MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.
MPENZI CHEUPE # 04 [SWAHILI].
MTUNZI: Sunday JoaquimContact : 0658 593 797
Alikutana na vifaranga vya kuku kama kumi,vilikuwa vidogo vyenye umri kama wa siku moja au mbili tangu kutotolewa,Brown alishtuka sana,macho yalimtoka,mapigo ya moyo yalizidi kwenda mbio,alijuwa ni ni mtu amegonga alipochelewa kufungua ndipo aliweka wale vifaranga,aliinama ili akishike kimoja,ghafla vilipotea,Brown alirudi mbio ndani kwake na kujifungia,akiwa bado amesimama hajui la kufanya,alisikia vyombo vikianguka jikoni,aliogopa kwenda,aliamua kuingia chumbani kwake na kujifungia,alijifunika shuka gubigubi na kupitiwa usingizi.
Asubuhi alipoamka alikwenda kuchemsha chai ili apate kifungua kinywa,wakati chai inachemka aliwaza "hiki kinachotokea kwenye maisha yangu ni nini? au kweli Salma ni mzimu?" yalikuwa maswali bila majibu kichwani mwa Brown,chai ilichemka alimimina na kuketi mezani akanywa chai,alipokaribia kumaliza aliona pembeni ya meza karatasi nyeupe imekunjwa vizuri,aliichukuwa na kuikunjua aliona imeandikwa "mpenzi mpishi mzuri wa chai,asante kwa kifungua kinywa,siku nyingine ongeza na viungo ili inoge zaidi,wako mpenzi Cheupe" jasho jembamba lilikuwa likimtoka Brown "ina maana nipo kwenye hatari,nimtafute yule dereva tax huenda akawa na majibu sahihi" Brown aliongea mwenyewe kama kichaa.
Alijiandaa na kutoka kuelekea mtaa wa Aggrey,alipofika alikuta tax nyingi sana,aliulizia kwa kutaja muonekano wa yule dereva tax,ilikuwa vigumu kumpata "mbona hakuna mtu kama huyo hapa" Brown alijibiwa na mmoja wa maderava tax,alikata tamaa ya kumuona,wakati anaondoka alipofika karibu na Mnazi Mmoja aliomuona yule dereva tax alikuwa na abiria wenye asili ya Asia,alipotaka kusogelea ile tax ilianza kuondoka,alijaribu kuifuata bila mafanikio,aliamua kurudi nyumbani kupumzika akiwa mwenye lindi la mawazo.
Brown alipokaribia nyumbani alipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kuiona ile tax imepaki mbele ya nyumba yake,alipiga hatua za haraka kuiendea ile tax,alipokaribia ile tax ilianza kuondoka "mh ! hii sasa maana yake nini? nipo macho naota?" alijiuliza maswali katika hali ya kutoamini anachokiona,maisha yake sasa yalijawa na mauzauza,aliamua kutulia nyumbani,mpaka giza lilipoingia,alienda kwa mama ntilie kula na kurudi kulala,siku ilikuwa mbaya kwake,alilala katika hali ya unyonge sana mpaka palipo pambazuka hapakuwa na kituko chochote,alijiandaa kwenda kwenye biashara zake,alifika kituoni kusubiri Basi kama abiria wengine,Basi lilifika,lilikuwa tupu,abria wote walikuwa pale kituoni walipanda.
Basi liliondoka kuelekea katikati ya jiji,cha ajabu lilipita vituo vyote bila kusimama,Brown alishangazwa na mwenendo wa lile Basi ndipo aligundua kuwa halikuwa na kondakta,wakati akiendelea kujiuliza mara abiria wote waligeuka kumwangalia,hawa kumsemesha neno lolote,Brown alipigwa butwaa alipo ona sura za kutisha za watu aliokuwa akiwafahamu ambao walishakufa miaka mingi iliyopita,mapigo ya moyo yalimwenda mbio nusu yasimame kwa woga,alikuwa ameketi kwenye siti ya nyuma kabisa "hiki nini tena!" alitamani kushuka lakini alijiuliza atawapitaje wale watu,haja ndogo ilimtoka bila kujijua,utanashati wote ulimwisha,mara lle basi lilisimama katikati ya msitu,wale watu walimgeukia tena kumwangalia,alielewa kuwa walimtaka ashuke,Brown alishuka,mmoja wa wale watu alimsukuma singi kama vile alimwambia usirudie tena.
