Notification texts go here Contact Us Buy Now!

AFTER DEATH (BAADA YA KIFO) SEHEMU YA 02

AFTER DEATH (BAADA YA KIFO)-02
MTUNZI-ANDREW SHADU
TELL-0677884981
EMAIL-andrewshadu44@gmail.com

ILIPOISHIA....
Hatimaye siku pendwa ya kufanyika mitihani iliwadia Emile akiwa bado yupo kitandani hoi hajiwezi kwasababu ya homa kali. Kutokana na Sheria za mitihani ya mwisho ilibidi Emile afanye ile mitihani akiwa kitandani japo alikuwa hawezi hata kuandika, Alijitahidi kutaja majibu kwasababu kuna mtu alikuwa anamsomea swali kisha yeye anajibu huku akihisi maumivu makali sana, Polisi wakusimamia udanganyifu hakuwa mbali kwani alikuwa anamlinda Emile hadi siku ya mwisho ya mitihani. Wiki moja mbele baada ya ile mitihani kupita Emile alirejewa na afya yake upya, Emile alilia sana kwani alijua kabisa hawezi kuifaulu ile mitihani kutokana na jinsi alivyoifanya pindi alipokuwa anaumwa.

SASA ENDELEA....Wanafunzi wote waliomaliza kidato cha nne kwenye shule ya Tusiime walirudi majumbani kwao kuendelea na mambo mengine huku wakiwa wanasubili matokeo ya kujiunga na kidato cha tano. Emile alirudi moja kwa moja hadi maeneo ya Ulongoni ambapo alikuwa anaishi na wazazi wake wote wawili mzee Chande na mama monge. Maisha nyumbani kwa kina Emile yalikuwa ni ya shida sana kwasababu Jenkison(yule mzungu) hakuwa anawasaidia sana bali yeye alijipa jukumu la kumsomesha Emile peje yake ila Jukumu la kuwalea wazazi wa Emile hakujivika nalo hivyo wazazi wa Emile ilibidi wawe wanajikongoja kwa kubangaiza ili waweze kula....."mke wangu monge mbona maisha kwa upande wetu yamekuwa ya tabu hivi, Jenkison naye yupo kimya tu tangu Emile ampigie simu aturushie japo kahela kidogo tununulie matumizi hajamjibu".....Aliongea mzee chande ambaye alikuwa ameshikilia tama shavuni huku akiwa ameketi kwenye kiti kilichokuwa kimechakaa sana, Mama monge alikuwa kimya akimsikiliza mzee Chande kwa makini, Wazazi hao wawili hawakuwa na kazi ya maana ya kuwaingizia kipato kwasababu Mzee Chande alikuwa ni fundi viatu wakati mama Monge alikuwa ni mama anayejihusisha na mambo ya kuuza mboga mboga, Shughuri zao hizo zote kwa pamoja zilikuwa zinawaingizia pesa ndogo sana ambayo haikuweza kukidhi mahitaji yao ya kila siku. Emile alikuwa anawaza usiku na mchana ili siku moja aje kuwa mtu mashuhuri duniani lakini kila alipokuwa anakumbuka jinsi alivyofanya mitihani ya mwisho machozi yalikuwa yanamtililika kwa wingi ila aliamua kujikaza kiume huku akijaribu kuomba miujiza itendeke. Wahenga wakisema kitu basi lazima kitokee kwani ile kauli ya siku hazigandi ilijidhihilisha siku ambayo matokeo ya kidato cha nne yaliachiwa rasmi na wizara ya elimu, Matumbo ya wanafunzi wengi waliokuwa wamemaliza kidato cha nne yalikuwa yanawaka moto, Emile hakuwa na Simu ya kisasa ya kumuwezesha kupata matokeo hivyo aliamua kumuomba baba yake shilingi mia tano ambayo aliitumia kwenda kulipia ili aangalie matokea yake kwenye moja ya internet cafe ambayo ilikuwa haipo mbali sana na sehemu ambayo alikuwa anaishi, Emile alivyoangalia matokeo yake hakuweza kuamini macho yake hata kidogo, Alijaribu kurudia mara mbili mbili ili kuhakikisha lakini kitu alichokiona kilikuwa sahihi kabisa, Matokeo ambayo aliyashuhudia yalikuwa yamejazwa kwake hivyo hakuwa na budi kuyapokea japo upokeaji wake ulikuwa ni watofauti....." Mimi kweli ndio nimepata hivi, kwanini lakini imekuwa hivi!!".....Emile