Kuna miongozo mingi juu ya jinsi ya kutengeneza blogi za pesa, Lakini utofauti ni kwamba mwongozo huu ni wa bure na rahisi kuelewa.
Kwenye ukurasa huu nataka kukutembeza kupitia mchakato wa jinsi ya kutengeneza blogi za pesa. Ni sawa kwa wale ambao tayari wana blogi lakini ikiwa bado hauna blog ningependekeza uangalie mwongozo wetu wa kuanzisha blogi yako (Ndio hatua ya 1 kabisa).
Hadithi yangu ya Jinsi nilivyoanza Kuingiza Pesa kupitia Blogging.
Mnamo 2015 nilianza kublogi, siku moja nilipata msukumo baada ya kuona blogi nyingine na kuvutiwa nazo na kwa wakati huo Sikuwa na wazo kwamba kile nilikuwa nikifanya kinaweza kusababisha mabadiliko katika maisha yangu na kazi zangu na Sikujua kama kitu hiki kingekuja nitengeneza kipato cha kutosha zaida ya hata cha baadhi ya watu walioajiriwa.Sikuwa na uzoefu au profile yoyote ile online, Sikua na uwezo wa kiufundi na sikua pia na uwezo mzuri wa uandisha na kuwasilisha vyema taarifa au mada kwa njia ya maandishi.
Sikufanya pesa yoyote kutoka kwa blogi zangu za kwanza kwa karibu miezi 18 (sikujua hata kama naweza kujaribu) na nilipoanza kujaribu kupata pesa kutoka kwa blog, mapato ya kwanza yalikuwa dola chache tu kwa wiki - lakini polepole mda ulivyokuwa unaenda mapato yangu yaliendelea kuongezeka siku baada ya siku mpaka kufikia kipato ambacho kimenifanya nifanye blogging kama kazi yangu ya full time.
Jinsi ya kupata Pesa Kupitia Blog yako?
Mimi huulizwa mara nyingi jinsi ya kutengeneza blogs za pesa kwa hivyo nataka kwenye nakala hii kuweka hatua kadhaa za msingi ambazo naona wanablogu wengi wanaopata pesa kutoka kwa kublogi wanapitia.Hizi ndio njia za kupata pesa kwa kufanya blogging:
- anzisha Blog. Anza Kuunda na Kutengeneza Blog
- Anza kuandika makala (Posts) ambazo watu wangependa kusoma
- Tafuta wasomaji
- Jenga ushirika na wasomaji wanaokuja kwenye blog yako
- Anza kupata pesa kupitia wasomaji wa blog yako
Kwa kiwango fulani mchakato huo ni rahisi - lakini unahitaji kujua mbele kuwa kuna mengi kwa kila hatua na chini nitakupa hints za kila hatua na baadhi ya tricks unazoweza kutumia kurahisisha mchakato mzima wa kuanzisha blog zitakazo kuingizia pesa.
Endelea kusoma ilikujua jinsi ya kupata pesa kutoka kwa blogi.
1. Anzisha Blogi
Ili kuanza kupata pesa kupitia blogging utahitaji kuwa na blogi. Ni dhahiri pia hili huwa ni kikwazo kwa blogger chipikizi wengi wanaokuja na wazo la kublogi wakiwa na historia kidogo au isiyo ya kiufundi.Ikiwa hivyo - usijali! Ilikuwa hadithi yangu pia na wanablogi wengi wanaanza kuhisi kuzidiwa kidogo na mchakato wa kuanza blogi yao.
Ikiwa unahitaji msaada mdogo ningependekeza sana uangalie nakala yangu Jinsi ya Kuanzisha Blogi ambayo mimi nimeiandaa hatua ambazo unahitaji kuchukua ili kuinuka na kuwa blogger wenye mafanikio. Sio ngumu sana kama unavyofikiria!
Soma zaidi juu ya kuanzisha blogi:
[Jinsi ya Kuanzisha Blog]
2. Anza kuandika Posts Kwenye blog yako
Blogi sio blogi kama haina posts ndani (Content) kwa hivyo mara tu utakapoanzisha blogi yako unahitaji kuelekeza umakini wako katika kuunda maudhui muhimu. Kile unachochagua kuunda au kuandika kitategemea kidogo juu ya mada unayochagua kuandika (Wanablogu waliofanikiwa zaidi wanazingatia kublogi kwao kwa kuanzingatia mada yao ya uandishi au idadi ya watu ambayo wanaiandikia).Technique Muhimu katika kuandika post zako ni kuifanya ziwe za muhimu iwezekanavyo kwa wasomaji wako. Zingatia kuunda maudhui ambayo hubadilisha maisha ya watu kwa njia fulani itakuwa aina ya maudhui ambayo watu watathamini zaidi na zitawafnya watu wakujua na kukuamini - ambayo ni muhimu ikiwa baadaye unataka kupata pesa kutoka kwa blogi yako.
