Notification texts go here Contact Us Buy Now!

Naomba ushauri wako kuhusu kaka yangu

Naomba ushauri wako kuhusu kaka yangu

Naomba ushauri wako, mimi ni Binti wa miaka 27, sijaolewa na kwasasa nipo kwenye mahusiano ya kawaida na yanaenda vizuri. Sikuja kukuomba ushauri kuhusu mimi bali ninaomba ushauri kuhusiana na Kaka yangu. Yeye ameoa, lakini kaka yangu ni wale watu wa kuchagua kazi, amesoma mpaka ana Master ila shida nikuwa kila kazi anayoipata basi anasema si kazi ya hadhi yake. Mke wake yeye ni mwalimu tu lakini ndiyo anahudumia kila kitu, wana watoto wanne, mke ndiyo anasomesha, chakula na wakati mwingine anampa Kaka pesa ya matumizi.
Hali hii ni ya muda mrefu, karibu miaka saba sasa Kaka hafanyi kazi lakini mambo yanaenda. Mimi naishi kwa Kaka yangu, sijapata kazi bado ingawa namimi nimemaliza chuo, si kama nachagua ila sijapata. Wifi yangu ni mtu wa dhaarau sana, nahisi hatupendi ila hana namna ya kutufukuza kwani nyumba ni ya Kaka. Mimi kw2angu si shida kwani simjali, najua siku moja ataondoka tu kama alivyokuja na kuacha kila kitu.
Shida iko hivi, kuna kipindi wifi alibadilika sana, akawa ni mtu wa kutokujali, hamheshimu kaka, anaweza kutoka na kucnelewa kurudi bila kujali kuwa kamuacha mume ndani. Nilichunguza nikagundua kuwa an amwanaume anatembea naye, tena ni mbaba mtu mzima ana nafamilia yake. Yeye ndiyo anamhudumia kila kitu, analipia watoto ada, anamjengea na sasa hivi kamnunulia Gari ambalo Kaka ndiyo analiendesha ila nimechunguza, ingawa kadanganya kuwa Gari ni la mkopo lakini si kweli. Baada ya kukusanya ushahidi wote nilimfuata na kumuambia kuwa nimejua kuwa ana mwanaume mwingine.

Kwakua sikutaka kuingilia ndoa ya watu nilimpa muda kuachana na huyo mwanaume au nimuambie Kaka. Baada ya kuniambia alinijibu dharau. “Kaka yako atakua ni mjinga kama akidhani kuwa hizo pesa naokota, kwa mshaara gani wa walimu nasomesha watoto watatu shule ada mtoto mmoja kwa mwaka milioni mbili, mnakuja hapa mnakula na kunya bure wewe na Kaka yako, sijavaa, sijaume kweli kwa mshaara wa laki nne wa mwalimu muembie tu akiniacha mtakua mmenipunguzia kero!”

Tuligombana sana,  lakini sikumuambia Kaka, niliamua kukaa kimya, ila shida imekuja, baada ya kujua kuwa nimejua wifi kaanza chokochoko anataka niondoke, nyumba ni ya Kaka, alijenga kabla ya kumuoa. Mimi niliongea na Kaka yangu basi nikamuambia kuwa siondoke, sasa baada ya kuona kuwa nimegoma kuondoka na Kaka yangu amekua upande wangu aliwapeleka watoto wake wote Boarding bila hata kutushiriksiha sisi mimi na Kaka. Baada ya kuwapeleka tu kaacha kutoa matumizi hapa nyumbani.
Amemfukuza binti wa kazi na anadai kuwa mimi nakaa tu sina kazi hivyo nifanye kazi za ndani. Haachi pesa ya chakula, yaani anachelewa kurudi akirudi kashakula mtaani. Baada ya kuona hivyo Kaka amenibadilikia ananiambia kuwa niondoke kweli niliamua kuondoka na kurudi nyumbani. Lakini baada ya kufika na kuongea na mama aliniambia nirudi atakua akinitumia pesa ya kula kwani nikimuacha Kaka yangu anaweza kuuliwa na mke wake, mke wake ndiyo anamharibu Kaka kiasi kwamba hatamani kufanya kazi.

Nilirudi Mama akaanza kuzunguka na kila sehemu anaambiw ahivyo hivyo kuwa ili Kaka milango ifunguke basi ni lazima amuache mke wake kwakua yeye ndiyo anamzibia Riziki, anatembea na nyota yake. Tumeonga na kaka mpaka tumechoka, bado anamng’ang’ania mke wake, sasa sijamuambia mtu yoyote kuhusu umalaya wa wifi yangu, lakini natamanhi kumuambia Kaka ilia fanye maamuzi sahihi, je niko sawa kumuambia, nakusoma san ahivyo sitaki kuwa kama wal emawifi ambao wanaingilia dnoa za wtau, naomba nisaidie nifanye nini ili kumuokoa Kaka yangu?

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.