(Mmarekani mweusi)
Mtunzi:Nelson Kimoyi
Sehemu ya 32
#Endelea___nayooo====>Laizer alisogea mpaka kitanda alichoweza kumuona mtu huyo ambaye ni mzungu aliyepata ajali
"General Brown hahaahahaaa you can't escape"general Brown huwezi kutoroka"
Alsema Laizer huku akimtazama Brown ambaye alikuwa akiugulia maumivu kitandani pale.......................
Alitoa pingu kiunoni akamuunganisha Brown pamoja na kitanda........
Dokta aliyekuwa akitoa huduma kwa Brown ndo alikuwa akiingia katika chumba cha Brown na kumkuta Laizer akimalizia kumfunga pingu Brown...........
Dokta huyo qlipotaka kugomba Laizer akatoa kitambulisho na kumuonyeshea dokta
"mtu huyu yupo chini ya ulinzi kwahiyo muhudumie vizuri ili apone akapande kizimbani"
"okay sawa"
Alijibu dokta baada ya kuona kitambulisho chenye jinq ambalo halikuwa geni kwake........
Laizer alipiga simu kituo cha polisi na maafande wqwil wakaweza kutimu hospitali hapo kwaajili ya ulinzi wa kumlinda Brown...
Simu ya Laizer iliita alipotazama kwenye kioo alipata kuona mpigaji ni O.C.D
"haloo O.C.D nakusililiza"
"ndiyo Laizer nimetokea sehemu ya tukio nimepata kuchukua begi pamoja na briwfcase kwahiyo nakusubiri uje ili nijue kuna nini ndani yake"
"okay im coming"
Laizer hakutaka kuchelewa aliondoka na kuelekea kituoni.......
Alipofika alivaa miwani yake kisha akascan briefcase majibu yakatokea kuwa hakuna kitu cha kuhatarisha maisha yao.....
Akafungua briefcase hiyo.akapata kuona laptop pamoja na bastol@
Hakutaka kuwaza sana aliichukua laptop akaichomeka kwenye umeme kisha akaiwasha ikawaka huku ikionyesha neno lililosomeka "put paswoord"
******Kilichojiri hospital******
General Brown alikuwa akitafakari.namna ya kutoroka hospital hakuwa na mawazo mengine zaidi ya hayo........
Upande wa Laizer alifungua begi lile la nguo akapata kuona sindano pamoja na vichupa viwili vidogo huku kijimfuko cha vidonge kikiwemo pia alionekana kushtuka kidogo
"vipi Laizer kuna tatizo??????"
Aliuliza O.C.D Bihamunuro Huku na yeye akisogea karibu zaidi....
"hapa kuna chupa ndogo ya spray ambayo hutumika kumtia mtu usingizi halafu hii chupa ingine ni ya sindano ya sumu ya kuulia wanyama wakali siku zote hutumika na na wawindaji haramu ukichomwa kwenye mwili hata uwahishwe vipi hospital we ni wakufa tu
Halafu hivi vidonge vinaitwa zosleep vinatumika kupoteza usingizi hata kama dawa ya usingizi imepulizwa pembeni yako hauwezi kulala"
Alimaliza kwa kusema Laizer......
Bihamunuro alikiri kweli Laizer hqkuwa mzembe shuleni........
Laizer alitafakari kwa dakika kadhaa
"hivi ulipata taarifa za bwana Jamali?"
Aliuiza Laizer huku akitazama baadhi ya vitu katika lile begi
"ndiyo nilipata kwani wachunguzi wamedai kuwa mwili wa bwana Jamali uliuwawa kwa kuchomwa na sindano ya sumu na hawajajua ni sumu gani"
"Oooooooh okay je nikikuambia qliyemuua bwana Jamali ni huyu mzungu utaamini??"
Aliuliza Laizer sasq akiwa anamuonyesha pasport ya General Brown
O.C.D Bihamunuro.............
O.CD Bihamunuro alijikuta akishangaa tu pasport iliyokuwa na jina lililosomeka Brown Karly.........
"ndio makubaliana na hilo kabisa tena asilimia miamoja"
Laizer alitabasamu tu kisha qkasimama
"twende kituo hospitali"
Alisema Laizer kisha O.C.D Bihamunuro akasimama wote kwa pamoja wakaufuata mlango.......
Walitoka nje wakapanda gari lao na kuondoka mahali hapo.......
******Hospital Ya Igunga******
General Brown sasa alikuwa kaweza kukaa mwenyewe katika kitanda akitafakari vitu vingi.........
Alishangaa kuona watu wawili wakiingia huku mmoja wa watu hao akionekana ni mtu mwenye wazifa mkubwa serikalini alikuwa amechafukwa na nyota mabegani mwake hakuwa mwingine alikuwa ni O.C.D Bihamunuro akiwa pamoja na Laizer........
