Notification texts go here Contact Us Buy Now!

NIMECHANWA CHANWA USO, MIMBA IMETOKA NA MWANAUME HANIELEWI!

NIMECHANWA CHANWA USO, MIMBA IMETOKA NA MWANAUME HANIELEWI!

Habari Kaka naomba ushauri wako, mimi ni Mama wa watoto wawili, siulizii kuhusu mume wangu kwani hana tatizo, anahudumia familia na kila kitu napata. Lakini nina rafiki yangu mmoja ambaye nilisoma naye chuo tukaja kupotezana, hakuwahi kuwa mpenzi wangu ila tulikua karibu tu. Mwaka jana mwanzoni nilikutana na huyo rafiki yangu, yeye hajaoa, tuliongea mengi akawa ananitaniatania na tukabadilisha mawazo ya hapa na pale kisha tukajikuta tu tunabadilishana namba za simu na tunakua marafiki.

Tulianza kuwa tunachart mara kwa mara kwenye simu, tunapigiana video call na vitu kama hivyo mpaka nikamzoea sana, tulikua tunaonge akila kitu, ananiambia kuhusu mpenzi wake na mimi namuambia kuhusu mume wangu, yaani nilizoeana naye na tulikua tunachara vitu vingi kuliko hata mume wangu. Sababu ya kuja kwako ni hivi, wiki iliyopita nilimpigia sana simu rafiki yangu, akawa hapokei, kila nikimpigia Video call anakata na nikituma meseji hapigi simu.

Kweli niliumia, nilimtafuta mpaka dada yak eili kujua tatizo ni nini lakini aliniambia kuwa hakuna shida yuko sawa na simu zake anapokea. Niliumia sana nikaanza kumtumia meseji za kumlaumu kwanini hapokei simu zangu, kwanini hajibu meseji zangu lakini karibu wiki nzima hakupokea simu zangu na mwisho aliniblock. Baada ya kuniblock nilipigiwa simu na dada mmoja alijitambulisha kuwa yeye ni mchumba wa huyo rafiki yangu na ana mimba yake.

Kusema kweli Kaka nilichanganyikiwa, roho iliniuma sana kwani nafahamu huyo Kaka ana mwanamke wake mwingine, alishanitambulisha na sijui ni kwanini anamsaliti. Kwa hasira niliamua kumpigia simu mwanamke wake na kumuambia kuwa jamaa yake ana mwanamke mwingine na ana mimba yake. Yule dada alipaniki akampigia jamaa ndiyo naye akanipigia simu kunitukana akiniambia kuwa naingilia mambo yake na hataki kuonana na mimi.

Nilijaribu kumuomba msamaha lakini hakuhangaika na mimi, aliniblock na kusema nisimtafute tena kwani nimemharibia mambo yake. Hali hiyo iliniuma sana, nikashindwa kuvumilia nilimtafuta Dada yake naye hakutaka kunisikiliza, nilipoona kuwa hanisikilizi nilimuaga mume wangu kuwa naenda kumsalimia mgonjwa kwetu ili niende kumuomba msamaha rafiki yangu kwani nilijua kuwa nimemkosea kwa kuingilia mapenzi yake.

Yeye anaishi Mwanza hivyo kwakua na kwetu ni shinyanga nilienda mpaka Mwanza, nilikua napajua kwake, nilifika Mwanza usiku kabisa, nikachukua chumba na asubuhi nikaenda ili kumuona, lakini Kaka nilipofika sikumkuta, nikamkuta huyo mwanamke wake, niligonga mlango na kujitambulisha kuwa mimi ni Dada wa mwanaume, kwakua ni rafiki na tulishakua kama ndugu basi alinikaribisha na kuniambia kuwa jamaa katoka kidogo kwani ilikua si siku ya kazi ni jumapili iliyopita.

