USO WA FEDHA | FACE OF MONEY.
USO WA FEDHA # 24 [SWAHILI].
MTUNZI: Sunday JoaquimContact: 0658593797
Nilipoanguka sikujitambua tena mpaka baada ya kifikishwa hospitali na kupatiwa huduma ya kwanza,nilianza kupata fahamu kwa mbali sana, niliona kama naota mpaka nilipopata fahamu vizuri ndipo niligundua nipo hospitali baada ya kusoma jina la ile hospitali kwenye mashuka meupe niliyofunikwa nayo,nilichachawa nusura nikimbie hovyo lakini maumivu ya viwembe mgongoni yalinikumbusha tukio baya maishani mwangu,niligeuka huku na huko sikuona ninayemfahamu zaidi ya wauguzi na matabibu,niliwaza kwa haraka bila kujua la kufanya.
Mara kumbukumbu za mamaa Jackie zilinijia nikataka kukurupuka tena pale kitandani,ilikuwa ni jioni jua linazama Babuu alikuja kuniona na kuniletea chakula "pole sana kaka" aliongea Babuu "ahsante" " basi kaa ule kwanza alafu tutaongea" "sawa lakini nawezaje kula wakati wanangu sijui wana hali gani?" "ah wakubwa wale nimewaona wamesharudi shule" "hapana Babuu simaanishi George na Geoffrey wapo wengine na mama yao niliwapata Zaire wapo hotelini Kariakoo sasa sikuwaachia hela sijui watafanyaje?" "Mh! Kaka mbona mimi hukuniambia kuwa una watoto wengine?" " nenda kwanza uwaone alafu ndio uje kunilaumu" " ah wapi nikulaumu kwanza wewe nakujuwa utazuga mpaka nitasahau" " basi mimi sili" "basi kaka naenda" nilimwelekza hoteli akaenda,aliwalipia siku tatu zaidi nitakapotoka hospitali ndipo awalete nyumbani.
Babuu alirudi na kunipa taarifa ya kuwalipia mama Jackie na watoto, roho ilitulia nikaanza kula chakula,kijasho chembamba kilikuwa kikinitoka kuashiria uhai kunirudia,nilipomaliza kula ndipo Babuu alitaka kufahamu nini kilitokea "nilipokuwa Zaire maisha yalikuwa magumu mno huyu mwanamke alinisitiri sana kwa kunipikia, kunifulia na malazi ndipo baada ya muda si mrefu aliniambia kuwa ni mjamzito ndio wale watoto mapacha uliowaona,sasa mimi niliondoka kule sikuwa na mpango naye tena lakini kumbe alishanihoji kijanja na aliandika kila kitu,bila taarifa namshtukia huyo sebuleni eh eh eh zikakanza kupigwa Selina na mama Jackie nikaona dawa ni kuamulia na kumpeleka mama Jackie na watoto hotelini mpaka nitakapo tatua tatizo,sasa kule hotelini nikaona nijinyooshe kidogo daah kushtuka pamekucha nilikurupuka kurudi nyumbani kufika nikamkuta Selina kalala nikajua kweli kalala nikaingia bafuni nioge nivae nije THE HOOD ile natoka tu bafuni nasikia wembe umepita na makali yake nageuka kumbe Selina alijibanza pembeni ya mlango wa bafuni ile nitake kumzuia kanichana mkononi nikaona nigeuke nikimbie duh kanichanja tena mgongoni nikahisi kuishiwa nguvu toka hapo sikuijatambua tena napata fahamu najiona nipo hapa"
"Daah pole sana kaka kuchuma chuma kwa mboga mwishowe unachuma mboga chungu" "anhaa umeshakuwa mswahili eeh kwa hiyo unanicheka?" "hapana kaka ile wewe ulinitunga mpaka jina ukaniita mzee wa wachumba" " kwa hiyo unalipa kisasi" " hapana kaka tunaambiana sote sisi ni wanaume" "Vipi Selina ulimkuta?" " ningemchija hadharani bahati yake sana ametokomea pasipo julikana" "mmmh punguza hasira shemeji yako yule.... aseeh Selina mtamu daah asikwambie mtu alafu mzuri" "eh naona wewe sasa sikio la kufa yaani kwa aliyokutenda bado una msifia kiasi hiki?" Hapo nilinyamaza nikawaza kidogo nilijiona mjinga kiasi fulani, nilibadilisha mada "vipi THE HOOD jana palichangamka?" " kuna zaidi ya THE HOOD kaka pale tumelenga kila mjanja wa mjini anaongelea THE HOOD ndio gumzo la mjini" " sawa vizuri nilikuwa nafikiria tuanzishe pia bekari ya mikate na keki naona pia itatulipa sana" " hayo ndio maneno kaka hapo umenena vema" muda wa kuona wagonjwa uliisha Babuu aliniaga na kuondoka,nilibaki peke yangu nikitafakari maisha yangu na jinsi Selina alivyotaka kuutoa uhai wangu kwa nyenzo nyepesi sana,nilijiona mwenye mikosi duniani hakuna tena, baada ya muda nilipitiwa usingizi nikalala.