"vipi general hii ndo Tanzania huwezi toroka kirahisi"
Alisema O.C.D Bihamunuro tena aliongea kwa matambo.........
******Yamekuwa Makubwa******
Taarifa zilifika mpaka jijini Dar es Salaam katika ofisi ya Mh Waziri wa ulinzi Johson Mazinge......
Ni simu ilisikika tu ikiita katika meza ya Mh waziri
" haloo???"
"ndiyo Mh waziri Laizer naongea hapa"
"ooooh Laizer sawa sawa nini kimejiri Igunga umebahatika kujua nini cha maana katika hilo tukio la nyumba kuchomwa na moto??"
"ndiyo mkuu ni vitu vingi tu lakini kikubwa ni kwamba tumeweza kumnasa General wa wanajeshi wa Marekani ndo aliyesababisha mpango mzima wa kuwapa kazi majmbazi kwenda kuchoma nyumba hiyo lakini pia aliyekuwa akimiliki nyumba hiyo hakuwa mtanzania naye alikuwa ni Mwanajeshi wa Marekani ambaye alishiriki kwenye mauaji ya Rais wa Marekani Mh Markdaniel Damiano kwahiyo hapo ukiunganisha tukio la nyumba kuchomwa na moto ni kuwa huyu General alitaka kupoteza ushahidi kwa sababu ni yeye ndiye aliyekuwa nyuma ya pazia na ili asijulikane ilitakiwa afanye mauaji lakini pia kuna binti yule wa Billionear Jensen Brown naye pia tunaye vipi unamjua huyo general wa Marekani????"
Alimaliza Laizer kwa kumuuliza Mh Johnson huku akitaraji kupata jibu la ndiyo lakini haikuwa hivyo...
"hapana simfahamu hata"
"ooooh mheshiwa hukumbuki mwezi uliopita mlimkaribisha mwekezaji wa kizungu aliyewekeza katika mradi wa kuku wa kisasa??"
"oooh sawa nimemkumbuka anaitwa Brown Karly"
"basi ndo huyo ambaye kwa sasa ni mtuhumiwa wa mauaji ya tajiri maarufu yule bwana Jamali Swalehe"
"whaaat mleteni huku kumbe alikuwa anaichora Tanzania nitaagiza helcopta mbili uje nao wote huku Dar es salaqm"
Alimaliza kw a kusema Mh Johnson.........
Laizer alimwambia O.C.D Bihamunuro kwa kila walichoongea na Mh Waziri wa ulinzi
******Gumzo Yasambaa wilaya ya Igunga******
Kila kona ilikuw ni story inayohusiana na wqmarekani waliokuwa wakiishi Tanzania kinyemela huku General Brown akichukuliwa kama spy aliyekuwa akiispy nchi ya Tanzania
"tokea lini Mmarekani akawekeza kitu katika nchi ya giza kama Tanzania ukimuona kawekeza ujue kuna kitu chake anakitafuta si unaona huyo kamuua Bwana Jamali halafu akataka kujiondokea"
Ualikuwa maneno ya vijana katika kijiwe mojawapo maarufu sqna Wilayani Igunga......
*****Ujio wa Helcopta******
Ulizidi kuwabungaisha zaidi wana Igunga ujio wa Helcopta mbili za kijeshi walishuka wanajeshi wakiwa na bunduki zao mikononi......
Laizer pamoja na O.C.D Bihamunuro walikuwa katika gari dogo lenye vioo vya tinted helcopta zilivyotua katika uwanja wa mpira wa miguu upatikanao katika Wilaya ya Igunga gari lile dogo liliendeshwa mpaka jirani na helcopta kumbe kulikuwa na gari jingine nalo lilifanya kama gari la mwanzo lilivyofanya......
Gari lile la kwanza likafunguliwa mlango akatoka Laizer na O.C.D Bihamunuro huku akifuatia na mzungu aliyefungwa na pingu mikononi mwake...
Wananchi walikuwa wakishangaa tu tena walikuwa wngi saana....
Gari lile la pili nalo lilifunguliwa akatoka askari mmoja na watu wawili wqliokuwa wamefunganishwa mikono yao kwa pingu mmoja akiwa ni msichana na mwingine akiwa ni mwanqume wa kati.....
Wqlipomalizikia kutoka mpaka nje yule mwanaume wa kati ni kama alijikuta akichanganyikiwa ghafla baada ya kumuona mtu ambaye hakuwa mgeni machoni pake
"lazimaaa nikuuuwe general"
Alisema maneno hayo huku akikimbilia usawa wa mtu huyo........
ITAENDELEAAAAAAA...............
Marafiki zqngu ni kuwa story yetu tutaisoma.mpaka mwisho lile swala langu la kwenda shule limebuma ni changamoto tu za maisha so nipo nanyi mpaka mwakani...
Wale wa story ya mimi na wewe tukutane baadae