(Mmarekani mweusi)
Mtunzi:Nelson Kimoyi
Sehemu ya 28
#Endelea_nayoo>>>>>Walifika kituoni O.C.D Bihamunuro hakuwa mbali katika kuwapokea maaskari hao ambao walikuwa katika mission
Majangiri ya bwana Jamali yalupokelewa na maasikari wengine huku wale waliokuwa kwe nye mission wakatawnyika kupumzika........
Sasa alibaki Laizer pamoja nwa O.CD Bihamunuro wakiongea vitu vingi vinavyohusiana na kazi
"vipi sergeant Edwine yuko wapi"
Ni swali alilouliza Laizer huku O.C.D Bihamunuro hakusita kumwambia ukweli wote Laizer
"nilimkamata sahivi yupo sero kwahiyo nilikuwa nakusubiri wewe tu umuhoji"
"ookay ni kweli mkuu haujakosea basi acha nifanye leoleo.hiyo kazi ya kumuhoji maana kesho inatakiwa nikamilishe suala zima la kumtia mbaloni aliyempatia Edwine kazi lakini nilikuwa naomba maaskari wengine tofaut na wale wa mwanzo wakachukue maiti za majangiri walioweza kupatwa na mauti kule msituni"
O.C.D Bihamunuro hakuwa na pingamizi kwanza ukitegemea ni yeye pekee ndiye aliyemtoa Laizer Dar es salaam mpaka Tabora..................
******Katika chumba cha mahojiano******
Anaoneka Laizer pamoja na O.C.D Bihamunuro huku pembeni yao akiwepo sergeant Edwine hapakuwa na kelele ya aina yeyote katika chumba kile zaidi ya sauti ya Laizer.........
Katika meza iliyopo ndani ya chumba kile kulikuwa na vifaa vya kutesea watu ambao ni wabishi kusema ukweli
******Msitu uliiopo jirani na wilaya ya Igunga******
Jangiri mmoja anaonekana akichechemea ni baada ya kupata fahamu hakufa !!!! Hakufaa!!!! Aliondoka eneo la tukio huku simu ikiwa sikioni kuashiria kuwa kuna mtu anampigia anaamua kujificha katika kichaka ili aweze kuongea na simu hiyo
"haloo Mpuncho mbona kimya mumemmaliza huyo Mmarekani mweusi??"
Ni sauti ya bwna Jamali ndiyo iliyosikika katika simu ya mtu huyo anayechechemaa
"hapana boss wenzangu wameuwawa baadhi na wengine sielewi ni wapi wameelekea nimebaki mimi tu na ndo nimepata fahamu nachechemea hapa kwani nilipigwa risasi
Ilikuwa habari mbaya kwa bwana Jamali
******Jijini Dar es salaam******
General Brown akiwa yupo katika nyumba ya kukodi.........Anaamua kumpigia simu bwana Jamali baada ya kuona kimya kimekuwa kimya kwa bwana Jamali ili ajue kazi aliyoweza kumpatia amefikia wapi naye bwana Jamali alikuwa akizunguka katka sebule la nyumba yake akiwa anawaza atamjibu nini General Brown endapo akimpigia punde kidogo simu yake iliita kuashiria kuwa amepigiwa anaisogelea simu yake iliyokuwa juu ya meza na kuipokea
"haloo bwana Jamali mbona kimya sana umemaliza kaazi niliyokupa :- "
Ni sauti ya General Brown ndo iliyokuwa ikisika katika simu ya bwana Jamali
"daaaaah Brown kazi yako ngumu sana naomba unipe mda"
Aliongea Bwana Jamali kwa kujitetea pasipokujua kwamba maneno hayo yalimkera General Brown
"okay naomba tukutane singida nikuongeze pesa za kufanikisha kazi hii"
"sawasawa tukutane kesho asubuhi nitakuwa huko"
Kisha simu ikakatwa......
Upande wa General Brown alijikuta akifurahi kukubaliwa ombi lake la kukutana na bwana Jamali hakutaka kupoteza mda usiku huohuo akaanza kupanga nguo zake katika begi...
Wakati anaendelea kupanga nguo akaiona bastora yake
"naomba kesho usiniangushe namuua kupoteza ushahidi halafu nasepa zangu ulaya nikajipange upya"
Alisema Brown huku qkiibusu bastora yake....
ITAENDELEA............
Nini kitajiri hapo mbele usikose muendelezo wake