USO WA FEDHA | FACE OF MONEY.
USO WA FEDHA # 32 [SWAHILI].
MTUNZI: Sunday JoaquimContact: 0658 593 797
Asubuhi na mapema tuliamka na kujiandaa, Babuu alitupeleka mpaka kituo cha Mabasi wakati huo Mabasi ya kwenda Moshi yalikuwa yanaegesha Kisutu,tulipofika tulipata tiketi mbili za pamoja,tulipakia mizigo yetu na kupanda ndani ya gari,saa kumi na mbili kamili basi lilianza kuondoka,nilimtazama Babuu kupitia dirishani nilihisi kulengwa machozi,makosa niliyoyafanya maishani mwangu leo yananifukuza mjini, mji bado nautaka lakini nikibaki hatari ya kupoteza maisha ni kibwa mno,nilijizuia kudondosha machozi, Mama Jackie na yeye alinipungia mkono nijihisi kama vile mwisho wa maisha yangu umefika, nilijikaza kiume lakini nilishindwa nakujikuta nikilia ndani kwa ndani,Wendo alijaribu kunituliza, kwa kuwa kipya kinyemi nilimudu kunyamaza.
Tulipofika Ubungo, Basi lilipakia abiria wengine, lilijaa na kuondoka, sikufika mbali nililala usingizi fofofo, Wendo aliona asinisumbue aliamua kuangalia runinga iliyokuwa ndani ya Basi.
Tulipofika Mombo Wendo aliniamsha ili twende tukapate kifungua kinywa pamoja na huduma za maliwato,laiti ningekuwa peke yangu nisingeamka mpaka mwisho wa Basi "umelala sana" aliongea Wendo "mmmh yeah nimechoka sana" "yeah lazima maana uliyoyapitia mmmh " basi tushuke tukanywe chai" "khe! kwani hapa wapi?" "Mombo tumefika Mombo" sikuamini, tulishuka na kwenda kwenye chai,tulipomaliza tulianza tena safari kuelekea Moshi mjini.
Tulipofika Moshi nilikodi tax ikatupeleka kijijini Kibisho kwa bibi, nilipofika nilimwona bibi amezeeka sana alikuwa ameketi juani anaota jua,nilikimbia kwenda kumlaki,nilipomfikia karibu tu "Nasikia harufu ya mjukuu wangu Egon" aliongea bibi kwa sauti ya kutetemeka, nilistaajabu ajabu kubwa,maana miaka niliyo ondoka nikiwa mtoto na sasa nimerudi mtu mzima bibi anasema anasikia harufu yangu! Nilistaajabu sana.
Nilipiga magoti mbele ya bibi na kumshika mikono yake iliyokuwa ya baridi sana,nilihisi uchungu moyoni, nilimkumbuka mama "Babuu yuko wapi?" aliuliza bibi "yupo Dar es salaam anasimamia biashara zetu,bibi alinyamaza kidogo alafu " biashara zenu?" aliuliza " ndio biashara zetu " niliingiwa na wasiwasi moyoni maana uliza ile haikuwa ya kawaida.
Bibi alikuwa haoni tena, mama zetu mama yetu mdogo aliyekuwa akimtunza bibi aliniambia "bibi yako alikuwa akikutaja kila mara.... na tangu juzi alikuwa akisema anaona unakuja... tulikuwa tikicheka... nashangaa umekuja kweli" nilivuta pumzi ndefu nikamkumbatia bibi "sogea hapa" aliongea bibi huku akipapasa kutafuta kichwa changu,alininiinamisha kichwa akanitemea mate na kunininea maneno kwa kilugha ambayo sikuweza kuyaelewa lakini nilihisi ni baraka.
Alipomaliza kunibariki alimtuma mama mdogo aende ndani akachukuwe mkoba wake,mama mdogo alikwenda kuleta mkoba "huu mkoba una nyaraka zote za mali zenu hasa nyumba na mashamba, nakukabidhi.... mama yako aliniletea niwatunzie na sasa umeshakuwa mtu mzima naomba uutunze mji wetu..... nakupa na nyaraka za mali zangu pamoja na bunduki aliyoiacha babu yako uitunze.... mimi siku zangu za kuishi zimekwisha..... nilikuwa nakusubiri wewe tu..... ndipo niondoke nilipo ona unakuja..... nilifarijika sana.....acha uovu mche Mwenyezi Mungu...... nawe utabarikiwa shambani...... utabarikiwa nyumbani" aliongea bibi alafu alitulia.
