Notification texts go here Contact Us Buy Now!

I'M NOT A BOY (Mimi sio mwanaume) SEHEMU YA 01


I'M NOT A BOY 
                   (Mimi sio mwanaume)
SIMULIZI: I'M NOT A BOY 
                   (Mimi sio mwanaume) 
MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 01

UTANGULIZI: Kuna mwana mama alikuwa anapatikana kwa jina la sofia alikuwa anaishi Zanzibar, mwana mama huyo aliishi na mumewe miaka 5 bila kupata mtoto, mumewe alikuwa amezaliwa pekee yake wa kiume kwenye familia ya baba yake aliekuwa anaitwa mutrah,mzee mutrah alimpata mtoto wa kiume aitwaye Abdullah ambae ni mme wa Sofia kwa bi Rukia ambae ni mwanamke aliekuja kuolewa kwa mzee mutrah akiwa na watoto wa nne wa kike baada ya kuolewa kwa mutrah akapata mtoto Abdullah. Baada ya miaka kadhaa wazazi wote wawili wa Abdullah walifariki na kumuachie urithi wa Mali zote kulingana yeye ndie muhusika. 
 Mutrah alipofariki akaacha amemrithisha Mali zote mtoto huyo wa kiume(kampuni,nyumba ya kifahari pamoja na magari), ko sofia kutokuzaa kwake ilimpelekea familia nzima kufurahi maana waliamini urithi utabaki kwao maana miongoni mwa mawifi zake walikuwepo baadhi wana watoto wa kiume. 

SONGA NAYO! 

Siku moja mwana mama Sofia alikaa kwenye msala huku akiomba Dua kwa sauti ya chini na akitokwa na machozi: ehh! Mola wangu! Nisaidia nahitaji mtoto, nahitaji kumuona Mme wangu akicheka, mtihani huu umekuwa mgumu kwangu siuwezi. 

Kumbe mda huo mmewe alikuwa anamsikiliza kwa umakini, Sofia alipomaliza mmewe alimfuata pale alipo na kumkumbatia. 
Sofia aligeuka kumwangalia mmewe na kusema kwa uchungu: roho inaniuma Mme wangu siwezi kukuzalia Mimi, naomba ntakachokuambia usikatae. 

Mme: nakusikiliza wewe tu mke wangu. 

Sofia: naomba umtafute mke umuowe aje kuwa bi mdogo. 

Mme alishtuka Sana na kusema: mbona umekata tamaa mapema lakini? 

Sofia: miaka tano sasa Mme wangu bila kupata mtoto! haya yote nayafanya kutokana na mapenzi ya dhati nilionayo juu yako, naomba usiwe mbishi fanya nililokuambia ili unifurahishe na Mimi pia. 

Mme alionekana kutokufurahia alakini kwasababu ameombwa na mkewe hakuwa mgumu walikubaliana hivo. 

Baada ya miezi mi tano tayari bi mdogo kashaletwa, mda mdogo akawa amenasa ujauzito cha ajabu na kushangaza mwana mama Sofia nae alikuwa amebeba ujauzito, bi mdogo stori zote ni yeye atakuwa mrithi ko alikuwa anadeka kupita maelezo. 

Siku moja Sofia na hafsa ambae ni bi mdogo walikuwa wamekaa huku wakipiga stori. 

Sofia: umekuwa mzaifu Sana inaonekana utajifungua mtoto wa kiume. 

Hafsa: yaaani Mimi ndo Mimi kwenye hii nyumba, unajua nikijifungua mtoto wa kiume hahemi mtu hapa!. 

Sofia akacheka na kusema: unanifurahishaga Sana ujuwe! Tuachane na hayo umeshaoga. 

Hafsa: naskia uvivu wa kunyanyuka. 

Sofia: a a a a! Acha hivo nyanyuka nenda uoge mtoto apate kupumua swahiba. 

Hafsa: skia! Nimepita kando hivi nikaskia wii mkubwa na mama Abu wapo wananizungumzia, eti Oooo ninajidai, ooo sipendi kufanya kazi, Oooo nikijifungua mtoto wa kike ntaumbuka.

Sofia: hhhhhhh ko ndo ukamaindi? Ila usijali wewe usifanye kazi ntafanya Mimi japo kuwa hata Mimi mjamzito Ila ntajikaza sawa, na kingine nakushukuru Sana maana wewe ndo uliniletea baraka mpaka nikanasa ujauzito. 

Hafsa: unavituko kweli Ila wewe usijifunguwe wa kiume bhana. 

