Notification texts go here Contact Us Buy Now!

USO WA FEDHA | FACE OF MONEY #31

USO WA FEDHA | FACE OF MONEY.
USO WA FEDHA | FACE OF MONEY #31 - BONGOLIFE

USO WA FEDHA # 31 [SWAHILI].

MTUNZI:Sunday Joaquim
Contact: 0658 593 797

Tulitupwa chini kama maiti,niliumia kisogo na mikono,harufu kali ya dawa na damu za maiti wa ajali zilinifanya nijisikie vibaya sana, nilikuwa nimefumba macho ili kuzuga wahudumu wa chumba cha maiti wasigundue kama nilikuwa mzima,nilianza kwa kufumbua jicho moja la kulia niliona wahudumu kwa mbali wakihudumia wale maiti wengi waliosukumwa kule Segerea,niliinuka taratibu nikajificha nyuma ya makabati ya kuhifadhia maiti,niliona wahudumu hawana habari, nilinyata taratibu huku nikiwaruka maiti walilazwa chini licha ya kuwa na maumivu mwili mzima lakini nilitambua hatari iliyo kuwepo kama wahudumu wangeniona nimeamka, wangeita polisi ili niwekwe chini ya ulinzi wakati polisi walishaniambia nisiwawekee kiwingu.

Nilinyata taratibu nikafikia mlango mkubwa wa kutokea nje nilimpa Wendo ishara anifuate,aliniinuka taratibu toka katikati ya maiti akafuata njia yangu tukatoka nje,nilijikaza kutembea tulitembea na kupita geti kubwa la kuingilia hospitali,nilikodi tax mpaka nyumbani kwangu Tabata, nilikuwa nanuka sana nilifikia bafuni kuoga pamoja na Wendo,mwanamke ni mwanamke tu,Wendo alikwenda jikoni alichemsha maji akaja kunikanda ba kunisafisha vizuri majeraha yangu yote,George na Geoffrey waliponiona walilia sana kwasababu nilikuwa nimevimba usoni na hasa mdomoni, baada ya muda mfupi Babuu aliingia " kaka... kaka kuna kitu gani kinaendelea kwenye maisha yako ambacho mimi sijui? Kwa nini kunificha kaka?" Babuu aliongea kwa hasira sana, nilikuwa sina la kujibu, nilinyamaza na kushindwa kumwangalia usoni "kaka umekuwa JAMBAZI umesahau kuwa ndiyo chanzo cha kifo cha baba yetu? kaka kwa nini unafanya hivi? Tulikuwa masikini mbwa lakini Mungu katubariki sasa tuna vitu vyetu lakini bado huridhiki unataka kufa ili nibaki peke yangu????" Hapo niliinua uso kumwangalia Babuu nilimwona akitokwa machozi na uso wa huzuni sana nilijikuta nikilia kwa uchungu sana,nilikumbuka alivyouwawa baba,nilisikia uchungu mkali sana moyoni.

Niliinuka na kumkumbatia Babuu kwa muda wa kama dakika moja alafu nilimwambia " kuanzia sasa wewe utakuwa mlezi wangu mimi narudi kijijini.... nimefanya dhambi nyingi sana..... sihitaji kuwa na kitu tena... nakuachia kila kitu...tunza mali zitutunze,nakuamini sana nakutegemea sana.... maisha niliyoishi na mazingira yamenilazimisha kurudi kijijini.... kumbuka dunia hadaa ulimwengu shujaa... huwezi shindana na njia uliyojia.... punguza wanawake utaishi" nilimkumbatia tena Babuu tukalia sote kwa uchungu mkali mpaka Wendo alikuja kutukumbatia wote pamoja akalia pamoja nasi.

Babuu alisimama akaniangalia alishindwa kujizuia kuendelea kulia akiniangalia nilivyopigika aligeuka na kutoka nje,nilibaki na Wendo tu, nilipanda kitandani kulala, Wendo alikwenda jikoni kuandaa chakula kwasababu njaa ilikuwa inatuuma vibaya sana.

