USO WA FEDHA | FACE OF MONEY.
USO WA FEDHA # 34 [SWAHILI].
MTUNZI: Sunday JoaquimContact: 0658593797
Nilitafakari bila majibu, woga ulitanda moyoni mwangu, niliamua kuingoja hiyo kesho ili maswali yangu yasiyo na majibu,niliona kesho inachelewa,saa zilikuwa haziendi,japokuwa niliogopa maana Hata Kakwezi alianza kama mzaha mwisho aliniponza na aijamuona hata kumsikia mpaka leo.
Kesho yake niliamka mapema kama kawaida ya wazee wote wa kichaga,kulala sana ni dalili ya mtu mvivu, niliona majirani wakija kunisalimu,nilipenda utaratibu huo wa kutakiana hali kila asubuhi na jioni kukusanyika kuota moto pamoja huku watu wakitaniana, wakisimuliana visa mbali mbali.
Ilipotimu saa mbili asubuhi nilienda kuoga na kujiandaa,kujiweka tayari kwa safari ya saa nne,niliweka macho yangu kwenye saa,ilipofika saa nne kamili asubuhi, ile gari iliyokuja jana ilifika nyumbani kwangu, alishuka ofisa yule yule, tukasalimiana " mmmh naona unaenda na muda!" Aliongea yule ofisa "
"Sijawahi kuchelewa kwenye maisha yangu" "safi sana nadhani wewe ni mtu sahihi.... haya twende" tuliondoka mpaka Moshi mjini,tulipita njia ya KCMC tukaingia kwenye geti moja,palikuwa na nyumba moja kubwa,mazingira yalikuwa tulivu sana yaliyozungukwa na miti mirefu na kufanya kuwa na hali ya hewa nzuri sana "usishuke mpaka nitakapo kwambia haya ni mazingira nyeti sana, haruhusiwi mtu yeyote asiyehusika kukanyaga maziwa haya" "sawa" niliitikia na kubaki ndani ya gari.
Baada ya kama dakika tano alitoka ndani ya ile nyumba kijana mmoja "samahani unaitwa ndani" nilishuka kwenye gari nakuelekea mlango wa ile nyumba yule kijana akiwa amenitangulia mbele, alifungua mlango tukaingia ndani, ndipo niligundua haikuwa nyumba bali ni ofisi baada ya kuona meza za ofisi na mafaili mengi na baadhi ya wafanyakazi wakiendelea na kazi.
Alikuja yule ofisa aliyenifuata nyumbani, akaniambia "jaza fomu hizi lakini usidanganye chochote na kama kuna sehemu huelewi uliza" "sawa" nilianza kujaza,nilifika mahala nikakuta swali ulishawahi kutuhumiwa au kupandishwa kizimbani kwa uhalifu? Daah jasho lilinitoka mpaka yule ofisa aligundua kwamba sikuwa katika hali ya kawaida " vipi bwana mbona jasho linakutoka wakati hapa ndani viyoyozi kama ulaya" nilishindwa kuongea, nilimwonyesha tu lile swali kwa kutumia peni " haaaa haaaaa we USO WA FEDHA nani asiyekujua? ..... taarifa zako tunazo nimekwambia usidanganye" niliitikia kwa kutikisa kichwa, nikaendelea kujaza zile fomu.
Nilipomaliza nilipigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole,kisha nikaambiwa "ingia hapo" nilionyeshwa mlango na yule ofisa, nikifungua mlango nikamuona mtu aliyeonekana ni bosi,nilitazamana naye uso kwa uso,akanionyesha ishara kwa mkono kunitaka niketi kwenye kiti, niliketi " Uso wa FEDHA karibu sana" "ahsante" niliitikia kwa woga " sasa bwana nimekuita hapa... kuna jambo zito sana nataka utusaidie" moyo wangu ulipiga "paaaa" kiasi yule bosi alielewa kuwa niliogopa "usiogope upo sehemu salama sana.... tunataka kupata taarifa za sehemu unayoishi kwa matukio yote... sisi tunakupa hiyo kazi ni ajira wala hakuna ubabaishaji.... sitegemei kuwa utakataa" " mh! Mheshimiwa mbona jambo zito sana... kwasababu mimi sijamaliza hata mwezi... isitoshe mimi ni mgeni mazingira haya sikuwepo zaidi ya miaka thelathini sasa leo habari nitazipataje?" " sawa labda nikutoe woga sisi tunajuwa wewe unajulikana na wengi.... pia una uwezo mkubwa wa kuchanganyika na watu.... matajiri wote wa hapa mjini wanajua kwamba upo hapa Moshi lazima watataka kukutumia tu kwa hiyo haitakuwa vigumu kwako kupata taarifa".