3. Anza Kutauta Wasomaji
unapokuwa ukitengeneza post zako ambazo watu wangependa kuzisoma ni rahisi sana kujikuta ukitumia muda wako mwingi ulioutenge kwa ajili ya blogging kuandika post ambacho sio kitu kibaya but inaweza ikawa kama mtego.Ikiwa unataka kupata pesa kutoka kwa blogi yako unahitaji kuzingatia sio tu kwenye blogi nzuri lakini pia ni muhimu kutoka kwenye blogi yako na kuanza kuitangaza.
Kuna njia nyingi za kujaribu kuongeza wasomaji kwenye blogi yako ambayo nimeandika katika machapisho ya blogi yaliopita lakini ni muhimu kuingia katika mikakati hii yote ukikumbuka kuwa wewe haipaswi kutafuta tu watu waingie kwenye blog yako bali unatakiwa utafute wasomaji ambao watakuwa wakisoma blog yako mara kwa mara.
Anza kwa kufikiria kwa uangalifu juu ya aina ya msomaji ambaye ungependa kusoma blogi yako. Unaweza kupenda kuunda picture ya msomaji huyo kichwani au ni vizuri ukaandika kabisa aina ya msomaji ambaye ungependa asome blog yako ili kukusaidia kujua ni nani unajaribu kumvutia kusoma blog yako.
Mara tu ukijua ni nani unatarajia kusoma blogi yako jiulize ni wapi mtu/watu wa aina hiyo wanaweza kuwa tayari wameikusanyika online? Anza kuorodhesha mahali ambapo wanaweza kukusanyika:
- Je, wanasoma blogi kadhaa? Orodhesha 3 za juu
- Je! Wanashiriki katika forum fulani? Orodhesha 3 za juu
- Je, wanasikiliza podcast? Orodhesha 3 za juu
- Je! Wanashiriki kwenye mitandao fulani ya kijamii? Orodhesha 3 za juu
- Je! Wanafuata akaunti gani kwenye kila moja ya mitandao hii ya kijamii? Orodhesha 3 za juu
Kila moja ya maeneo haya ambayo wasomaji wako tayari wanakuwa wamekusanyika inakupa fursa ya kukuza kujulikana kwako online (Online Presence) ikiwa ni kwa kuacha maoni mazuri kwenye comments za blogs au forums ambazo wasomaji watakao pendezwa na blog yako wanapatikana, kutoa au kuunda machapishokwneye blog nyingine kama mgeni (guest posting) au kwa kusaidia na kujibu maswali.
Ukiwa na orodha hii ya blogi, forums, podcast, akaunti za social medias utapata nafasi nzuri za kuanza kupata umaarufu na kuipa thamani blog yako pia na wewe kama mwandishi.
Technique ni kutambulika online, kuongeza thamani, kukuza uhusiano - sio kujihusisha na mazoea ya spammy
4. Jenga ushirika na wasomaji wanaokuja
Kwa umakini endelevu wa kuunda maudhui mazuri na kupata wasomaji wa blogi yako utaanza kugundua watu wanaotembelea blogi yako na kushiriki nawewe kwenye posts zako kwa kuacha comments au kwa kuasiliana na wewe.Katika hatua hii unahitaji kubadili mwelekeo wako ili ushirikiane na wasomaji hao na kujenga community.
Jibu maoni, uwafikie wasomaji hao kibinafsi na fanya kila unavyoweza kuwafanya warudi tena na tena kwa kujenga blog itakayoanya warudi na kuisoma kila unapopost makala mpya.
Tunza wasomaji ambao tayari unao vizuri na utakuta wanakusambaza neno la blogi yako na usaidie kuifanya blogi yako isomwe zaidi.
Kuwa na wasomaji ambao wako engaged na blog yako inakuwa ni rahisi kupata pesa.
5. Anza kupata pesa kutoka kwa wasomaji ulionao.
Hatua nne za kwanza ambazo ni kuanzisha blogi, kuandika posts, kupata wasomaji na kushiriki na kujenga uhusiano na wasomaji hao ni misingi muhimu ambayo unahitaji kweli kupata kuwa nayo tayari kabla ya kuweza kuunda mapato ya muda mrefu kwa kutumia blogi yako.sio siri kuwa kile nimekueleza ni kazi ngumu lakini ukifanya vizuri utajiweka sawa na kujikuta katika nafasi ya kuweza kupata pesa kutoka kwa blogi yako.