Palikuwa ni mazingira ya kutisha sana,msitu mnene kiasi gari ziliwasha taa machana kupita eneo hilo,Brown akiwa katika hali ya woga na kutetemeka Basi liliondoka na kumwacha peke yake pale msituni,ghafla alisikia upepo mkali ukivuma,hali ya giza iliongezeka,radi zilipiga kwa fujo,Brown akiwa amesimama hajui wapi pa kuelekea,ghafla alimuona mtu amesimama mbali kidogo na pale alipokuwa Brown,alikuwa amevaa nguo nyeupe sana,alimpa Brown ishara amfuate kuelekea kule lilipotoka Basi,Brown alijuwa anaonyeshwa njia ya kutoka pale msituni na kumbe.............ENDELEA KUSOMA SEHEMU YA 05 YA SIMULIZI YA WHITE LOVER.
WHITE LOVER #04 [ENGLISH VERSION]
He met chicken chicks like ten, they were small age like one or two days since they were not released, brown was so shocked, the eyes came out, the heart of the heart kept going to run, he knew it was someone who hit when it was late to open it then he put those chicks, bowed down so that he could hold it. One, suddenly lost, brown ran into him and locked himself, while he was still standing, he heard the vessels falling in the kitchen, he was afraid to go, decided to get into his room and shut himself up, covered himself with a bed and fell asleep.In the morning when he woke up he went to boiling tea to get breakfast, when the tea was boiling he thought " what is this happening in my life? Or indeed salma is a ghost?"it was questions without answers on brown head, the tea was boiling and sat on the table drinking tea, when he was about to finish she saw it beside the table white paper well filtered, she didn't know it and saw it written" a good tea cook, thank you for the Breakfast, another day add with ingredients to get more fat, they are a white lover " sweat sweat was coming from brown " means I'm at risk, looking for that taxi driver might have the correct answers " Brown spoke himself as crazy.
He prepared himself and from going to aggrey street, when he arrived he found a lot of tax, he asked by mentioning the appearance of the driver taxi, it was hard to find him "why is there no one like that here" Brown was answered by one of the maderava taxi, he gave up hope to see him, when he leaves Near one coconut tree he saw the taxi driver had passengers with an Asian Nature, when he wanted to swim the taxi started to leave, he tried to follow it without success, he decided to go back home to rest with a thought guard.
When Brown came home, he got a huge shock after seeing the tax sitting in front of his house, he took quick steps to go to the taxi, when he approached the taxi started to leave " MH! What does this now mean? I am awake I dream?" he asked himself questions in the situation of not believing what he sees, his life was now full of weakness, he decided to rest at home, until when the darkness entered, he went to the mother ntilie to eat and went back to sleep, the day was bad for him, he slept in a very weakness until Where it was dawn, there was no doubt, he prepared to go to his business, and arrived at the station waiting for then as other passengers, then it came, it was empty, all the passengers were at the station.
So it went out towards the city center, strange passed all stations without standing, brown was amazed by the trend of that then he realized that he had no conductor, while he continued to ask himself once all passengers turned to look at him, these have said any word, brown was beaten when he saw the faces The horror of the people he knew who had already died many years ago, the heart beat ran half to stand out of fear, he was sitting on the back seat " what again!" he wanted to come down but he asked himself how he will pass those people, the little need came out without knowing himself, he will get the shirt. All of you killed him, immediately it stood in the middle of the forest, those people turned him back to look at him, he understood that they wanted him to go down, brown came down, one of those people pushed the singer as he told him don't come back again.
It was a terrible environment, a bit fat forest. The car lit a lamp in the slaughter to pass the area, brown when he was in a state of fear and trembling then it went out and left him alone in the forest, suddenly he heard a severe wind blowing, the dark state increased, the thunder beat , when brown was standing he doesn't know where to go, suddenly he saw someone standing far away and when he was brown, he was wearing a very white dress, he gave brown a sign to follow him towards where it came from then, brown knew he was shown the way from there in the forest and so...........CONTINUE TO READ PART 5 OF WHITE LOVER