Sofia: hhhhhhh kwanza mi nataka wa kike ili nimfundishe dini vizuri mi naona wivu nikiona tutoto twa kike twa wenzangu tukienda madrasa tumejistili yaani nadata. 

Story ziliendelea. 

Baada ya miezi 6 kila mmoja mimba yake ilikuwa inakaribia kujifungua maana miezi Tisa toka wanase ujauzito. 

Kila siku walikua wakiumia tumbo, Mara watapike vitu vyeusi, Mara kulazwa mpaka ikiwatia hofu familia nzima. 
Bwana Abdullah alipoona hizo dalili aliogopa Sana akagundua kuna watu wanamchezea kamchezo ndipo akawasiliana na mganga wake anaetibu kupitia dawa za kiasili yupo arusha vijijini ili aweze kumsaidia, jibu lililokuja ni yeye kuwaruhusu waende arusha. 

Abdullah aliwaeleza wake zake kwa usalama zaidi waende arusha, hawakuwa wabishi walikubaliana hivo, Abdullah aliwataka radhi kutokana yeye anakazi Kenya inatakiwa akaifuatilie kenya ili kupata kidogo atakachowasaidiza kwa siku hizo za uzazi. 
Kila mmoja alikubali Ila wakamuomba asiwasahau. 

Baada ya siku chache safari ya kuelekea arusha ilianza manshallah wakafika salama kwa mzee huyo aliekuwa akiishi peke yake kwenye msitu mkubwa. 

Baada ya siku chache wote walijifungua, Sofia alijifungua mtoto wa kike ambae ni mimi, hafsa nae akajifungua mtoto wa kiume. 
Kila mmoja alikuwa na raha maana Allah aliwasikiliza kweli. 

Baada ya siku mbili, walijaribu kuwatafuta mjini zanzibar ili kuwapa taarifa ila ikashindikana kutokana mtandao ulikuwa ni mbaya. 

Ndipo Sofia na hafsa wakatulia wakimsubiri mganga aende mjini arusha awapigie awape taarifa kuwa wamejifungua salama. 

Siku moja wanawake wale walikuwa wamekaa chini huku wakipiga story. 

Sofia: siamini macho yangu. 

Neno hilo alilizungumza huku akiniangalia usoni. 

Hafsa: mwenyezimungu ameskia kilio changu. 

Sofia: mwanangu kwa kuwa nampenda Sana nampanga jina la aisha. 

Hafsa: hhhhhhh mbona jina lakishamba,kila ukipita Aisha duh! kuna majina yanaboa kweli,nami mwanangu jembe nampanga jina la Babu yake mutrah ili niwakomowe zaidi na atakuja kuwafukuzeni nyooote.
 
Sofia: nijambo nzuri ila na Mimi atanifukuza?. 

Hafsa: ikibidi. 

Sofia: acha utani bhana. 

Walifurahia hivo. 

Baada ya siku tano mtoto wa mamdogo ambae ni mutrah aliugua Sana bila kukawa akapoteza maisha maskini ya mungu, hakika ilikuwa ni pigo kubwa upande wa mamdogo hafsa alilia mno mpaka akatamani ajiuwe tu atoke dunia. 

Mama alimpoza kwa kutumia kauli nzuri: hafsa usiongee hivo yote ni matakwa ya mungu wewe unabahati na utapata mtoto mwengine maana Allah anasema subira ni nusu ya dini, acha kulia jikaze. 

Hafsa akamsukuma pembeni na kusema huku akiwa amekunja uso: unaonge kitu gani? Au wewe ni kama Nani unaongea hivo! Niache nilie naumia huyu ni mwanangu ujuwe.

Sofia: sio mwanao peke yako hata Mimi ni mama yake hafsa muombe mola wako atakujalia mtoto mwingine tena bora kama huyu. 

Hafsa: niache, niacheeeee. 

Baada ya siku chache, wivu za kishetani ziliojaa tamaa na chuki zikamuingia hafsa, akatoka hapo na kuelekea kwa mganga huyo anakofanyia kazi, alipofika alimsalimu na kumuomba aongee nae maneno machache, mganga hakua mgumu akakubali. 

Hafsa: nimekuja kukuomba kitu kimoja, naomba usikatae na usisite tafadhali muuwe Sofia ambae ni mke mwenzangu kwa gharama yoyote ile. 

Mganga alishtuka mno na kumjibu:........!!!! 

   Kipi kitatokea! Usikose sehemu ya pili
Pia like yako na comment yako nimuhimu Sana kwangu, pia nikukumbushe usisahau ku share ili wengine wajifunze kupitia hii simulizi. 

       ASANTE SANA. 

 

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.