Nilipokea zile nyaraka zote katika hali ya huzuni sana kwa kuwa nilikumbuka mbali sana,nilimkumbuka baba, nilimkumbuka mama,nilianza kububujikwa machozi,bibi aliniambia "usilie.... furahi...... kwasababu umeniona na nimekubariki.... kuanzia sasa.... utakuwa baba wa mjini huu" niliinama miguuni pa bibi nilimshika miguu nilimjibu "ahsante bibi kwa kunibariki.... asante kwa kutunza mali zetu,ahsante bibi kwa kunikabidhi mali zako na kuniweka msimamizi wa Boma nashukuru sana bibi yangu" niliamka na kugeuka ndipo nilimwona Wendo, muda wote wala sikuwa namkumbuka wala yule dereva tax, nililipa tax na kushusha mizigo.
Tuliingia ndani nikatayarishiwa chumba cha kulala na maji ya kuoga,nilioga na Wendo alioga,tukaketi kwa chakula,muda huo ilikuwa yapata saa kumi na mbili jioni, niliona watu majirani wakilikuja kunisalimu na kuniambia taratibu za mila na desturi zetu za Wachaga endapo mtu au mtoto aliyepotea akionekana tena lazima achinjwe mbuzi dume apakwe damu iliyotiririka toka kifuani mwa huyo mbuzi,kwa hiyo shughuli hiyo ilipangwa kufanywa siku iliyo fuata asubuhi sana.
Niliamka mapema wazee wa kimila walinipeleka katikati ya migomba,walinipa kisu ili nichome katikati ya kifua cha beberu, nilifanya hivyo,damu ilikingwa,nikapakwa kwenye paji la uso na iliyobaki walinipa niinywe,nilikunywa wazee walichukuwa bilauri ya mbege walikunywa alafu walinipulizia ile mbege kichwani alafu walitamka maneno kwa kichaga kama vile walikuwa wakitaja majina ya koo za mababu na kunionbea radhi,shughuli hiyo ilipoisha tulirudi nyumbani.
Ilikuwa sherehe kubwa sana iliyoanza kama mchezo,walifurahi kuonekana kwangu.
Ilipofika jioni vijana walikoka moto,vilipangwa viti kuzunguka moto,walimwita Wendo wakaomba utambulisho " huyu ni mke wangu.. baada ya kupata changamoto za mahusiano huyu ndiye aliyekuja kunifariji" nilijibu hivyo kwasababu kumleta mwanamke ambaye si mke kwenye Boma ya bibi ni makosa kimila,ghafla mzee mmoja aliuliza " mmefunga ndoa" "hapana bado ndio maana nimekuja naye huku" "anhaa sawa.... we mama sogea hapa" Wendo alisogea katikati karibu na ule moto, vililetwa kiuri (kinu kidogo) mwiko,na chungu akakabidhiwa Wendo " tunakukabidhi Boma uwe mama na mlezi wa wote kwenye ukoo huu" Wendo hakutakiwa kujibu chochote alipokea vile vitu kisha niliitwa mimi nikaambiwa nimshike Wendo mkono kisha tulifungwa kwa kitenge na kamba za mgomba mkono wangu wa kushoto na mkono wa kulia wa Wendo alafu walituwekea kuni chini kuni mbili zilizokuwa na moto " haya rukeni hapo... wote kwa pamoja huku mkitanguliza mguu wa kulia mbele" tulifanya kama tulivyoambiwa,ghafla kelele za shangwe zilisikika,kumbe ndio tumefungishwa ndoa kimila haaaa haaaaa ilikuwa burudani sana.
Baada ya watu kula nyama za mbuzi na kunywa mbege mzee mmoja alisimama na kuanza kuongea " karibu sana kijana wetu... hapa sasa ni nyumbani kwako.... sifa ya mwanaume kamili ni kulea familia na kukabiliana na matatizo... lakini kutokana na yaliyotokea najua hujui nini kiliendelea baada ya ninyi kutoroka kwa shangazi yenu... upelezi ulifanyika na baba yako mdogo alikutwa na hatia ....... ENDELEA KUSOMA SEHEMU YA 33 YA SIMULIZI HII IITWAYO USO WA FEDHA.
FACE OF MONEY #32 [ENGLISH VERSION].
In the morning and early we woke up and prepared, the father took us to the bus station at that time the smoke buses were yanaegesha in kisutu, when we arrived we got two together tickets, we loaded our luggage and climb into the car, twelve o'clock then it started leaving, I watched the babuu Through the window I felt tears, the mistake I made in my life today is driving me out of the city, I still want it but when I remained the risk of losing life is too hard, I stopped taking tears, my mother Jackie and she pushed me to feel like the end of my life has reached me, but I was defeated. I find myself crying inside inside, chronological tried to calm me, because I am new in a house I kept quiet.When we arrived at ubungo, then it loaded other passengers, it was full and left, I didn't get far I slept asleep,, chronological saw that he didn't bother me he decided to watch the tv that was inside the bus.
