Notification texts go here Contact Us Buy Now!

USO WA FEDHA | FACE OF MONEY # 04

USO WA FEDHA | FACE OF MONEY

USO WA FEDHA | FACE OF MONEY #4 - BONGOLIFE

USO WA FEDHA # 04 [SWAHILI]

MTUNZI : Sunday Joaquim
Contact : 0658 593 797

"Jamani mume wanguuuuu" kilikuwa kilio cha mama Mlay,Dokta alianza kutokwa mapovu mdomoni,wafanyakazi waliokuwa ndani walikuja kusaidia kumwinua,walimwingiza ndani wakamlaza kwenye kochi sebuleni,Mama Mlay alipiga simu kwa wadogo zake Dokta Ephraim na Aaron,walikuja haraka sana,wakati huo mimi nilipata wasiwasi juu ya uzima wa Dokta lakini pia uzima wangu na Babuu endapo lolote likitokea,wadogo zake Dokta walishauri wampeleke hospitali,walimpakia kwenye gari na kumkimbiza hospitali,Dokta alipewa kitanda sehemu ya wagonjwa mahututi,taarifa za kuuguwa ghafla kwa Dokta zilisambaa haraka sana,watu wengi walifurika hospitali kuja kumjulia hali,hawakurusuhusiwa kumwona kwasababu ya hali yake ilikuwa mbaya,alikuwa mwema sana kwa watu,alisaidia wengi ndiyo maana watu wengi walifurika hospitali.

Baada ya dokta kuondolewa nyumbani mimi na Babuu tuliondoka pia,maana nilijuwa wazi kuwa mama Mlay akirudi akatukuta pale ingekuwa balaa,tulirudi makazi yetu ya awali stendi kuu ya Mabasi Moshi mjini,maisha yetu ya pale stendi yalikuwa mabaya na magumu mno,ukosefu wa chakula,maji safi ya kunywa na kuoga,kupigana na wenzetu wenye maisha magumu kama sisi,kuvuta bangi,uonevu wa bila sababu vilikuwa ni sehemu ya maisha yetu,hakuna aliyetuhurumia,hatukuwa na msaada wowote,ilinilazimu kwenda kuomba kazi ya kukatisha ticketi za Mabasi ya mikoani,mara ya kwanza nilikataliwa kwasabau ya umri,sikuchoka nilienda mara ya pili,ndipo mmoja wa wale wanokatisha tiketi akasema "jamani kwani hii nayo ni ajira? mpeni tuone" walibishana wao kwa wao mwisho walinipa kitabu cha tiketi.

Kwa kuwa nilikuwa mdogo sana,niligeuka kivutio kwa wasafiri,wengi walipenda kuongea nami hivyo niliuza tiketi nyingi sana kwa siku,hali ile iliwashangaza wengi pale stendi,nikaanza kugombewa,kila Basi lilitaka kuuza tiketi nyingi waliniwahi asubuhi sana,nilionekana wa ajabu na nilileta changamoto kubwa kwa wapiga debe na wauza tiketi wenye umri mkubwa,nilipachikwa jina la utani USO WA FEDHA.

Mwisho wa siku nililipwa fedha yangu ya siku na kuitunza vema,nilitafuta chumba cha kupanga,nilipata chumba kwa taabu sana,wenye nyumba walinikataa kutokana na umri wangu,miaka ilisonga na umri ulisogea,kimo na maarifa viliongezeka,ikatokea tajiri mmoja mwenye Mabasi aliona ushindani wa kunigombea pale stendi ni mkubwa,aliamua kunitorosha na kunihamishia Dar,nilifika jijini Dar,nilipangiwa chumba kimoja mtaa wa Tabora Ilala,nilikuwa na Babuu na yeye alishakuwa mkubwa,nilimwombea kazi kwa tajiri yangu,alikubali kumchukuwa.

