Notification texts go here Contact Us Buy Now!

BLACK AMERICA SEHEMU YA 30

BLACK AMERICA
(Mmarekani mweusi)
Mtunzi:Nelson Kimoyi
Sehemu ya 30
#Endelea___nayooo>>>>General Brown alitoka katika chumba chake na moja kwa moja akaelekea katika chumba cha bwana Jamali akagonga mlango ukafunguliwa.....
Bwana Jamali alishangaa ujio wa General Brown ujio wa ghafla...
"vipi Brown mbona wahudumu hawajanipigia simu"
Aliongea Jamali huku akianza kuwana hofu juu ya General Brown maana haikuwa kawaida kwa hoteli kubwa kumruhusu mtu aonane na mteja kiholela pasipokuwa ruhusa ya mteja 
"inaonekana simu zao za mezani zina matatizo kwahiyo nimekuja na mdada wa mapokezi akaniacha kisha yeye akarudi vipi Jamali una wasi wasi na mimi rafiki yako??"

"hapana nakuamini Brown"
Alisema Jamali huku akiwa hana amani kabisa moyoni mwqke General Brown alitoa vichupa vidogo viwili kama zile chupa za perfume kisha kichupa kimoja akaanza kukipulizia chumbani humo 
"Vipi Brown chumba hakina harufu mbona unaa..."
Bwana Jamali hakumaliza kauli yake akawa ameweza kuanguka chini Haraka sana Brown akatoa sindqno kisha akavuta dawa katika kile kichupa cha pili akamsogelea bwana Jamali ambaye macho yake yaliyokuwa yamelegea.....
"Brooown kweeeli unaniiiuwaaa?"
Kauli ya mwisho kutoka kwa bwana Jamali kauli aliyooitoa kwa shida tenw kwa sauti ya kilevi...
Naye General Brown hakujali kauli hiyo qlimsogelea na kumchoma sindano ya shingo sindano ya sumu sindano ambayo huwezi kupona hata kwa miujiza...
"safari njema Jamali"
Alitamka mqneno hqyo huku akioka katika chumba hicho cha bwana Jamali kwa tahadhari kubwa hukusahau kubeba vitu alivyotumia katika mauaji hayoo akatumia funguo ile kufunga chumba cha Jamali kisha akatoka......
Alipofika katka chumba chake akakusanya kila kilicho chake...
Ni kama alikumbuka kitu akfunguq begi lake nq kutoa kidonge kisha akakitafuna 
"daaah ningesahau kutafuna hiki kidonge na mimi ningelqla kama Jamali"
Alijisemea Brown huku akimalizia kufunga begi lake.......
Alitoka mpaka mapokezi kukabidhi funguo yake......
"thanks so much african girls sure i enjoy youre care"ahsanteni sana mabinti wa kiafrica hakika nimefurqhia huduma zenu"
Alisema brown huku akiwapatia funguo pamoja na dollar 100 ya kimarekkani yenye thamani ya laki moja....
"thanks too mr"
Mabinti wale wa mapokezi walimshukuru General Brown pasipo kujua ni mtu hatari sana alivyoondoka tu wakaanza mwmneno yao.......
"shost yaani wazungu wote wangekuwa hivi ingekuwa raha kweli kila sku tungekuwa tunakula madola tu"
Alisema mdada mmoja wapo wa mapikezi...
General Brown alipotoka nje tu Haraka sana aliondoka eneo hilo huku akiingia ndani ya gari lake ...
Dereva wa bwana Jamali aliweza kumshuhudia general Brown kwa mbali akiingia ndani ya gari lake na sasa alikuwa akiondoka mahali hapo 
"mmh huyu Brown amekuja saa ngapi?"
Alijiuliza dereva huyo huku akiwa na wasiwasi nq general Brown hakuangalia hata pleti namba za gari la general Brown.....
Alitoka ndani ya gari akaelekea mpaka mapokezi na kuomba kuonana na bwana Jamali.......
Mhudumu mmoja alinyanyua simu ya mezani kisha akabinyeza namba ya simu ya mezani iliyopo chumba alichokodi bwana Jamali........
Katika chumba cha bwqnq Jamali simu iliita pasipo kupokelewa kitu ambacho kilizidi kumuogopesha dereva wa bwana Jamali...
Mdada mmoja wapo wa.mapokezi akasimama ili aende kumgonge mlango......
Alifika aligonga sana mlango lakini wapi mlango haukufunguliwa na wala hakukuonekana kuwa kuna.uwepo wa ndani ya chumba hicho alirudi mapokezi na kumuelezea mwenzie...
"au amelala lakini ni kitu ambacho hakiwezakani hebu piga simu tena"
Alisema dada yule anayeonekana kumzidi mwenzie cheo naye yule dada akanyanyua mkonga wa simu akapiga lakini majibu yalikuwa yaleyale kama ya awali.........
"tufanyaje Loita??"
Aliuliza yule mdada mwenye cheo kikubwa kumzidi mwenzie.....
"tutumie master key tukaangalie huenda mtu akawa qmepatwq na mattizo"
Alishauri yule mdada anayeitwa Loita.....
Hawakupingana walimuita mlinzi mmojawapo wa hoteli hiyo kisha qkaongozana na Loita mpaka kqtika mlango wq chuma cha bwana Jamali.....
Yule dereva naye hakuwa mbali katika kutaka kushuhudia ni kipi kitakuwa kimemkumba boss wake......
Lolita ambaye ni yule mdada wa mapokezi alifungua mlango...
Alipiga kelele ambayo iliwashtua mlinzi pamoja na yule dereva wakaingia na wao ndani kushuhudi kuna nini kimejiri wote hawakuamini macho yao yalipotua juu ya mwili wa bwana Jamali aliyekuwa hana uhai huku damu iliyoambatana pamoja na povu ikiwa inatoka puani na mdomoni nishipa ya damu nayo ilipasuka na kutoa damu ambayo ilikua ni nyeusi tiiiii.....
Muhudumu yule ajulikanaye kwa jina la Lolita alikimbia mpaka mapokezi 
"ninii tenaaa mbona mkukumkuku"
Lolita Aliulizwa na mwenzie yulee wa mapokezi.
Ambaye alikuwa na shauku ya kutaka kujua kipi kimejiri
"yule mtu amekufaa yule wa chumba namba 99"
"ninii??? Hebu ngoja nitoe taarifa"
Kisha akabonyezbonyeza namba kwenye simu ya mezani simu ilipokelewa akasema jisi hali ilivyo
"okay tunakuja tupo njiani"
Ni sauti ya askari police......
Baada ya dakika kadhaa gari la polisi liliweza kutimu katika hoteli hiyo ya Singidian..........
Waliuchukua mwili wa bwana Jamali na kuelekea nao katika hospitali ya kituo cha polisi kwaajili ya uchunguzi zaidi........
*****Igunga yanayoendelea******
Masanja ambaye anajulikana kwa jina la Rocky akiwa pamoja na Lissa wakiwa katika ulinzi mkali wanaingizwa ndani ya chumba cha mahojino katika chumba ambacho ni Laizer na O.C.D Bihamunuro walikuwepo.....
Wqnafikishwa na kukaa katika upande wa pili wa meza wanatazamana uso kwa uso na Laizer pasipo kupepesa macho
"ndugu Masanja macho yako yananiambia kuwa unajifunza uharifu ilihali wewe si muharifu ni kweli si ndio??"
Alihoji Laizer huku akiwa kamkazia macho Rocky ambaye alionyesha mshangao tu...
ITAENDELEA........

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.