KISA CHA KWELI
Mfahamu kijana huyu aliyeonekana akisoma Qur'an jela,jina lake ni Nafis Yaqoub ni kijana wa Thailand ambaye aliingia Malaysia kinyume na sheria kwa lengo la kufanya kazi.
Siku moja alitoka alipokuwa amejificha kwa kuogopa kukamatwa na kwenda kutafuta chakula cha kununua.
Bahati mbaya akakutana na police wa Malaysia na kumuuliza utambulisho wake,police alimchukua na kumpekeka chumba cha mahojiano na kugundua kuwa alikuwa Mthailand na alikuja Malaysia kinyume na sheria hivo wakamuweka jela wakisubir utaratibu wa kumrudisha kwao.
Jela kulikuwa na joto sana hivo ikamlazimu avue shati na kusubiri chakula,wakati abasubiri chakula akawa anasoma Qur'an sauti yake ilikuwa nzuri Sanaa.
Moja ya Askari akamrekodi na kuichapisha kwenye mitandao ya kijamii ( internet) kijana nasif akapata umaarufu Sana.
Hii ilimpelekea Nasif Yaqoub police wamuachie kutoka gerezani walipokuwa wanamshikilia na kuchaguliwa kuwa Imam katika msikiti huko Malaysia,akashinda zawad mbalimbali na fedha za kutosha akawa anatoa kwa wakimbizi BURMA.
Na leo ni miongoni mwa maimamu maarufu sana Malaysia.
SUBHAN ALLAH
" Tusikate tamaa na rehma zake Allah,kila jambo linalokufika lina sababu zake"
Namuomba Allah atujaalie sote tuwe waumini wa KWELI,Ameen