Babuu na yeye aliwashangaza watu pale stendi ya Mabasi Kisutu wakati huo,sifa zake za uuzaji tiketi zilivuma stendi ya Mabasi Kisutu na Mnazi Mmoja,wenye mabasi walikuwa wakimgombea awauzie tiketi zao,aliuza tiketi kwa muda wa miaka minne ndipo aliamua kujifunza udereva.Tajiri yangu alikuwa anapenda sana kuwinda wanyama pori,aliniomba niende naye porini kuwinda,tulifunga safari mpaka Mikumi mkoani Morogoro,tulipiga kambi,akaanza kunielekeza jinsi ya kutumia bunduki,alinifundisha kwa siku kadhaa na wakati mwingine aliniruhusu kipiga wanyama wadogo kama Swala,tuliendelea na uwindaji kwa siku kama wiki hata siku hiyo ilitokea Simba mzee alikuwa akitunyemelea kwenye kambi yetu,niliokota bunduki haraka sana,yule Simba alikuwa anakuja kwa kasi,nilipo mlenga risasi alikuwa ameruka juu ili kutukabili,risasi ilimpiga kidevuni.

Simba aliangukia miguuni pangu,kwa woga nilipoteza fahamu kwasababu nilijua ameshanimaliza,baada ya muda nilianza kusikia watu wakiongea "bahati yake sana...jamaa ana bahati sana yaani kukosa shabaha leo ulikuwa mwisho wake Simba hana mchezo" niliinuka taratibu nikiwa na uchovu,niliwauliza kwani imekuwaje? wote walicheka "we pumzika kwanza utajua baadae" mmoja wa watu tuliokuwa nao alinijibu hivyo,nilijaribu kuulizia baadae kuwa nini kilitokea hakuna aliyetaka kuniambia mpaka tuliporudi Dar ndiyo walinisimulia ilivyokuwa,tajiri yangu alianza kuniamini zaidi kwa ujasiri niliouonyesha,alikuwa akinituma kazi zake nyingi za pesa,hakumwamini mtu ila mimi tu.

Ilifika wakati wa tajiri yangu kujitambulisha rasmi kwangu kuwa yeye ni nani na anafanya nini "sikiliza Egon maisha ya mwanaume ni mapambano,uwoga wako ndiyo umasikini wako,leo nataka nikueleze mambo mazito ukielewa sawa hukuelewa shauri ni lako unanielewa?" aliongea tajiri yangu,niliitikia kwa kutikisa kichwa juu chini kisha nilikaa kwa umakini mkubwa sana kumsikiliza "ni hivi nimekuona wewe kijana hodari sana na mwaminifu nami nimekuamini....nataka nikueleze siri za mafanikio lakini tafadhali usiziseme popote kama hutaziweza basi funga mdomo wako" aliongea huku akiweka kidole chake cha shahada mdomoni ili kunisistiza usiri "wewe umeshajuwa kutumia bunduki sasa kwa nini ufe masikini? nitashangaa sana kama utachaguwa umasikini kuwa ni maisha yako".

Alinyamaza kwa muda kidogo ili kuona nimechukuliaje kauli yake ya mwisho alafu aliendelea "wewe bado kijana sana lazima upange maisha yako kuanzia sasa usipo changamka uzeeni utapata shida.... labda nikwambie kitu..... mjini hakuna ngekewa kila kitu ni kupambana tu sasa leo usiku nataka ukapige kazi moja ya kutumia bunduki hutakuwa peke yako wapo wengine utwaona na watakuongoza" daaah ! hapo niliishiwa nguvu,"unamaanisha ujambazi Bosi? mh ! mh !" nilimuuliza tajiri yangu "wewe vipi unauliza maswali gani hayo? sasa matumizi ya bunduki usiku yatakuwa ya nini kama si shughuli hiyo?" "naomba nifikirie kwanza Bosi maana mh!" "ufikirie nini zaidi muda unakwenda lazima kujipanga mapema wacha uwoga wewe".................. ENDELEA NA SEHEMU YA 05 YA USO WA FEDHA.