Pamoja na msingi huu sasa uko tayari kuanza kujaribu kupata pesa kutoka kwa blogi yako lakini unahitaji kujua kuwa sio kweli kwamba baada ya kuanzisha blogi yako, na kuwa na post za kutoshana na tayari umeshirikisha wasomaji kuwa pesa zitakuja zenyewe automatically.
Inachukua kazi endelevu na majaribio ya mara kwa mara kupata pesa kutoka kwa blogi yako.
Njia za kuingiza pesa kupitia blog yako.
Mojawapo ya dhana potofu kubwa ambayo naona wanablogi wanayo kuhusu kuingiza pesa kupitia blogi ni kwamba wanalazimika kuifanya kwa kupitia njia moja. Ukweli ni kwamba kuna njia nyingi za kupata pesa kutoka kwa blogi.1. Mapato ya Matangazo
Hapa ndipo blogi nyingi zinaanza. Mtindo huu wa kupata pesa kutoka kwa blogi sio tofauti na jinsi gazeti au majarida wanavyouza matangazo. Wakati wasomaji wa blog yako na umaarufu wa blog yako unapozidi kukuwa na kuongezeka utapata watangazaji watakaokuwa tayari kulipa ili kupata fursa ya kujulikana na wasomaji wako.Unahitaji kuwa na wasomoji wa kutosha kufanya mpango wa moja kwa moja na watangazaji au makampuni, lakini hilo lisikuumize kichwa kwakuwa kuna mitandao ya matangazo (kama Google AdSense) ambayo hufanya kama middleman na kuwezesha blogger wadogo kuweka matangazo kwenye blogi zao. Hapa ndipo wanablogi wengi huanza (hata mimi nilianzia hapa na bado naendelea kutumia njia hii).
2. Affiliate Marketing
Utafiti wa hivi karibuni wa wasomaji wa bongolife uligundua kuwa matangazo ya afiliate ndio aina ya kawaida ya mapato ambayo wasomaji wetu wanayo.Kwa maelezo marahisi - mapato ya affiliate ni wakati unapo weka link ya bidhaa ambayo inauzwa kwenye tovuti nyingine (chukua Amazon kwa mfano) na ikiwa mtu atafuata link yako na kuishia kununua bidhaa hiyo unapata gawio kwenye mauzo hayo.
Kuna zaidi ya hapo lakini hii ni sehemu nyingine nzuri ya kuanza na kupata mapato kwa blogi yako kwani affiliate programs ni rahisi kujiandikisha na ikiwa una watazamaji wanaohusika utapata kuwa wanafuata maagizo unayotoa kwenye bidhaa.
3. Kuuza Bidhaa
Wakati nilianza kupata pesa kutoka kwa blogi zangu kupitia matangazo na matangazo ya affiliate leo chanzo namba moja cha mapato ni kupitia kuuza eBook na kozi kwenye blogi zangu. Hizi bidhaa zinachukua mda na kazi ngumu kuunda lakini zimekuwa faida kwangu na kwa wanablogu wengine wengi.Bidhaa zinaweza kuwa za aina toauti tofauti kama vile eBooks au kozi za online lakini pia bidhaa zingine kama programu, ripoti n.k.
Aina nyingine ya bidhaa ambazo wanablogu wanauza ni bidhaa za mwili. Hii ni kawaida wakati mwanablogi akiwa na biashara lakini wakati mwingine wanablogi pia huunda bidhaa (T-shti nk) au bidhaa zingine zakuamishika mama simu, computer n.k.
4. Kutoa Huduma
Njia ya kawaida ambayo wanablogi wengi hutengeneza pesa ni kupitia kutoa huduma kwa wasomaji wao. Hii inaweza kuwa kitu chochote kutoka kwa kufundisha na kushauri, kuandika au kudesign, kubuni, mafunzo au huduma zingine za wakala.Wacha Tushirikishane kwenye safari ya kupata pesa kutoka kwa Blogi yako
Natumai kuwa nakala hii imekusaidia katika safari yako ya kupata pesa kutoka kwa blogi. Na kama unaswali lolote au ungependa kushare experience yako katika blogging nikotayari kuwasiliana na yoyote yule ambaye atakuwa tayari kuwasiliana nami na pia kama unaswali ambalo ungependa kujibiwa na community ya bongolife kuwa huru kuandika katika comment box na utajibiwa kwa haraka zaidi.
