Notification texts go here Contact Us Buy Now!

AFTER DEATH (BAADA YA KIFO) SEHEMU YA 03

AFTER DEATH (BAADA YA KIFO)-03
MTUNZI-ANDREW SHADU
TELL-0677884981
EMAIL-andrewshadu44@gmail.com

ILIPOISHIA....
 Emile alifanikiwa kumfikisha yule msichana hadi stendi kisha akapewa elfu tatu yake, Kipindi anarudi kwenye chimbo lake sokoni, Emile alipishana na wanafunzi wa kike waliokuwa wamevalia unifomu za jangwani, Moyo wa Emile ulijawa na simanzi zito kwani alikumbuka kipindi alipokuwa anasoma, Hakuamini kabisa kama yeye ndiye aliyekuwa anaangaika na kazi za kubeba mizigo kule sokoni kariakoo. Emile alijifuta machozi akawa anatembea kwa unyonge mikono amejiwekea kwa nyuma huku akiamini kuna siku atafanikiwa na kuishi kama mfalme.

SASA ENDELEA....Emile alirudi hadi sehemu ambayo anapendaga kuyasubili malori ya kubebea mizigo akawa tayari kashajiweka sawa kwa ajili ya kulikimbilia lori ambalo litakuwa la kwanza kuingia. Kule sokoni kariakoo kulikuwa hakuna utaratibu maalumu wa kushusha mizigo kwa vijana hivyo mwenye nguvu ndiye alikuwa anawapiku wenzake, Kila kitu kiliendeshwa kiubabe ubabe, kama inavyojulikana kila sehemu huwa kuna wababe wanao ogopeka basi hivyo ndivyo ilivyokuwa hata kule sokoni kariakoo kwasababu kuna baadhi ya vijana walikuwa wanajikuta wababe kwa kuwaonea wenzao waliokuwa hawana nguvu, Emile alikuwa kwenye upande wa vijana wastarabu wasiokuwa na nguvu kwaiyo tenda zake za mizigo zilikuwa ni za tabu sana, kuna siku alikuwa anashindwa hata kuambulia shilingi mia moja kwasababu wababe wa kijiwe walikuwa wanachukua tenda zote, lakini ugumu wa maisha ndio ulimfanya Emile aendelee kuvumilia yale manyanyaso kutoka kwa baadhi ya vijana wenzake. Baada ya kubangaiza kule sokoni kwa miezi kadhaa hatimaye Emile alifanikiwa kupata kiasi kadhaa cha pesa ambacho hakikuwa kingi sana, Zilikuwa ni kama shilingi Elfu thelathini. Kwakuwa Kariakoo na Ulongoni ilikuwa siyo mbali sana, Emile aliamua kuwapelekea wazazi wake kiasi cha shilingi elfu ishirini kisha akawaaga na kurudi sokoni kuendelea na zile kazi ngumu za kushusha mizigo, Emile alitaka siku moja wazazi wake waje kuishi kitajili hivyo moyoni mwake alijiwekea ahadi ya siku moja kuja kuwafanyia jambo moja kubwa la kheri wazazi wake. Ukarimu wa Emile pale sokoni ulipelekea aweze kuzoeana na baba mmoja ambaye alikuwa anapenda kila mwisho wa wiki kuja pale sokoni kununua magunia kadhaa yaliyojaa mahitaji ya nyumbani, Emile ndiye alikuwa kijana ambaye alikuwa anapenda kumpakizia yale magunia yule baba ambaye kwa majina alijulikana kama Faraji kiemba mkazi wa Chang'ombe. Ilikuwa ni jioni moja tulivu ambayo lilikuwa limetanda wingu moja zito, Faraji kiemba alikuwa amewasili sokoni kununua mahitaji yake ya wiki nzima, Emile hakuwa mbali kwani naye alikuwa pembezoni mwa Faraji kiemba akimsaidia kupakia magunia ya vitu kwenye gari lake aina ya carry ndogo....."leo naona umeamua kuongeza mahitaji ya nyumbani".....Emile aliuliza huku akiwa anapakia gunia la vitunguu kwenye carry,...."Ah si unajua mama watoto huwa ananisumbua ndio maana nimeamua kuongeza mahitaji".....Fariji kiemba alimjibu