Macho yalinitoka, nilijiuliza ina maana watu wanaifuatilia kiasi hiki? sikuwa na namna nikikubaliana na hiyo kazi "safi sana... sasa pokea kitambulisho na barua ya ajira" nilizidi kushangaa imekuwaje mimi kuingia kwenye kitengo nyeti namna hii? Nilipokea kitambulisho na ile barua kisha yule bosi alimwita ofisa yule aliynifuata nyumbani "lete vitendea kazi" yule ofisa bila kuchelewa alileta mkebe mdogo mweusi pamoja na bahasha kubwa ya khaki akanikabidhi, bosi aliinuka toka kwenye kiti chake akazunguka nilipoketi mimi,akachukuwa ule mkebe akaufungua alafu akauinamisha kunionyesha kilichokuwemo ndani ...........ENDELEA NA SEHEMU YA 35 YA SIMULIZI HII YA USO WA FEDHA.
FACE OF MONEY #34 [ENGLISH VERSION].
I thought without answers, fear fell in my heart, I decided to wait for that tomorrow so that my questions without answers, I saw that tomorrow is late, the time was not going, though I was afraid because even when he started as a joke at the end he served me and hasn't even heard him until today.The next day I woke up early as usual for all chaga people, sleeping too is a sign of lazy man, I saw neighbors coming to greet me, I loved the procedure to cooperate every morning and evening gathered to dream fire together while people call each other away.
At pm, I went to take a bath and prepare, getting ready for a-hour journey, I kept my eyes on the hour, when it reached am, the car that came yesterday came down to my house, and went down the same officer, and said " hmm i see you going with time!" Spoke to the officer "
" I have never been late in my life " " very clean I think you are the right person.... okay let's go " we went out to smoke in the city, we passed through the way of CMC and entered into a single gate, there was one big house, the environment was so cool surrounded by tall trees and To make a good weather "don't go down until I tell you that this is a very sensitive environment, no one is allowed to step on this milk ok" I responded and remained inside the car.
After five minutes he went out inside the house one boy "sorry you are called inside" I went down in the car and heading to the door of the house when the boy was ahead of me, he opened the door and we went in, then I realized it wasn't the house but the office after seeing the office tables and Too many files and some employees continue to work.
Came to the officer who followed me at home, and said to me " fill these forms but don't lie to anything and if there is a place you don't understand ask " " OK " I started filling, I came to the place and found the question you have ever accused or raised in the court for crime? Daah sweat came from me until the officer realized that I was not in normal condition " how is my sweat coming out when inside air air like Europe " I was unable to speak, I just showed him the question using pen " haaaa haaaaa we face money who doesn't know..... Information..... Yours we have told you not to lie " I responded by shaking my head, and I kept filling out the forms.
When I finished taking a picture and taken a fingers, then I was told to " enter there " I was shown the door by the officer, when I opened the door and saw someone who seemed to be a boss, I looked at him with his face to face me to sit on the chair, I sat " the face of the money So much " " thank you " I responded with fear " Now Lord I have called you here... there is a very heavy thing I want you to help " my heart beat " AAAA " less that boss understood that I was afraid " don't fear you are in a very safe place.... we want to get information of where you live For all events... we give you that job is employment and no transfer.... I don't expect that you will deny it " " MH! Honorable, why is it so heavy... because I have not finished even a month... countless I am new this environment I was not there more than thirty years now today how will I get the news?" " okay maybe I should fear you, we know you are known by many.... you also have Great ability to get confused with people.... all the rich in the city know that you are here in moshi they must want to send you only so it won't be difficult for you to get information ".
My eyes came out, I asked myself does it mean that people follow this amount? I had no way agree with that "very clean... now receive id and employment letter" I kept wondering how did I get into this sensitive unit like this? I received the id and the letter then the boss called the officer who followed me at home "bring some work" the officer without delay he brought a small black cup with a big envelope and handed over me, the boss rose from his seat and sat down and opened it. Showing me what's inside.......CONTINUE TO READ PART 35 FACE OF MONEY NARRATIVE.