FACE OF MONEY #04 [ENGLISH VERSION]


"oh my husband" was the cry of mama mlay, the doctor started getting foam from her mouth, the workers in the inside came to help raise her, they threw her in and laid her on the couch in the living room, the mother mlay called to her young ones doctor Ephraim and Aaron, they came fast at that time. I got worried about doctor's life but also my life and father if anything happens, his younger ones advised him to take him to the hospital, they carried him to the car and drove him to the hospital, doctor was given a bed part of ill patients, information about sudden people spread out quickly. Many were flooded to the hospital, they were not allowed to see him because of his situation, he was not allowed to see him because of his situation, he helped many people, that's why many people flooded the hospital.

After the doctor was removed from home I and my father left too, because I knew clearly that the mother mlay came back to akatukuta where it would be a disaster, we went back to our previous residence at smoke in the city, our life at the station was very bad and very difficult, lack of food, Pure Drinking water and bath, fighting with our colleagues with hard life like us, smoking marijuana, non-cause was part of our lives, no one pity us, we didn't have any help, had to go to ask for a job to cancel local bus buses, At the first time I was rejected because of ages, I didn't get tired I went the second time, then one of those who cancel the ticket said " guys, is this also employment? Give him let's see " they disputed with them at the end they gave me the book of tickets.

Since I was very young, I turned to attraction for travelers, many liked to talk to me so i sold a lot of tickets per day, the situation surprised many at the station, I started being prayed, every then wanted to sell many tickets they ever got me in the morning, I looked amazing and brought a big challenge For voters and sellers of old tickets, I was named joking face of money.

At the end of the day I paid my money for the day and kept it well, I looked for a room for a lot of misery, the owners rejected me from my age, the years moved me from my age, the years moved on, stature and knowledge increased, came out one rich with buses saw competition Running for me at the station is big, he decided to run me and moved me to dar, I arrived in dar es salaam, I was assigned to one room in tabora town, I had a father and he was great, I asked him for a job for my rich man, he agreed to take him.

Father and he amazed people at the bus station at kisutu at that time, his reputation of selling tickets blew a bus station in kisutu and one coconut, with buses were candidate to sell their tickets, he sold tickets for four years and decided to learn the driver. My rich man was very loving to hunt wild animals, he asked me to go with him wild hunt, we scored a trip to ten in morogoro region, we kicked out, he started to direct me how to use guns, he taught me for several days and sometimes allowed me to beat small animals like prayer, we kept hunting for A day like a week even that day it happened an old lion was floating in our camp, I picked up the gun very fast, the lion was coming fast, when I focused on the shot he had jumped up to face us, the bullet hit him in the chin.

A Lion fell at my feet, with fear I lost consciousness because I knew he has already finished me, after a while I started hearing people talking "his very lucky man... the guy is very lucky I mean lack of target today was the end of the lion he has no joke" I woke up slowly when I was tired, I asked them. How? They all laughed "we rest first you will know later" one of the people we were with answered me so, I tried to ask later that what happened no one wanted to tell me until when we came back to dar that's what they told me was, my rich started to trust me more with the courage I showed, he was sending me his lot of money, No one believed except me.

It came at the time of my rich to introduce myself to me who he is and what he is doing " listen to egon the life of a man is a struggle, your fear is your poverty, today I want to tell you heavy things when you understand ok you didn't understand the counsel is yours you understand me?" he spoke my rich man, I answered By shaking my head up down then I stayed seriously seriously listening to him "it's like this i have seen you a very brave and faithful boy and I have believed you.... I want to tell you the secrets of success but please don't speak it anywhere if you won't be able then close your mouth" spoke while putting his degree finger In your mouth to cover me confidentiality " you have already known how to use guns now why should you die poor? I will be surprised if you will choose poverty to be your life ".

He kept quiet for a while to see how I have taken his last statement and then he continued " you are still too young you have to organize your life from now on. If you don't live in old age, you will get problems.... maybe I should tell you something..... in the city no ngekewa everything is just fighting now tonight I want If you do one work to use guns, you will not be alone, there are others you will see and they will lead you " huh! There I ran out of strength," you mean gangster boss? MH! MH!"I asked my rich man" how are you asking which questions are that? Now what will be the use of a gun at night if it's not that activity?" " I ask you to think first boss because mh!" " what do you think more when time is going you have to prepare yourself early let fear you ".................. CONTINUE WITH PART 05 OF FACE OF MONEY

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.