Kama mwanaume ndiyo anakutongoza, narudia kama mwanaume ndiyo anakutongoza, naona sauti haitoshi kama mwanaume ndiyo anakutongoza. Wewe na yeye ni dini tofauti, narudia kwani nafundisha kama nafundisha wale watoto wa darasa la kwanza, kama ndiyo anakutongoza, ukakuta nyie ni dini tofauti, ukamuambia ungemkubalia lakini nyie ni dini tofauti. Ukaongea kwa msimamo kabisa kuwa wewe huwezi kubadilisha dini akakuambia “Mimi kwetu dini sio ishu kabisa!” Akakutajia Kaka yake, sijui Shangazi yake sijui marehemu babu yake alikua dini kama yakwako kwahiyo si ishu.
Anakutajia watu ambao hata huwajui, akakuambia yeye yupo tayari na labd a kufunga ndoa ya serikali au kubadilisha dini. Kumbuka hapa hata hajatembea nawewe, basi dada yangu ni uongo! Uongo! Uongo! Iko hivi, wanaume wanabadilisha dini lakini si kiharaka namna hiyo, wanabadilisha wakishapenda mpaka basi, lakini hapo hhara rangi ya sijui nini haijui yupo tayari sijui kwenda kanisani au kwenda msikitini na kanzu kuvaa na jina anajichagulia kwakua tu sijui nani wao alikua muisalamu au muikristo dada yangu ni ile wanasema ukiona manyoya tu… Najua una hamu sana ya kuolewa lakini jua mwanaume akitaka kufanya mapenzi na wewe atakubali chochote kile, hata ukimuambia huaki awe anaongea na Mama yake atamblock mbele yako na hutaamini!
Angalau mshaingia kwenye mahusiano labda viuno vimemchanganya kachanganyikiwa! Yaani ukikubali hapa ni sawa na utongozwe na mpare halafu umuambie akupe ATM Card yake, yaani anaweza kukupa lakini jua kuwa haitakua na kitu! Au ni sawa na umkute mwanamke wa kichaga anasachi mifuko yako akudanganye kuwa alikua anaangalia kama unachepuka alikua anangalia kama umebeba Condom na wewe uamini kuwa kweli alikua anasachi mifuko kuangalia Condom! Hana muda huo!