When we arrived at mombo, he woke me so that we can go and get breakfast together with services, if i were alone I wouldn't wake up until the end of the bus " you slept so much " he spoke chronological " hmm yeah I'm so tired " " yeah we must come down and get tea " ! Where is this?" " Mombo we arrived at mombo " I didn't believe, we went down and went to tea, when we finished we started the journey to moshi in the city.
When we arrived at moshi, I rent a taxi and took us to the village. When I arrived, I saw my wife very old, she was sitting in the sun dreaming, I ran away to meet him, when I reached him almost "I heard the smell of my grandson Zion" spoke grandmother in a loud voice, I was surprised because I was surprised. Leave when I was a child and now I am back old man. Grandmother says she is feeling my smell! I was so surprised
I kneel in front of the grandmother and held her hands that was very cold, I felt pain in my heart, I remembered the mother " where is the father?" she asked the wife " she is in dar es salaam managing our businesses, the wife kept quiet and then " your businesses?" asked " This is our business " I was worried in my heart because ask the one that wasn't normal.
The Grandmother was not seeing again, our mothers our little mother who was taking care of the grandmother said to me " your wife was always mentioning you.... and since the other day she was saying she sees you coming... we were tikicheka... I wonder you have come true " I pulled a long breath and hugged the grandmother " Sogea Here " she spoke grandmother while she was supposed to look for my head, she bowed my head and spit on me and pushed me words in a language that I couldn't understand but I felt a blessing.
When she finished blessing me, she sent a young mother to go inside and take her bag, the younger mother went to bring a bag " this bag has all documents of your property especially houses and lands, I deliver you.... your mother brought me to care for you and now you are already grown up, I ask you to take care of our city..... I give you the documents of my wealth and the gun that your grandfather left to protect.... me my days of living are over..... I was just waiting for you..... then I get away from where I see you coming..... I was very comforted..... stop evil and fear the Almighty God. ...... and you will be blessed in the farm...... you will be blessed at home " she spoke grandmother and then she was calm.
I received all those documents in a very sad situation since I remembered so far, I remembered dad, I remembered my mother, I began to tear tears, grandmother said to me " don't cry.... be happy...... because you saw me and I have blessed you.... from now on.... you will be father. From this city "I bowed down at my grandmother's feet. I held her feet and I answered him" thank you grandma for blessing me.... thank you for keeping our wealth, thank you grandmother for giving me your wealth and keeping me an admin of the veil. I woke up and turned away when I saw her doing, all the time. Neither did I remember nor that taxi driver, I paid tax and downloading.
We went in and prepared a bedroom with a shower water, I took a bath and the shower took a bath, and sat down for food, that time was about pm, I saw people neighbors coming to greet me and tell me our ways of our customs and traditions if someone was lost. And if he is seen again, a male goat shall be taken from the bosom of the goat, and the blood of the goat has been prepared to be done on the next morning.
I woke up early, the old elders took me to the middle of banana, they gave me a knife to burn me in the middle of the chest of goat, I did that, the blood was poured, I was painted on the forehead and the remaining gave me to drink, I drank the old men took the cup of the seed and then they said that it was a drink. Words in chaga as they were mentioning the names of their ancestors and showed me pleasure, when the activity ended we returned home.
It was a great celebration that started as a game, they were happy to appear to me.
When it was evening, the boys saved the fire, arranged seats around the fire, they called her chronological and asked for identity "this is my wife.. after getting challenges of relationships this is the one who came to comfort me" I answered that because bringing a woman who is not a wife to the wife's veil is wrong in tradition, Suddenly one old man asked " you have married marriage " " no it's still why I have come with him " " Anhaa ok.... you mama move here " chronological who moved in the middle near the fire, they were brought to the oven (a little bit) a taboo, and the pot was handed over " May the veil be the mother and guardian of all in this clan " chronological was not supposed to answer anything she received how things then I was called I was told to hold the chronological hand then we tied to the print and ropes of the banana my left hand and the right hand of the chronological and then they laid us down two wood that was And the fire "come out there... all together while putting your right foot forward" we did as we were told, suddenly the noise of joy was heard, so we have been tied to marriage in tradition haaaa haaaaa it was really fun.
After people eating goat s' meat and drinking the seed old one stood up and started talking " welcome to our boy... here is now your home.... the reputation of a perfect man is to raise a family and deal with problems... but due to what happened I know you don't know what happened after you escape from your aunt... Extension was done and your little father was found guilty.......CONTINUE TO READ PART 33 OF FACE OF MONEY NARRATIVE.
