifa nyeti za maadui na kuzifanyia kazi kwa maslahi ya watu wake. 

Jeshi lile dogo la watu 320 tu bila shaka walimuona Mkwawa ni mtu wa mchezo mchezo, huwezi kumvamia mtu kama Mkwawa na watu 320 tu. Mkwawa alipata taarifa ya ujio ule mapema sana, akatuma jeshi lake la watu 3000 kuwadhibiti askari wa Zelewiski kabla hawajafika popote. Jeshi la Ujerumani walikuwa na sihala kali za kisasa, ila jeshi la Mkwawa ni silaha za jadi zenye sumu kali sana, licha ya kuwa silaha za jadi, ila walikuwa majasiri zaidi.

Agosti 17 1891 vita kali ikapiganwa eneo la Lugalo. Mkwawa alitoa maelekezo yafuatayo kwa wanajeshi wake. “Kila mwanajeshi aje na korodani za adui atayemuua, atakaye kuja na chache nitamuua”... basi unaambiwa wanajeshi wale walienda wakaua jeshi lote la Zelewiski, hadi Zelewiski mwenyewe walikamata wakaua. Ilifikia wakati wanajeshi wa Mkwawa wakaanza kudundaba kugombania korodani, mana ukienda na chache kwa mkuu basi hali yako itakuwa mbaya.. Huyu ndio Mkwawa, kuna muda kiongozi lazima utoe maagizo na maamuzi magumu kuwatia watu wako ujasiri.

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.