Notification texts go here Contact Us Buy Now!

BLACK AMERICA SEHEMU YA 31

BLACK AMERICA
(Mmarekani mweusi)
Mtunzi:Nelson Kimoyi
Sehemu ya 31
#Endele__nayooo====>sasa Rocky alishajua kuwa mbele yake alikuwa akitazamana na mtu ambaye hakuwa wa kawaida wakati anawaza hayo akagutuliwa na sauti ya Laizer
"nambie bwana Rocky mbona upo kimya nikuelewaje sasa ukweli ndo kitu kitakacho kuweka huru ndugu yangu ngoja nikuache wewe nigeukie kwa mwenzio "
Alisema Laizer sasa alikuwa amebadilika na kuwa na hasira
"afandeeee??"
Aliita Laizer naye afandee akawa ameitikia wito......
"chukua huyu peleka ndanii"
Naye afande akatii kama alivyoambiwa akasogea mahali alipo Rocky ambaye kwa jina jingine anaiitwa Masanja......
"nasema ukweli wote mkuu"
"okay afande we kaendelee na shughuli zako."
Rocky alianza kuelezea mambo yote jinsi yalivyo maisha aliyopitia....
Hakusahau pia kueleza jinsi anavyoqndamwa na General Brown hakusahau pia kuhusiana na swala la kupachikwa cheap ya kuonyesha ramani katika mwili wake upande wa moyo.......
Na ndo kitu ambacho General Brown anajiaminisha kwa sababu akimtafuta katika programe yake anampata pasipo tatizo.......
"kwahiyo hata kama yupo marekani au nchi yeyote anakuona!!!!??"
Aliuliz Laizer huku akishangaa technologia iliyotumika katika mwili wa Rocky....
Naye Rocky alimjibu na kumwambia tena vithibitisho alikuw navyo Laizer alipoomba.....
Rocky akamwambia kuwa 
"katika purukushani ya kutukamata tuliacha kila kitu huko porini"
Alisema Rocky....
Laizer hakuwa na jinsi kwa kuwa alitaka vithibisho ili kukamilisha upelelezi wake aliwaita wale maafande alioshirikiana nao katika mpango huo wa kuwatia mbaroni Rocky pqmoja na Lissa....
"nimewaita najua wote mnashangaa ni nini nimewaitia ni kwamba katika kukamata watuhumiwa hawa kuna vithibitisho tumesahau kwahiyo naomba mrudi tena kwenye hema lile muweze kuchukua kila kitu na muweze kuja nacho mahali hapa"
Maasikari wale watano walichukua gari wakaweza kuelekea porini huko.......
Ilikuwa ni zamu ya Lissa kuhojiwa naye hakuwa mbishi alieleza kila kinchomuhusu alieleza pia uhusiano wake yeye na General Brown....
"mmmh mjue mnanichanganya kidogo sasa wewe na Rocky mlielewana kuwa mkutane Tanzania katika mkoa wa Tabora au!!?"
Aliuliza Laizer huku akimtazama Lissa kwa.macho ya kipelelezi 
"hapana mimi na Rocky tumekutana kama bahati tu sikuwa namjaua kabla ila alivyonipa historia yake ndipo nilipoweza kumjua kuwa ni mdungaji wa jeshi la U.S.A nami nikampa historia yangu na ndo mpaka leo nipo nae"

Alimaliza Lissa.......
******Ajali upande wa General Brown******
General Brown alikimbiza gari kwa kasi tena kwa furaha tele akiwahi Mwanza na sasa alikuwa Shelui akianza kuitafuta Igunga akiwa katika mwendo kasi alikuwa akipishana na magari makubwa.....
Hakika madereva wa gari kubwa walipatwa na mstaajabiko ila watafanya nini kama General Brown hakutaka kuzingatia usalama wake baada ya masaa mawili alianza kuiona Igunga kwa mbalii............................
******Kituo cha police Igunga******
Maasikari waliokuwa wamekwenda porini sasa walkuwa wamerudi na vithibitisho vyote na kumkabidhi Laizer ambaye alivitizama tu vitu hivyo lakini katika tazamaza tazama alieza kuona memory card.......
Aliichukua na kuiweka ndani ya adapter ama card reader kama wengine wajuavyo..........
Alipoweka akachomeka ndani ya pc/personal computer aliyokuwa nayo kando ya meza aliweza kufungua baadhi ya mafaili akakuta picha nyingii ambazo zilionyesha mfumo wa moyo lakini pia aliweza kuona video ambayo na yenyewe haikuwa na tofauti na picha,,,,,
O.C.D Bihamunuro yeye alikuwa mtazamaji tu........
Wakati ambao Laizer anatazamana na tarakishi yake simu ya O.C.D ikaita naye akapokea 
"ndiyooo"
Aliitikia O.C.D katika simu
"kuna ajali hapa Makomero ilitokea jana ni ajali iliyosababishwa na gari ndogo ambalo lilikuwa linatokea Singida na lilikuwa likiongozwa na Mzungu kwa sasa yupo Igunga Hospital lakini hakuna trafiki hata mmoja aliyefika"
"okay tunakuja"
Alisema O.C.D kisha akakta simu..........
Alimpasha Laizer habari hiyo....
Laizer alihisi kitu ikabidi wagawane majukumu yeye aende hospital na O.C.D aende sehemu ya tukio....
******Mambo yamekuwa mambo******
O.C.D Bihamunuro alifika Makomero kijiji ambacho hapakuwa mbali sana na wilaya ya Igunga.....
Alikuta wanakijij wazarendo wakiwa wamelilinda gari lililopata ajali...........
Alichungulia kupitia dirishani akaweza kuona begi la wastani halikuwa kubwa wala dogo.....
Wanakijiji hawakuwa mbali kuangalia kila kinachoendelea...............
O.C.D alimuita askari mmoja....
"prosper"
"yes sir"
"naomba uingie ndani ya gari kwa tahadhari kubwa na uchukue kila kinachowezekana kuubebwa"

Alisema O.C.D Bihamunuro naye afande yule ajulikanaye kwa jina la Prosper akafanya kama mkuu wake alivyomuagiza.......
Alitoa briefcase pamoja na begi.....
Upande wa Laizer alipofika hospital aliangaza macho yake kila kitanda kilichopatikania katika ward ya hospital hiyo ghafla aliweza kumuonaa akajikuta akisogelea kitanda hicho alichomuona......
TUKUTANE SEHEMU IJAYO...........

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.