MTUNZI-ANDREW SHADU
TELL-0677884981
EMAIL-andrewshadu44@gmail.com
ILIPOISHIA....
Mwezi wa nne ulivyoingia mambo yakaanza kumuendea kombo Emile, Siyo kwamba Faraji kiemba hakumuhitaji bali ni mke wa Faraji kiemba ndiye alikuwa kikwazo, Nadra mrisho alianza kumtaka Emile kimapenzi huku akiahidi kumpatia pesa nyingi zaidi ya mshahara anaolipwa na Faraji kiemba. Nadra mrisho alianza kumletea Emile mitego ya kila aina ili ampate kimapenzi kitu ambacho kilikuwa kinahatarisha maisha ya Emile.
SASA ENDELEA....Yale maisha yalianza kumuweka Emile njia panga kwani alikuwa kwenye wakati mgumu wa kuamua. Emile alimuweka wazi mke wa bosi wake ya kwamba hakuwa tayari kushiriki mapenzi kwasababu alikuwa anamuheshimu sana Faraji kiemba....." Tafadhali Nadra naomba uniachie nikafanye kazi zilizonileta, kushiriki mapenzi na wewe sitaweza kwasababu mume wako(Faraji kiemba) akijua ataniua".....Aliongea Emile huku akijiondoa kutoka kwenye mikono ya Nadra Mrisho ambaye alikuwa amemkumbatia kwenye stoo ambayo Emile alikuwa anafanya usafi. Nadra mrisho alimuachia Emile kisha akaondoka kwa hasira kuelekea chumbani kwake, Emile alimuangalia kwa makini Nadra mrisho kwa nyuma jinsi alivyokuwa anatembea huku nyama za ziada zikijaribu kupishana. Kwa muonekano wa haraka haraka Nadra mrisho alikuwa ni mzuri kiasi, hakubarikiwa sana uzuri wa sura lakini rangi yake nyeupe mwilini ndio ilimfanya avutie pamoja na umbo lake namba nane ambalo alikuwa amejaaliwa, Emile ilibidi aendelee kufanya usafi huku akijaribu kutafakari jinsi ya kukwepa vishawishi vya mke wa bosi wake. Kile kitendo cha Emile kumkatalia penzi Nadra mrisho kilimuumiza sana Nadra akawa anakosa raha ndani ya nyumba, Ilifikia muda akawa anashindwa kula hata chakula kisa Emile. Faraji kiemba aliweza kuugundua utofauti wa mke wake ikabidi usiku mmoja wakiwa wawili kitandani amuhoji kitu kinachomsumbua...." mke wangu mbona siku hizi umebadilika, muda mwingi nakuona umechukia, hebu nieleze nini tatizo mke wangu".....Faraji kiemba aliongea huku akijaribu kumpapasa mke wake maeneo ya begani ili aeleze tatizo linalomsumbua, Nadra mrisho alikaa kimya kwa muda kisha akaanza kuongea huku akiwa na jazba moyoni mwake...."Haiwezekani faraji unifanyie hivi, wewe kila siku haunifikishi mwenzio, Yani kila siku unaniacha na hamu zangu, Roho inaniuma faraji kwa nini lakini haunitendei haki mume wangu".....Nadra mrisho alivyomaliza kuongea aligeukia upande wa pili kwa hasira, Faraji kiemba alijisikia vibaya kuambiwa vile na mke wake, Aliona kabisa anahadhilika mbele ya mke wake kwasababu kila siku alikuwa hamfikishi mpenzi wake huyo kwenye suala la kushiriki tendo, Faraji kiemba hakutaka kabisa ile aibu iendeleee kuwepo hivyo aliamua kwa hasira kushiriki tendo muda huo huo na mke wake ili amrizishe lakini hali ilikuwa ni yatofauti....." Ona sasa umenichafua tena, Yani moja tu umeshachoka, wewe mwanaume ni wa aina gani lakini".....Nadra mrisho aliongea kwa hasira huku akionesha kuchukizwa na Faraji kiemba ambaye alishindwa kabisa kurudia raundi ya pili. Hicho ndicho kilikuwa chanzo cha Nadra mrisho kumtaka kimapenzi Emile kwasababu alihisi kabisa Emile anaweza kumtimizia haja zake zote kwakuwa alikuwa ni kijana ambaye alionekana kuwa na nguvu nyingi. Kuna siku Faraji kiemba na mfanyakazi wa ndani waliondoka nyumbani, Kila mmoja alienda kwenye miangaiko yake