JINSI YA KUTENGENEZA BUTTERCREAM YA KUPAMBIA CAKE NI RAHISI SANA
Ingredients / Mahitaji
1➡ Siagi isiyokuwa na chumvi gram 283 ( Unsalted butter )
2➡ Icing sugar gram 288 ( Sifted sugar )
3➡ Arki ya vanilla kijiko kimoja cha kulia ( 1 tablespoons )
4➡ Rangi chakula ya kijani kiasi tu inategemea na wewe mwenyewe unataka ikolee vipi nyingi au kiasi tu ( au pia unaweza ukatumia rangi nyengine yoyote unayopenda wewe ya chakula )
5➡ Maziwa ya maji ya kawaida vijiko viwili mpaka vinne vya kulia
6➡ Sprinkle ( hivi vinapatikana supermarket vimekaa kama vipipi flani )
Recipes / Maelezo
1➡ Chukua bakuli tia Siagi yako anza kusaga kwa mashine ya cake au mwiko wa kusongea ugali mpaka ibadilike rangi iwe cream
2➡ Baada ya hapo achia kusaga mimina Icing sugar yako na Endelea kusaga mpaka uhakikishe Icing sugar imechanganyika vizuri
3➡ Baada ya hapo achia kusaga tia arki ya vanilla au yoyote unayopenda wewe mwenyewe pamoja na Rangi ya chakula ya kijani au yoyote unayopenda wewe mwenyewe pamoja na Maziwa ya maji ya kawaida
4➡ Endelea kusaga mpaka uhakikishe rangi yako imechanganyika vizuri
5➡ Chukua cake yako ikate sehemu ya juu kabisa kama imevimba na kama haijavimba si lazima kuikata
6➡ Anza kuieneza cake yako buttercream juu na pembeni moto halafu iweke sawa kwa kutumia spatula au kisu cha kusawazishia cake iwe smooth vipo special na vinapatikana maduka ya vifaa vya cake ( au unaweza ukaipamba zaidi )
7➡ Baada ya hapo ipake sprinkle Jemmy juu ( sprinkle hizi zinapatikana supermarket vimekaa kama vipipi flani )
8➡ Baada ya hapo unaweza ukaiweka kwenye fridge cake yako ili ipate kukazana isigande ipate baridi tu
9➡ Baada ya hapo itoe cake yako kwenye fridge
10➡ Na mpaka hapo cake yako ipo tayari kwa kula ni rahisi sana
Please usisahau ku-like pamoja na ku-comment
Ahsanteni sana kama una swali au hujafahamu vizuri uliza kwenye comments usione tabu .