Nikakaa pale kwa wasiwasi na kwsauti tu niligundua kuwa huyo ndiyo yule mwanamke ambaye alinitukana kwenye simu akidhani kuwa mimi ni mpenzi wake. Kwa bahati hakunitambua kwnai wakati ananitukana mimi sikuongea sana. Baad aya kama nusu saa hivi mwanaume alikuja, kwanza alishangaa kunuiona pale, mimi nilijaribu kumuelezea kuwa sikwenda pale kwa sahari lakini alianza kunitukana na kunifukuza, nilimuomba sana msamaha nikimuambia kuwa mimi sikuja kwa ubaya kwani nilienda tu kumuona na kuomba msamaha ila hakusikia.

Basi wakati tunabishana ndiyo yule Dada aligundua kuwa ni mimi, alianza naye kunitukana na kutaka kunipiga lakini mwanaume alimzuia, basi hapo ndipo niliona kuwa kumbe bado ananijali nikasema sitoki mpaka nisamehewe. Nilimpandisha mwanamke hasira, alichukua stuli akanipiga nayo mongonei, aliniumiza sana na mimi kwa hasira nilinyanyuka na kuanza kumpiga, yeye kamwili kake ni kadogo hivyo nilimpiga sana, mwanaume alijaribu kunishika lakini nilimzidi nguvu.

Kuona vile yule dada alikimbilia chumbani, mwanaume aliniambia niondoke lakini mimi nilikazania kuwa anisamehe wkanza kwnai sikupanga kumharibia. Wakati tunabishana na mwanaume basi yule dada alikuja na viwembe, alianza kunichana chana na viwembe usoni, mgongoni na kila sehemu, damu zilianza kutoka, kuona vile nilianza kukimbia kutoka nnje, lakini dada alinishika nguo niliyokua nimevaa, akanichania kwani nilivaa dera kwakua nilikua na ujauzito wa miezi minne.

Wakati nakimbia kumkwepa na yeye kanishika nilitelkeza na kudondoka wkenye ngazi kwani nyumba yao ipo kwa juu, nilizimia palepale, wakanichukua na kunipeleka hospitalini wakaniacha huko. Nililazwa jumapili ile mpaka jana ndiyo nimeruhusiwa kutoka tena kwa kulazimishia kwani mimba ilitoka na mume wangu alikua ananitafuta sana kwani alishajua kuwa sijaenda nyumbani. Mbaya zaidi nikuwa yule dada wakati napelekwa hospitalini alinipipiga picha na kuzitumakwenye group moja la Whatsapp akaandika kuwa kanifumania na mume wake.

Hilo group wifi yangu yupo, akaona picha zangu na kumuambia mume wangu. Kaka mume wangu aliziona na kuniuliza nilimuambia ni kweli niko mwanza lakini sijafumaniwa kwakua nilikua sichepuki ila mwanaume hataki kunielewa kabisa.kaka kila mtu anajua nimefumaniwa lakini si kweli, mimi nilienda tu kuomba msamaha kwa rafiki yangu na sina mahusiano naye, ni rafiki tu ambaye tulizoea kuchart naye hajawahi kunivunija heshima yaani nashindwa hata chakufanya, nisaidie Kaka nimuambieje mume wangu ili aniamini kuwa nampenda sijamsaliti?

Lakini Kaka uso wangu umeharibika kwa kuchanjwa, nina bandeji nyingi usoni, mimba imetoka na sasa hivi nina maumivu makali sana, yaani nipo Mwanza nawaza kwenda nyumbani lakini nashindwa, sijui nifanya nini, natamani hata uongee na mume wangu umuambie ukweli, mimi Kaka sijachapuka naweza kushika hata Bibilia, huyu kaka ni rafiki yangu tu na nilienda kuomba msamaha baada ya kuona kuwa nimemhartibia mahusiano yake, alikua hapokei simu zangu Kaka sasa mimi ningefanya nini, nisaidie kaka yangu?
MWISHO

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.