(Mmarekani mweusi)
Mtunzi:Nelson Kimoyi
Sehemu ya 33
#Endelea__nayooo==>>Alisema mtu huyo huku akielekea usawa wa Generql Brown....
Hakufika alidhibitiwa na maaskari Wqliokuwa nyumq yake
"tulia ®ocky usiwe na papara"
Alisema yule msichana aliyekuwa amefunganishwa mkono pamoja na Rocky
"Lissa huyu ni wakufa tu Astahili kuishi"
Oooh tumepata kujua kumbe ni Lissa pamoja na Rocky....
Walichukuliwa wakapandishwa ndani ya ndege General Brown alipandishwa ndege tofauti........................
Safari sasa ilianza helcopta zile za kijeshi zilichana anga kwa mbwembwe......
Hatimaye masaa yalisonga na sasa helcopta zile ziliweza kutua katika kambi ya kijeshi ya
J.W.TZ ipatikanayo Gongolamboto Dar es salaam......
MP (militaly police) walizisogelea helcopta zile kwa umakini wa hali ya juu baadhi wakiwa na silaha nzito za kivita huku wengine wakiwa na pingu moja kwa moja wakawafuata watuhumiwa walioweza kuletwa.......
General Brown alifungwa pingu huku
Rocky na Lissa walishushwa na kupelekwa chumbq tofauti na Brown.......
*****Ofsin mwa Waziri wa ulinzi*****
"inatakiwa huyu general wa marekani afungwe maana haiwezekani aje kutuspy tena taarifa zake zisisambae"
Yalikuwa ni maneno ya hasira kutoka kwa waziri wa ulinzi
"sawa mheshimiwa na vipi kuhusu hawa wengine?"
Aliuliza Laizer akimaanisha Rocky na Lissa wapewe hukumu gani
"oooh kuhusu hao wapelekwe kwenye ofisi ya ubalozi wa Marekani ili wasafirishwe kurudi kwao sioni kosa zaidi naona kwa huyu general"
Yalikuwa ni maneno ya faraja kwa Laizer maana hata yeye hakutaka Rocky na Lissa wafungwe....
Ilikuwa ni siku mpya siku ambayo ilikuwa ni simanzi upande wa General Brown baada ya kusimamishwa kizimbani na kuhukumiwa kifungo cha maisha kutokana na na upelelezi uliofanywa na Laizer na kugundulika kuwa amemuua bwana Jamali.....
Rocky nq Lissa sasa walikuwa huru ni Laizer ndiye aliyechukua jukumu la kuwapeleka ubalozini hilo halikuwa tatizo ukitegemea Laizer alikuwa akijulikana vuzuri saana
"sawasawa kesho mujiandae kuelekea
America tena kutokana na bwana Laizer kuniambia historia zenu nimewapangia mkaishi Ontario itakuwa salama kwenu"
Aliongea balozi wa Marekani kwa kiswahili fasaha kabisa.....
Laizer alikuwa akitabasamu tu mpaka muda wanaondoka
"thanks Laijer"shukrani Laijer"
Alisema Lissa kwa kusoe jina la Laizer wote walicheka tu kwa furaha
"msijali ndugu zangu leo twendeni leo mkapumzike kwangu ila kabla ya yote twendeni shopping"
Wotee wakaelekea katika gari la Laizer wqkapanda na kuondoka kuelekea katika duka la nguo na wakafanya manunuzi yao.kisha wakarudi nyumbani kwa Laizer......
Asubuhi imekucha na makucha yake Rocky na Lissa walikwisha jiandaa kwaajili ya safari yao ya kuelekea U.S.A Laizer hakuwa nyuma kuwasindikiza..
Aliwasindikiza mpaka uwanja wa ndege.
Rocky na Lissa ni kama walikuwa ndotoni maana hawakuamini kabisa
"mr Laizer nitakukumbuka kaka daima na milele nitarudi tena Tanzania kuja kukuona tuombeane uzima"
Alisema Rocky
"usijali Rocky tupo pamoja"
Laizer alimjibu Rocky
"hata mimi nitakukumbuka Laizer nitarudi tena pamoja na Rocky"
Lissa naye alimjibu Laizer huku akimkumbatia wakaw wanaagana sasa baada ya kusikia sauti ya mdada mrembo iliyokuwa ikiwataarifu kuwa ndege itaondoka muda si mrefu...
Rocky pqmoja na Lissa walielekea ndani ya ndege wote kwa pamoja walipofika karibu na mlango wa ndege waligeuka nyuma wakampungia Laizer mkono naye Laizer alikuwa bado akiwatazama akawapungia pia mkono.
****MWISHOOOOOOOOOOOOOOOOOO****