Nikiwa usingizini niliota ndoto mbaya za kutishatisha tu,baadae nilihisi kuna mtu amsimama pembeni ya kitanda changu,nilijitahidi kukurrupuka toka usingizini,nilipofumbua macho daah uso kwa uso na Selina,macho yalinitoka,sijui alipenya penya vipi mpaka akafanikiwa kuingia hospitali muda ule,alikuwa amevaa fulana nyeusi na suruali nyeusi akiwa na kisu mkononi, nilihisi kuchanganyikiwa ...ENDELEA NA SEHEMU YA 25 YA USO WA FEDHA.
FACE OF MONEY #24 [ENGLISH VERSION].
When I fell, I didn't recognize myself until after the hospital was delivered, I started to get consciousness from far, I saw that I was dreaming until when I got to know that I was in the hospital after reading the name of the hospital in the white sheets that I was covered with, I ran away but run away. The pain of blade on the back reminded reminded me of the worst incident in my life, I turned around and there I didn't see who I know more than nurses and doctors, I quickly thought without knowing what to do.Once the memories of mom Jackie came to me I wanted to stir you up again in bed, it was evening when the sun was drowned. Father came to see me and brought me food " sorry brother " spoke father " thank you " then stay the one first and then we will talk " " okay but how can I eat when my children don't know. What is the situation?" " ah elders I have seen them back to school " " no father I don't mean George and Geoffrey there are others and their mother I found zaire in the hotel in kariakoo, now I didn't leave them money, I don't know what they will do?" " MH! Brother, why didn't you tell me that you have other children?" " go first and see them and then come to blame me " " ah where I blame you first, I know you will see until I will forget " " then brother I'm going " I moved to the hotel and went, he also went out three days when I came out. The hospital then bring them home.
Father returned and told me to provide for the mother Jackie and children, the spirit gave me to eat food, sweat sweat was from showing life to me, when I finished eating, then my father wanted to know what happened " when I was in Zaire, life was very difficult, this woman gave me a lot of food, and she gave me life. Accommodation then after a long time she told me that she was pregnant are those twins you saw, now I left there I had no plan with her anymore but so she questioned clever and wrote everything, without any information I happened to that living room eh eh zikakanza to be beaten Selina and mother Jackie I saw The medicine is waking up and taking Jackie's mother and children to the hotel until when I solve the problem, now in the temple I saw that I should hang myself a little bit daah shocked the pamekucha I exploded back home to arrive and I found selina sleeping and I went to wear the hood and I came to wear the hood and I just heard that I should hang myself a little bit huh. Shocked Pamekucha I ran back home to arrive and I found selina sleeping and I went to wear the hood and I am turning so selina was useless next to the bathroom door, I want to block her in my hand and I saw her turn around and run away, I felt that I was losing strength since I didn't recognize it again, I find myself here I am here "
" huh! I am so sorry brother to get iron in vegetables, you end up getting bitter vegetables?" " you have already been a toothbrush huh so you laugh at me?" " no brother, that you called me a man of a couple " " so you pay revenge " no brother we are telling each other. It's men " " how did selina find her?" " I would have brought her in public luck so much she has gone out unknown " hmm reduce your anger your brother-in-law.... huh selina sweet daah she should not tell anyone then good " " eh I see you now a dead ear I mean to the one who did you You are still praising this bit?" when I kept quiet and thought a little bit I saw myself a bit stupid, I changed the topic " how is the hood yesterday?" " there is more than the hood brother when we focused on every city clever talking about the hood is the city chat " Ok well I was thinking we should start also a bekari of bread and cake I see it will also pay us a lot " " those are the words brother there you have spoken well " time to see the sick ended babuu passed away and left, I remained alone thinking about my life and how Selina wanted to give my life for material Very Easy, I saw myself who has misfortunes on earth no more, after a while I fell asleep I slept.
When I was in sleep, I dreamed bad dreams of making me, later I felt someone standing beside my bed, I tried to stir you up from sleep, when I opened my eyes daah face to face with Selina, the eyes came out, I don't know how she passed through until she succeeded in the hospital, she was wearing. Black and black pants with a knife in hand, I felt confused .........CONTINUE WITH PART 25 OF FACE OF MONEY