Emile huku akitoa pochi yake na kuanza kumuhesabia kiasi cha fedha kama hubia ya kumlipa Emile. Emile aliipokea ile pesa lakini akaamua kuhoji kitu...."samahani bosi mbona leo umenipa pesa nyingi, si huwaga nakupakilia kwa elfu tano, naona umejisahau umenizidishia elfu kumi na tano".....Faraji alitabasamu kisha akamwambia Emile kuwa achukue pesa yote aliyompa...."Usijali kijana wewe ni mchapa kazi mkubwa hivyo iyo elfu ishirini yote ni yako nimekupa, Oh halafu nilitaka kusahamu kukuambia kuwa ninahitaji kijana wa kazi nyumbani kwangu wakunisaidia kazi zangu nyumbani".....Emile baada ya kusikia vile alitaka kuzimia kwasababu aliona kama malaika wa kumfungulia riziki zake amemjia, Aliona kabisa ile ilikuwa nafasi adimu kuwahi kuisikia masikioni mwake tangu alipojiingiza kwenye mambo ya kubeba mizigo....." Nipo tayari baba yangu, hata leo naomba nikaanze kazi, nitafanya kazi zote hata kulisha kuku kama unao nitawalisha".....Emile aliongea kwa unyenyekevu mkubwa huku akitaka kupiga magoti chini lakini Faraji kiemba alimuwahi na kumnyanyua juu kisha akamwambia aingie kwenye gari na kuanza safari kuelekea chang'ombe. Baada ya muda mchache Faraji na Emile walikuwa wamefika chang'ombe sehemu ambayo alikuwa anaishi Faraji kiemba.
-'-'-'-'-Faraji kiemba alikuwa anaishi na mke wake ambaye alikuwa anaitwa Nadra Mrisho kutoka Tanga pamoja na mfanyakazi wa ndani, Nyumba ya Faraji kiemba ilikuwa ni kubwa sana iliyozungushiwa wigo wa ukuta uliokuwa mpana. Faraji kiemba alikuwa ameajiliwa serikalini katika kitengo cha utalii hivyo alikuwa anapokea pesa nyingi sana kila ifikapo mwisho wa mwezi. Emile alipokelewa vizuri bila tatizo lolote kisha Faraji kiemba akamtambulisha siku iyo iyo kuwa ni mfanyakazi ambaye atasaidia kazi za nje ya nyumba. Emile alitokea kupendwa na nyumba nzima kwa uchapakazi wake mzuri wa kazi kwani alijituma kufanya kazi zote alizohitajika kuzifanya bila kuchoka, Alifyeka majani, Alichota maji, Alifagia mabanda ya kuku, Aliwarisha mbwa, Yali alifanya karibia kazi zote. Miezi mitatu ya mwanzo mambo yalienda sawa kwasababu Emile alikuwa analipwa kiasi cha shilingi laki tatu ambazo alinunua simu ya kawaida kisha akawanunulia na wazazi wake simu aina ya nokia, Alifanya vile ili apate urahisi wa kuwarushia wazazi wake pesa ambazo atakuwa analipwa ili ziwasaidie wazazi wake. Ndani ya iyo miezi mitatu Emile alikuwa ameshawatumia wazazi wake kiasi cha shilimgi laki nne na nusu kwani kila mwezi alikuwa anatuma nyumbani kwao nusu ya mshahara wake. Mwezi wa nne ulivyoingia mambo yakaanza kumuendea kombo Emile, Siyo kwamba Faraji kiemba hakumuhitaji bali ni mke wa Faraji kiemba ndiye alikuwa kikwazo, Nadra mrisho alianza kumtaka Emile kimapenzi huku akiahidi kumpatia pesa nyingi zaidi ya mshahara anaolipwa na Faraji kiemba. Nadra mrisho alianza kumletea Emile mitego ya kila aina ili ampate kimapenzi kitu ambacho kilikuwa kinahatarisha maisha ya Emile.

Itaendelea....
Emile kwenye mtihani mzito. Je ataweza kukwepa vishawishi vya Nadra mrisho au atashawishika?

Usikose muendelezo.

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.