Babuu alirudi baada ya muda mfupi, alienda kumfuata mama Jackie,alipoingia ndani alikuja moja kwa moja chumbani alinikuta nimelala,aliona mishono ile ya viwembe mgongoni kwangu alishtuka na kupiga kelele za kuomboleza,nilishtuka toka usingizini nikageuka ghafla " nini.... nini tumevamiwa? "Babuu alikuja haraka,nilikuwa kwenye mawenge ya usingizi, fahamu zilipotulia nilimwona mama watoto mama Jackie, niliinuka haraka na kumkumbatia lakini aliponiona usoni alipoteza fahamu.

Ilianza kazi ya kumpepea, huduma ya kwanza na kumweka pahala penye hewa safi tulisaidiana na Babuu,baada ya kumpepea sana aliamka lakini alikuwa amechoka sana,nilijuwa bado anahitaji hewa safi, nilimshauri alale apumzike kwanza.

Babuu alienda kuongea na Wendo kule jikoni " samahani wewe ni nani? Unamfahamu vipi kaka yangu?" Wendo alitabasamu " tnaitwa Wendo" " okay.... okay vzr ulimfahamu vipi huyu bwana?" " kwenye kazi" " usiniambie mwanamke mzuri hivi na ww jambazi!!!" " hapana.... hapana kaka yangu... mimi nashiriki mashindano ya urembo" " mh! hainiingii akilini... ujambazi na urembo wapi na wapi?" " mimi waliniambia..." Wendo alipoinua uso alikutana na macho yangu alishindwa kuendelea "enhe.... enhe niambie nitakupa kiasi kikubwa cha fedha" Babuu hakugundua kuwa nilikuwa imesimama nyuma yake Wendo alishindwa kuendelea kuongea aliinamisha kichwa chini "calm on niambie usione aibu je ningekuomba....... niambie tafadhali" niliona kumsaidia Wendo na kumkata kauli Babuu ni kuingilia kati " akawambie nini?" Babuu alishtuka kwa kurusha mabega juu kidogo, alitoka nje bila kugeuka nyuma.

Nilimsogelea Wendo,alikuwa akitetemeka sana "usiogope mimi ndiye mwenye mali zote hizi upo salama sana" aliitikia kwa kutikisa kichwa "vzr.... sasa usithubutu kumwambia chochote huyu bwana.... tena usimsogele atakupitia sasa hivi utazaa mpaka wajukuu" nilimtisha kidogo ili Babuu asiharibu shughuli.

Nilijiuguza kama wiki moja pale nyumbani kwangu,ilikuwa ngumu kulala usingizi kwasababu chumbani nililala na mama Jackie,Wendo alilala chumba kingine, niliwaza kiwavi Babuu anaweza kuzamia chumbani kwa Wendo, ilinilazimu kuamka mara nne mpaka tano kwa usiku mmoja ili kuhakikisha Wendo yupo salama.

Baada ya wiki nijiandaa kurudi kijijini, mama Jackie ilimlazimu abaki jijini Dar es salaam, Wendo nilipo muaga aliweka wazi msimamo wake " samahani baba yangu mimi kwa nilivyo kufahamu na niliyo shuhudia katika siku hizi chache nimebadili mtazamo wa maisha yangu.... naomba niambatane nawe popote utakapo kwenda" kauli ile ilimshtua sana Babuu, mama Jackie alikuwa akifanya kazi kama meneja msaidizi aliona ni fursa pekee ya kujipatia kipato na kudhibiti mali kwa ajili ya watoto wake hivyo alikubali kubaki Dar.

Babuu aliniita pembeni na kunipa kiasi kikubwa cha fedha, niichukuwa kiasi kidogo nikampatia Wendo ili aende kutafuta nguo na mahitaji yake mengine kama mwanamke nilikitia kibindoni,niliandaa mizigo yangu tayari kwa safari ya kijijini........... ENDELEA KUSOMA SEHEMU YA 32 YA SIMULIZI HII YA USO WA FEDHA.

FACE OF MONEY #31 [ENGLISH VERSION].

We were thrown down like a dead body, I hurt a logo with hands, a severe smell of medicine and blood of accidents made me feel so bad, I had closed my eyes to see the dead room workers not to discover if I was alive, I started by disturbing one eye I saw the workers in As far serving the many dead bodies in segerea, I woke up slowly and hid myself behind a dead body, I saw workers have no information, I took it slowly while waking up the dead were laid down despite having pain the whole body but I realized the danger would have been called if the police had called me. So that I can be put under security when the police told me not to keep them for them.

