Mimi ni Binti wa miaka 30, sijaolewa ila nina mchumba ambaye naishi kwao, ni mwaka wan ne sasa anishi kwa mchumba wangu, wazazi wake wananipenda lakini yeye hanitaki kabisa. Yeye ndiyo alinitambulisha kwao, lakini kuna kipindi alipata mwanamke mwingine akaniacha, mama yake alisema kuwa hamtaki huyo mwanamke kwani si mtu wa kabila lake lakini hakumsikia, Mama yake na ndugu zake wote walisema kuwa wananitambua mimi tu si huyo mwanamke mwingine.
Lakini mwanaume alinikataa na kusema kama naolewa na Mama yake au ndugu zake basi nibaki. Kwakua nilikua nampenda nilibaki nikiamini kuwa atabdilika na kusikiliza radhi za wazazi wake. Nilipata m,oyo kuna kipindi alikua akija nyumbani tunashirikiana naye kimwili mpaka nimepata watoto wawili lakini bado yeye alikua akisisitiza kuwa hanitaki ingaw awatoto anahudumia.
Sababu ya kuja kwako kaka nikua nimechoka, hataki kumuacha huyo mwanamke mwingine na nimesikia kashafunga ndoa ya bomani na huyo mwanamke kwani wazazi wake walikataa kabisa ndoa ya kanisani. Kaka nimekaa nimevumilia na mwaname haelekei, mimi sina kazi, kuna kipindi nilipata kazi TANESCO mkoa mwingine lakini Mama mkwe aliniambia nibaki watanilewa kwani nikiondoka hapo nyumbani basi ndiyo hatanioa tena.
Kila siku mwanaume tumekua tukigombana ananiambia mimi ndiyo namgombanisha na ndugu zake lakini kaka mimi sio hivyo, nampenda na kwakua ndugu zake wananipenda mimi basi anagombana nao. Juzi wifi yangu mmoja alikuja na mwanume, huyo Kaka ni Malaya na annatembea na rafiki yangu, alishajitambulisha mpaka kwao, mimi nilimuambia tu kwa roho nzuri lakini maneno yakazuka kuwa nina mdomo, namchulia na mambo kibao.
Kaka huwezi amini familia nzima imenigeuka, mpaka Mama mkwe ananiambia kuwa mimi nina mikosi namgombanisha na watoto wake kama vipi niondoke. Kaka nimechanganyikiwa, kweli nimechoka lakini mwanaume bado nampenda, wamenipotezea muda wangu mwingi sana mpaka sijui hata nifanye nini? Nawaza hata niwashitaki, nasikia mwanaume huko mjini ana nyumba sijui kajenga na huyo hawara wake kaka si naweza kwenda kudai hata na mimi wanangu wapate haki zao, yaani nimechanganyikiwa hata sijui nifanye nini?
