Notification texts go here Contact Us Buy Now!

BLACK AMERICA SEHEMU YA 27

RIWAYA:BLACK AMERICA
        (Mmarekani Mweusi)
MTUNZI:NELSON KIMOY
SIMU:0758638391
SIMU2:0625293917

{{ SEHEMU YA 27 }}
#Endelea_nayoo==>>Ndipo Laizer alipoweka target akiwa anamuona adui yake lakini yeye akiwa haonekani na adui yake.......
Laizer hakuwa na nia ya kumuua Rocky......
Wakati Rocky anaendelea kuangaza huku na kule kwa kutumia bunduki yake yenye lenzi alishangaa kuona lenzi ya bunduki yake ime7ambaratika..........
Hata Lissa mwenyewe alipigwa na bumbuwazi....
Laizer alikuwa akitabasamu tu kwani siku zote sniper hawezi kutumia bunduki yake pasipokuwa na lenzi....... Laizer akasimama kisha akamwambia asikari aliyekuwa naye

"fanya fasta twende hana ujanja tena yule"

Haraka sana wakasimama na kwenda katika lile hema na kujibanza kwa nyuma.......
Rocky baada ya kuona lenzi yake imesambaratika alianza kushuka kwenye mti kwa tahadhari kubwa huku akimsihi Lissa abaki

"baki huko huko ngoja nirudi ndani nikachkue lenzi narudi sahvi ila ukiona nimekawia ujue kuna tatizo limenisibu usisahau kuangalia kwa darubini sawa?"

"haya usijali ntafanya hivyo"

Rocky akashuka mpaka chini kwa mwendo wa kijeshi akaanza kusonga mbele kuelekea kwenye hema lao....
Laizer akiwa nyuma ya hema aliona ujio wa Rocky akiwa anakuja kwa kujibanza kwenye miti.....
Rocky alipohakikisha hakuna chochote katika hema lao alisogea mpaka katika uwanja wa hema lao akiwa bado anafanya uchunguzi alishtuka kuona watu wawili wamejitokeza huku wameshika bunduki kumuonyeshea yeye........
Lissa akiwa yupo juu ya mti aliweza kuona Rocky akiwa kawekwa chini ya ulinzi akaona ashuke akamsaidie kwani alikuwa na bastola.............
Wakati anashuka Laizer aliweza kumuona kupitia miwani yake ile ya kikompyuta hvyo Laizer alichokifanya ni kumsogelea Rocky kwa kasi ya fisi akamnyang'anya silaha yake kisha akamfunga pingu....... 
Lissa yeye bado alikuwa akihangaika kushuka kutoka juu ya mti.....
Laizer akiwa na askari wake wamchukua Rocky mkukumkuku mpaka kwenye vichaka ambavyo vilikuwa jirani na hema lile Lissa akiwa keshashuka kutoka juu ya mti na sasa alikuwa akikimbia kwa kasi kuelekea katika hema ambalo walikuwa wakiishi yeye na Rocky hakujua kama Laizer alikuwa akimuona kupitia miwani ya kikompyuta...... 
Sasa Lissa alikwishafika katika uwanja wa hema lao huku akiwa na hasira zilizojionyesha dhahiri kupitia macho yake........
Akiwa anaangalia huku na huku aliamua kuingia ndani huku akiita....

"Rocky? Rocky?"

Laizer alipoona Lissa akimuita Rocky alisogea mpaka nyuma ya hema kisha yeye ndiyo akaitika........ .

"yes dear"
 
"where you're? are you okay?"upo wapi? Uko salama?"

"yes im okay come outside"ndiyo niko salama njoo nje"

Lissa hakujua kama anajipeleka mtegoni naye alitoka pasipokuweka silaha yake mbele.....
Yaani alitoka huku akiwa amebweteka tu kweli Laizer alijua kucheza na akili za watu........
Ile Lissa ametoka tu nje alijikuta amebung1aa tu na asijue nini cha kufanya Laizer aliweza kumsogelea kisha akamnyang'anya Lissa bastola yake ile kisha akasema...

"we ni mwanamke najua huwezi kunifanya chochote haya ongoza njia"

Lissa hakutia ubishi ukitegemea mtu aliyemuona ni mtu aliyejazia mwili kwa mazoezi Laizer hata hakumuonyeshea Lissa bunduki aliongea katika microcheap 

"afande ambaye upo na mimi toka na huyo mwingine tukapande gari turudi wilayani"

Kelele za shangwe zilisikika masikioni mwa kila afande kwa kukamilisha mission hiyo iliyowasumbua vilivyo sasa Rocky pamoja na Lissa wakawa wamefungwa pingu kwa kuunganishwa mikono yao.......
Wakati wapo njiani walikuwa kimya kila mtu akiwaza lake ni Laizer ndiye aliyevunja ukimya huo

"hey mdungaji unaitwa nani vile?"

Rocky hata hakuwa na ubishi wowote wa kusema kwamba labda atakataa kujibu alimjibu Laizer kwa usahihi kabisa......

"naitwa Rocky Rodgers"

Jibu hilo lilimshangaza sana Laizer kwani hakutegemea kama mtu huyo angemjibu vizuri pasipokutia ngumu yeyote 

"good good napenda nikiwa namuuliza mtu awe ananijibu asijifanye gaidi haya na wewe pretty girl jina lako unaitwa nani?"

Lilikuwa ni swali lililomlenga Lissa......
Lissa alitafakari sana akafikiria kwa dakika chache lakini kabla hajajibu.....
Laizer alimuwahi kwa kumwambia...

"ukweli ndio utakaokuweka huru niambie tu ukweli unaitwa nani"

"naitwa Lissa Jensen"

"mmmh jensen jensen jensen"

Laizer liliwaza jina la Jensen amewahi kulisikia wapi alitafakari dakika tano nzima wakiwa bado wanatembea kuelekea kule ambapo wamewaacha maaskari wenzao......
Ni kama vile alikumbuka akamuuliza tena Lissa

"hivi unayemzungumzia ni Jensen yule billionea kijana wa General Brown Karly ama?"

"ndiyo huyo huyo hata hujakosea"

"okay sisi ni askari msiogope mpo katika mikono salama"

Rocky pamoja na Lissa hawakutegemea kauli nzuri kutoka kwa Laizer hatimaye walifika wakakuta mambazi wale bado wapo chini ya ulinzi waliwanyanyua na safari ya kurudi wilayani ikaanza
ITAENDELEAAAAAAAAA
Usikose Muendelezo wa riwaya hii

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.