Notification texts go here Contact Us Buy Now!

MKASA MAALUM WA KUSISIMUA: MWISHO WA UBAYA AIBU


#inasikitisha sana

Robert baada ya kumaliza chuo kikuu na kupata kazi katika kampuni moja pale ilala jijini Dar es Salaam alimuoa binti mmoja mwanafunzi wa diploma ya sociology katika college moja iliyopo mjini maeneo ya mnazi mmoja. Binti alikua mke wa KUTACHI yaani kama simu ya smartphone toleo jipya mtoto wa kike haelewi chochote kuhusu nidhamu katika ndoa wala namna ya kuishi na ndugu hususani ndugu wa mumewe.Hajafundwa kujua thamani ya wakwe wala ndugu anachojua ni kuchati, kupiga selfie na kupost picha Facebook kutwa nzima. Siku moja wakiwa sebuleni mumewe alimwambia,

"Mke wangu nimewakumbuka sana ndugu zangu (kaka zangu dada na hata baba na mama) kesho tujumuike pamoja na kula pamoja,,,,

Nitawaalika ili tujumuike nao ktk chakula cha mchana,itabidi uandae chakula kwa ajili yao."

Mke akasema kwa unyonge "Mmmmmmmmh Okay Sawa ucjal hubby mungu akipenda."

Asubuhi ya siku iliyofuata Robert akatoka kwenda kazini lkn baada ya masaa kadhaa akarejea nymbn na kumuuliza mke wake.

"Mke wng umeandaa chakula cha mchana kwa ajili ya wageni? maana baada ya lisaa limoja watakuwa wameshafika."

Mke akajibu "hapana sijapika kwani ndugu zako sio wageni hapa watakula chochote watakachokikuta."

Robert akamwambia Mungu akusamehe mke wangu kwa nini unayasema hayo ilihali tokea jana nilikuambia ya kuwa wazazi wangu wanakuja?

Na kwa nin hukuniambia mapema kuwa hutopika ilihali baada ya lisaa limoja wazazi wangu watakuwa hapa "nini sasa unafanya mke wangu."

Mke akamjibu "waache waaje nitawataka radhi kwani wao si wageni hapa watakula chochote watakachokikuta."

Basi Robert ikambidi aondoke pale nymbn kwa kukwepa fedheha.

Baada ya dakika kadhaa mlango ukagongwa mke akaenda kuufungua.

Kwa mshangao mkubwa alipofungua mlango akakuta wageni waliokuja hapo ni wazazi wake babaake mamaake dada zake pmj na kaka zake.

Akastuka kwa mshangao na kuwakaribisha ndani,

Baba akamuuliza kuwa mume wake yupo wapi?

Akajibu yule mwanamke kuwa alikuwepo hapa ametoka dakika chache kabla hamjafika.

Baba akamwambia "mumeo jana alitupa taarifa kuwa Leo anatuarika hapa tuje kula pmj chakula cha mchana sasa vipi yy ametoka si busara."

Yule mwanamke akastuka kwa taarifa hiyo na kuanza kujifikicha mikono yake huku akiipiga piga hali ya kuchanganyikiwa."

Ikambidi aingie ndani na kumpigia simu mumewe Robert akamwambia "kwa nn hukuniambia kuwa wazazi wng ndio wanaokuja?"

Robert 
 akamjibu "Wazazi wng na wazazi wako wote ni kitu kimoja/hawana tofauti
Mke akamwambia " Lete chakula huku kilichokuwepo hakiwatoshi kwani ni kichache sana hakitawatosheleza"
Robert akamjibu " Mimi nipo mbali na hao wageni watakula chochote kilichopo kama wewe ulivyokuwa ukitaka kuwalisha wazazi wangu"

Akiwa amepaniki,
akatoka nje akabaki mikono kichwani analia kwa aibu asijue cha kufanya maana hata ela ya matumizi alokua kaachiwa na mmewe kuandalia chakula kizuri wageni alikua ashaitumia kununua wigi jipya.

SOMO: Watendee watu kama vile unavyopenda kutendewa wewe.

Nakutakia Siku Njema, Mungu Akubariki na kukulinda

Usisahau ku COMMENT

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.