hivyo Emile na Nadra mrisho walibaki nyumbani wao wawili, Nadra aliona iyo ndiyo siku sahihi yakumbana Emile hadi akubali kufanya naye mapenzi, Kitu ambacho Nadra mrisho alikuwa anakitaka kwa wakati huo ni kurizishwa kimapenzi na Emile kwasababu raha ya mapenzi hakuipata hata kidogo kutoka kwa Faraji mrisho, Siku iyo Emile alifanya usafi wa kila aina ambao alihitajika kuufanya kisha mwishoni aliamua kwenda kuoga ili ajiweke sawa, Kipindi anaenda kuoga alikuwa amevalia bukta ya mpira huku shingoni amezungushia taulo lake, Kumbe kwa muda huo Nadra mrisho alikuwa yupo dirishani akimpiga chabo Emile, Umbile la Emile lilionekana kumvutia sana Nadra, Emile alikuwa na urefu wa wastani huku kifua chake kikiwa kimejikata vilivyo kutokana na mizigo mizito ambayo alikuwa anaibeba kipindi cha nyumba ndani ya soko la kariakoo. Nadra aling'ata kucha za vidole vyake kwa matamanio huku akipandwa na wazimu wa mapenzi, Emile hakuwa anafahamu kama mke wa bosi wake(Nadra mrisho) alikuwa anampiga chabo hivyo alivyomaliza kuoga alipitiliza moja kwa moja hadi chumbani kwake ili abadilishe nguo. Kwa uharaka wa hali ya juu Nadra mrisho alivamia kwenye chumba cha Emile bila kugonga hodi huku akiwa amejifunga kanga peke yake bila kuvaa kitu chochote ndani yake, Emile alishtuka sana akaamua kujifunga taulo lake haraka huku akimsihi Nadra mrisho aondoke haraka ndani ya kile chumba kwasababu ilikuwa ni hatarishi kama Faraji kiemba akiwakuta....."Emile leo siondoki mpaka unipe, Ukikataa nakuchongea kwa bosi wako ulitaka kunibaka".....Aliongea Nadra mrisho maneno ambayo yalimvuruga Emile. Nadra mrisho alijisogeza kwa karibu zaidi akawa anaanza kumpapasa Emile maeneo ya kiuno, Emile hakuwa na lakufanya alikuwa anamuangalia mke wa bosi wake kitendo ambacho anataka kukifanya, Mwanzoni Emile alijikaza bila kupata hisia zozote lakini mwishoni uvumilivu ulianza kupungua kwani baadhi ya viungo vyake vilianza kutamani mambo matamu, Taulo la Emile lilianza kucheza cheza maeneo ya mbele, Lilikuwa linapanda juu na kushuka, Nadra mrisho baada ya kuona vile udenda wa uchu ulimtoka akatamani ajihudumie mapema, Tamaa za mapenzi zilianza kumuingia Emile lakini akajaribu kukumbuka maisha magumu aliyoyapitia, Alikumbuka pia ukarimu wa Faraji kiemba halafu leo hii atembee na mke wake(Nadra mrisho), Emile aliona sio haki kabisa kulitenda lile jambo, Aliamua kumsukuma kwa nyuma Nadra mrisho ambaye kwa muda huo alikuwa yupo mtupu kabisa kwani kanga yake alikuwa ameiangusha chini...."Siwezi kumsaliti bosi wangu, Naomba ujifunge kanga yako kisha utoke Nadra".....Emile aliongea kwa ukali kidogo huku akimsukuma Nadra mrisho ili atoke mule ndani ya chumba, Nadra hakuamini macho yake, Pamoja na kumuonesha Emile utupu wake lakini bado alishindwa kueleweka mbele ha Emile....." Emile naomba unisikilize kwa makini, kujirahisisha kwako haimaanishi mimi ni malaya hadi uuone mwili wangu na kuniacha na hamu zangu, Sasa mimi naondoka lakini kati yangu mimi na wewe tutajua nani mjanja, Hii nyumba utaiona chungu nakuambia, utakumbuka kwenu ulipotoka".....aliongea Nadra mrisho kwa hasira kisha akabamiza mlango kwa nguvu na kutoka ndani ya kile chumba. Nadra mrisho aliwaza kumfanyia Emile mambo mabaya sana kama njia sahihi ya kumlipiza.
Itaendelea....
Mambo yameanza kupamba moto ndani ya AFTER DEATH (BAADA YA KIFO)
Usikose muendelelzo