I followed gradually and reached the big door to come out. I gave him a sign to follow me, he raised me slowly from the middle of the dead and followed my way we went out, I tried to walk and walked and passed a big entrance to the hospital, I rent a taxi to my home, I used to get a bath together. And chronological, a woman is just a woman, chronological went to the kitchen and washed the water and came to me to clean all my wounds, George and Geoffrey when they saw me crying a lot because I was swollen in my face and especially in my mouth, after a short time my father entered " brother... there is something. Which is going on in your life that I don't know? Why hide me brother?"babuu spoke so much angry, I had nothing to answer, I kept quiet and failed to look at him on the face" brother you have been thug you forgot that it is the cause of our father's death? Brother, why are you doing this? We were poor dog but God blessed us now we have our own things but still you don't care you want to die so that I can remain alone????" there i raised my face to look at the father I saw him crying out of tears and a very sad face, I remembered how he was killed father, I heard very painful in the heart .

I woke up and hugged my father for a moment and then I told him " from now on you will be my guardian I am going back to the village.... I have done so many sins..... I don't need to have anything anymore... I leave you everything... take care of the wealth to keep us, I trust you so much I depend on you so much.... the life that I lived and the environment forced me back to the village.... remember the world huh world hero... you can't compete with the way you came.... Reduce Women you will live " I hugged him again father let's sit all of us in severe pain until the chronological came to embrace us all And she wept with us.

Father stood up and looked at me and failed to stop crying and looking at me how I was beaten, he turned out and went out, I just remained with some things, I got up to bed, and he went to the kitchen to prepare food because hunger was really hurting us.

Father returned shortly, went to follow Jackie's mother, when he went in and came straight to the room and found me sleeping, he saw the designs tips on my back, she was shocked and shouted for mourning, I was shocked from sleep and I turned " what have we been attacked? " the father came quickly, I was in the sleep of sleep, when the consciousness was calm I saw mother's children Jackie, I rose up quickly and hugged him but when she saw me in the face she lost consciousness.

It started the job of kumpepea, first service and put him in a clean air we helped each other with father, after giving him so much he woke up but he was so tired, I knew he still needs fresh air, I mentor her to sleep and rest first.

Father went to talk to chronological in the kitchen " I'm sorry who are you? How do you know my brother?" chronological smiled " " Okay.... Okay.... okay well how did you know this man?" " at work " " don't tell me a good woman like this and you thug!!!" " No.... No.... no my brother. ... I am sharing beauty contest " " MH! It doesn't enter into mind... where did you spread with beauty where and where?" " I told me..." when he raised his face he met with my eyes he failed to continue " Enhe.... Enhe tell me I will give you a huge amount of money " Babuu didn't realize that I was standing behind him chronological He failed to keep talking. He bowed his head down "calm on tell me don't be ashamed. Can I ask you....... tell me please" I saw helping him chronological and cut the statement. Father is intervene by throwing his shoulders up a little bit, he came out without turning back.

I swim to him, he was shaking so much " don't be afraid I am the one who has all these wealth you are very safe " he responded by shaking his head " well.... now don't dare to tell him anything this man.... again don't worry he will go through you now you will give birth until grandchildren " I fed him a little so that my father doesn't destroy. Activities.

I felt myself like a week at my home, it was hard to sleep because in the room I slept with Jackie's mother, chronological slept in another room, I thought the caterpillar could go into the room for the room, it had to wake up four to five times in one night to make sure she is safe.

After a week I am preparing to go back to the village, Jackie's mother had to stay in dar es salaam, when I sent her, she exposed her stand " sorry my father for what I knew you and what I witnessed and what I witnessed in these few days I have changed my view of my life.... I pray to meet you anywhere. When you went " the statement really shocked the father, Jackie's mother was working as an assistant manager saw it was the only opportunity to earn income and control wealth for her children so she agreed to remain in dar.

My Father called me aside and gave me a huge amount of money, I was not a little bit I gave her to go and look for her clothes and other needs as a woman I put in hunting, I prepared my luggage ready for a village trip.........CONTINUE TO READ PART 32 OF THIS NARRATIVE KNOWN AS FACE OF MONEY.

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.