Darasa la mapenzi na ndoa
*KWA NINI HAIWEZEKANI MKE NA MUME KURUDIANA BAADA YA TALAKA TATU?*
Allaah Aliyetukuka Anatuambia yafuatayo kuhusu hilo:
```“Talaka ni mara mbili. Kisha ni kumuweka kwa wema au kumwacha kwa ihsani...Na kama amempa talaka (ya tatu) basi mwanamke huyo si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine” (al-Baqarah [2]: 229 – 230).```
Inafahamika kuwa kila Dini au ideolojia yoyote ina nidhamu yake ya kuendesha maisha kwa hali na njia iliyo nzuri. Bila ya nidhamu basi mahusiano hayatakuwa mema wala mazuri.
Kukiwa hakuna nidhamu na sheria madhubuti, mara nyingi itakuwa ni kuchezeana na katika kufanya hivyo mwanamke ndiye atakayeumia zaidi. Ili kumlinda mwanamke asiwe ni mwenye kuchezewa na mwanamme, ndio ikawekwa nidhamu kuwa talaka ni mara tatu tu.
Mara nyingi mume huwa anamwambia mkewe kuwa yeye anampenda sana lakini kwa kosa dogo tu huwa tayari ametoa talaka. Kwa minajili hiyo Uislamu ukaweka kuwa hakuna dhihaka katika talaka, hata ukiitoa katika dhihaka talaka itakuwa imepita.