USO WA FEDHA | FACE OF MONEY.
USO WA FEDHA # 25 [SWAHILI].
MTUNZI: Sunday JoaquimContact: 0658593797
Macho yalinitoka kumwona Selina mbele yangu tena ameshika kisu chenye makali,niliinuka kitandani kumkabili bila kujali maumivu ya mishono mgongoni na mkononi,nilihakikisha hanipi maumivu mengine "aaghh Selina... Selina ah mh!" Nilimwita Selina mara kadhaa ili kumlegeza lakini hakulegea hata kidogo, alikuwa mwenye nguvu nilijikaza kumkabili tulipekkeshana tukaangukia kitanda cha jirani,nilihakikisha siangukii mgongo nilijitahidi kumtanguliza Selina chini.
Tuliinuka tena niliona Selina atanizidi nguvu na kuniuwa,niliamua kufa au kupona nilisukuma Selina kwa nguvu zote, alienda kujipigiza kichwa kwenye kona ya meza ya chuma alilegea na kuanguka chini,nilipatwa na mshtuko nikijuwa nimemuua Selina,wakati nipo kwenye butwaa nikimuona Selina akijiokota okota,niwahi kisu chake kilicho kuwa kimeanguka pembeni nilikiokota nikamwahi pale chini ili nimmalize maana niliona wazi kuwa nikifanya mchezo ataniuwa kweli,niligeuka mnyama kutetea uhai wangu.
Nilimpiga teke kali sana usoni,Selina alipasuka puani kwa ndani damu nyingi ilianza kumtoka, akapoteza fahamu, nilimkalia juu ili nimtofoe tofoe afe kabisa nyama huyu.
Nilimchoma kisu cha kwanza tumboni,nilinyanyua kisu tena kabla sijashusha mkono nilidakwa mkono,nilijikuta nimeshikwa kwa nguvu na kunyuliwa juu juu "weeeeh tulia..... utauwaa... wacha... mshike huyo" yalikuwa maneno ya wauguzi waliokuja kumwokoa Selina,nilidhamiria kumwua kabisa.
Niliinamishwa kwenye kitanda na kukandamizwa hapo kwa muda,nilianza kuona giza,mishono ilifumuka nikawa nimepoteza damu nyingi,nilipopata fahmu nijikuta ndani ya chumba cha upasuaji,sikuwa na nguvu hata ya kusogeza mguu,nilitolewa na kupelekwa wodini,nililazwa kitandani huku mkono mmoja umefungwa pingu kwenye kitanda,nilishangaa sana lakini sikuwa na uwezo wa kufungua mdomo.
Nilitundikiwa drip kadhaa,na kuangaliwa kwa karibu zaidi na madaktari Kumbe nilikuwa kwenye wodi ya mahabusu,nilikuwa mtuhumiwa wa mauwaji bila kufahamu,nilishangaa kuona nakaguliwa kila baada ya muda na askari
polisi,nilianza kupata nguvu nikathubutu kumuuliza askari mmoja "mbona nipo huku na nimefungwa pingu?" "Subiri atakuja wa kujibu swali lako hiyo si kazi yangu" alinijibu yule askari,nilinyamaza nikawa nasali kimoyo moyo tu, ghafla mlango ulifunguliwa wakaingia maafisa wa polisi wenye vyeo vikubwa wakiwa waneongozana na mtu aliyevalia suti nyeusi, moyo ulinipiga kwa nguvu nikiamini mwisho wangu umefika,nilikuwa na shauku ya kujuwa kilicho waleta na nini hatma yangu..... ENDELEA NA SEHEMU YA 26 YA SIMULIZI HII YA USO WA FEDHA.
FACE OF MONEY #25 [ENGLISH VERSION].
The eyes came out to see selina in front of me again holding a sharp knife, I woke up in bed to face her regardless of the pain of the designs on the back and hand, I made sure she didn't hurt another pain " Aaghh Selina... Selina ah mh!" I called Selina several times to wash her but she didn't even wash her , he was strong. I tried to face him when we fell on a neighbor's bed, I made sure I don't fall back I tried to put selina down.We rose up again I saw Selina will be stronger and killed me, I decided to die or heal I pushed Selina with all strength, she went to beat her head in the corner of the metal table she ran and fell down, I got shock when I knew I killed Selina, when I was in the puzzled when I picked up Selina, when I was in the whole strength, she went to beat her head in the corner of the metal table she ran and fell down, I got His knife that had fallen on the corner I picked it up and I picked him down to finish him because I saw it clearly that if i made a game he will really kill me, I turned an animal to defend my life.
I kick him so hot on the face, Selina burst into the inside. Many blood started to get out of her, she lost consciousness, I sat her up so that I could shoot tofoe completely this meat.
I burned the first knife in the womb, I raised a knife again before I fell down my hand I drunk my hand, I found myself caught strong and raised up "wow relax..... you will kill it... stop... hold on that" were the words of nurses who came to save Selina, I tried to kill her. Very.
I was dropped on the bed and compressed there for a while, I started seeing darkness, the plans broke up and I lost a lot of blood, when I found myself in the surgery room, I was not even able to move my foot, I was removed and taken to religion, I was laid in bed with one hand tied in the knot. Bed, I was so surprised but I was not able to open my mouth.
I was hanged several drip, and more closely checked by doctors so I was in the prison, I was accused of murder without understanding, I was surprised to see that I am being reviewed every time by the police
Police, I started getting strength and I dare to ask him one policeman " why am I here and I am tied?" " wait he will come to answer your question that is not my job " He answered me that police, I was quiet and I became praying earnestly, suddenly the door was opened and they entered the police officers with Big titles when they were accompanied by a person dressed in black suit, the heart beat me strongly when I believed my end has reached, I had the desire to know what brought them and what my fate..... CONTINUE TO READ PART 26 OF FACE OF MONEY.