aliongea peke yake kwa mshituko kisha akaanguka chini na kuzimia, Ghafla taharuki iliibuka kwenye ile internet cafe ambayo Emile alikuwa amezimia, Watu walimtoa Emile nje wakaanza kumpepea huku wakimwagia maji ili apate hewa, Baada ya muda mfupi fahamu zilimjia tena Emile akazinduka na kuanza kukimbia huku akilia kuelekea kwao, Njia nzima Emile alikuwa analia sana hadi watu wakawa wanamuonea huruma. Mzee Chande ilibidi amtulize Emile kwa kumfariji ili asijisike vibaya, Ilikuwa ni ngumu kuamini lakini Emile alikuwa amefeli kwa kupata alama sifuri. Jenkison alisitisha huduma zote kwa Emile kwani aliona haina haja ya kuendeleza huduma za kumsomesha mtu ambaye amefeli. Maisha kwa upande wa Emile yalizidi kuwa magumu sana kwani kuna baadhi ya siku walikuwa wanashinda njaa siku nzima, Umasikini ulionekana kuimaliza familia ya Emile hivyo Emile alipanga kuondoka kwenda mbali kutafuta maisha....." Mama na Baba yangu nawaomba mniruhusu nikatafute maisha ili nije kuwasaidia, kama mnavyoona maisha ya apa nyumbani yalivyo magumu, mimi naomba mniruhusu nikatafute maisha tu wazazi wangu nawaahidi nitajitahidi kujituma".....Emile aliongea akiwaomba wazazi wake wampe baraka za kuondoka pale nyumbani na kwenda kutafuta maisha kwani ndoto za kuitegemea shule ili imsaidie zilikuwa zimezimika kama mshumaa. Emile alipewa baraka zote na wazazi wake aingie mtaani akapambane kiume ili aje kuikomboa familia. Emile alianza safari ya kuondoka kwao huku kichwani akiwa na mawazo mengi sana. Emile aliingia mtaani na kuanza kufanya kazi za kushusha mizigo kwenye malori makubwa yaliyokuwa yanaleta mizigo kwenye soko la kariakoo, Mara nyingi Emile alikuwa analala mule mule sokoni, alitamani kumpigia Simu rafiki yake mpendwa Fred lakini kwa wakati huo ilikuwa ni vigumu kwasababu simu yake aina ya bontel alikuwa tayari ameshaiuza. Emile aliifanya ile kazi ya kushusha mizigo sokoni kwa bidiii huku akiamini itamsaidia lakini bado hali ilikuwa ngumu kwasababu kwanza ile kazi ilikuwa ni nzito, Kila siku alikuwa anakumbana na changamoto mbali mbali hadi kuna muda alikuwa anakaa pembeni peke yake na kuanza kulia, Japo alikuwa mwanaume lakini chozi lilikuwa linamdondoka, Aliwaza kuiba lakini vifo vya kuchomwa moto kwa baadhi ya wezi ambao aliwashuhudia vilimuogopesha. Kuna siku Emile akiwa sokoni kariakoo akisubilia lori la mizigo alipata tenda la kumbebea msichana mmoja mizigo yake hadi ilipo stendi ya magari ya temeke...." Dada yangu nitakufanyia Elfu tatu kwasababu una mizigo miwili".... Emile aliongea huku akijitwishwa kichwani viroba viwili vya viazi tayari kwa safari ya kuelekea stendi ya temeke. Emile alifanikiwa kumfikisha yule msichana hadi stendi kisha akapewa elfu tatu yake, Kipindi anarudi kwenye chimbo lake sokoni, Emile alipishana na wanafunzi wa kike waliokuwa wamevalia unifomu za jangwani, Moyo wa Emile ulijawa na simanzi zito kwani alikumbuka kipindi alipokuwa anasoma, Hakuamini kabisa kama yeye ndiye aliyekuwa anaangaika na kazi za kubeba mizigo kule sokoni kariakoo. Emile alijifuta machozi akawa anatembea kwa unyonge mikono amejiwekea kwa nyuma huku akiamini kuna siku atafanikiwa na kuishi kama mfalme.

Itaendelea....
Nini hatima ya Emile kwenye maisha yake. Je, kwa upande wa Fred mambo yapo vipi. Ili kufahamu yote hayo tukutane sehemu inayofata.

Usikose muendelezo.

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.